MREMA: Biashara ya kugombea Urais sina MTAJI nitamuunga mkono LOWASSA 2015!!

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Mwenyekiti wa TLP Agustino Lyatonga Mrema amesema kwamba hana mpango wa kugombea Urais 2015 kwani hana Mtaji na kuwa atamuunga mkono Mbunge wa Monduli na Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa kwani anauhakika wa MTAJI na kuwa stashinda.

Alisema kwamba yeye (Mrema) anaona biashara hiyo ya kugombea Urais inahitaji Mtaji mkubwa na kuwa yeye hataweza!

Source: Gazeti la Habari leo.
 
Huyu Mzee Kweli Kachoka.Yaani kugombea Urais imeshakuwa Biashara?.Namshauri arudi Rasmi CCM aache kuwadanganya Wanachama wa TLP kwamba naye ni Mpinzani.
 
Kaona ajaribu ufisadi,uzalendo haulipi bongo,sanasana utaishia kubebwa na kusukumwa kwenye gari,ila watu hao hao wanaoteswa na mfumo twawala huwa wa kwanza kuishabikia ccm baada ya kupewa elfu mbili,kofia,mataptap na fulana hongera mzee wa kiraracha kwa kutokuwa mnafiki.
 
habari leo ni gazeti la ma_ccm,sijajua kama credibility yake kama inakubalika na umma wa watz.
 
Kaona ajaribu ufisadi,uzalendo haulipi bongo,sanasana utaishia kubebwa na kusukumwa kwenye gari,ila watu hao hao wanaoteswa na mfumo twawala huwa wa kwanza kuishabikia ccm baada ya kupewa elfu mbili,kofia,mataptap na fulana hongera mzee wa kiraracha kwa kutokuwa mnafiki.

Mkuu nimecheka sana umeandika kiutu uzma halafu ukweli wa dhahiri kabisa.
 
Yeye akimuunga mkono kwani ana impact gani siku hizi?Kwanza ni lini alishawahi kuwa mpinzani?Hata 2010 alimuunga mkono JK aliyeponea chupuchupu

Asubiri kukiona cha moto jimbo la Vunjo

Hivi baada ya akina Ngawaiya na Tao hakuna vijana wenye akili ndani ya hicho chama wakapanga mapinduzi wamuondoe huyu mnafiki?Heshima ndogo niliyo nayo kwake inakaribia kuisha sasa!
 
Yeye akimuunga mkono kwani ana impact gani siku hizi?Kwanza ni lini alishawahi kuwa mpinzani?Hata 2010 alimuunga mkono JK aliyeponea chupuchupu

Asubiri kukiona cha moto jimbo la Vunjo

Ben hebu twende kwenye reality unaamini 2010 padri slaa alishinda? Usiongee kishabiki wala kinafiki achana pia na propaganda zile za kujifariji
 
kwa sasa hana chake, maana kariba mpya ndo inamtoa kwenye systeam kiulaini
 
yeye akimuunga mkono kwani ana impact gani siku hizi?kwanza ni lini alishawahi kuwa mpinzani?hata 2010 alimuunga mkono jk aliyeponea chupuchupu

asubiri kukiona cha moto jimbo la vunjo

hivi baada ya akina ngawaiya na tao hakuna vijana wenye akili ndani ya hicho chama wakapanga mapinduzi wamuondoe huyu mnafiki?heshima ndogo niliyo nayo kwake inakaribia kuisha sasa!
doogo vp ile kitu bado unayo mende na panya bado wananisumbua hp ss?
 
Mrema njaa imemlegeza moja kwa moja,
AMEKUMBWA NA TUFANI YA NAMNA GANI LAKINI??

I THINK ANASUBIRI KUZIKWA TUH SASA...
 
Back
Top Bottom