Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mwenyekiti wa bodi ya Parole, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labor Party (TLP) Augustine Mrema ameunyooshea kidole mpango wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa kufanya maandamano nchi mzima Septemba 1,kupitia Operesheni waliyoipa jina la UKUTA.
Akizungumza muda mfupi baada ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kutangaza kuvialika vyama vya siasa kwenye Baraza la vyama vya siasa kwa lengo la kufanya mazungumzo kuhusu hali ya kisiasa nchini, Mrema amekosoa mpango huo akidai umelenga kuwabembeleza Chadema.
Chanzo ar24