Mrema kuwasilisha hoja binafsi

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,972
3,830
Sunday, 08 May 2011 21:00
Nora Damian
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Augustino Mrema, anatarajia kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu kufanyiwa marekebisho sheria zenye upungufu, ili kuzima mtandao wa ufisadi ulioenea nchini.
Mrema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), alisema miezi miwili aliyofanya kazi ameona iko haja ya kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria.
Alisema mojawapo ya sheria hizo, ni za utumishi ambazo nyingi zina upungufu, kwani zinamlinda mfanyakazi hata utaratibu wa kumshtaki unachukua muda mrefu.
Mbunge huyo alisema upungufu mwingi wa sheria hizo umeonekana kwenye adhabu wanazopewa watumishi wa serikali hasa wanapobainika kufuja fedha za umma. “Ukaguzi unafanyika miaka miwili baada ya ubadhirifu
kufanyika, yaani tunangojea mtu afe halafu ndiyo tufanye postmortem (uchunguzi) ,”alisema Mrema na kuongeza:
“Hata ukisema umsimamishe kazi hawezi kuona athari za kusimamishwa, kwa sababu sheria inamtaka mwaajiri atoe fungu na kumlipa kipindi atakachokuwa amemsimamisha.”
Alisema tatizo la ubadhirifu wa fedha serikalini ni kubwa, tena linatisha na kama hali hiyo ikiachwa iendelee nchi itakuwa ya walaji.“Ni aibu, baada ya miaka 50 ya uhuru bado taifa limejaa ufisadi, watumishi wengi wa serikali hawako kwa manufaa ya wananchi bali kutengeneza fedha,” alisema.
 
kila jitihada inahitajika mradi inuie kumkomboa mtz katika rindi la umasikini.
 
Back
Top Bottom