Mrejesho wa Zoezi la Kutoa Tabasamu Tarehe 24 Desemba

Mrejesho wa Zoezi la Kutoa Tabasamu Tarehe 24 Desemba

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,449
Reaction score
2,496
Nilikuja na post Zawadi yangu ya kuzaliwa: Kuwapa wengine tabasamu

Jioni ya juzi, tarehe 24 Desemba, nilihitimisha safari yangu ya kuwasaidia familia kadhaa. Ingawa hazikuwa nyingi, familia wachache tulizozitembelea walifurahia msaada wetu. Kila familia ilipokea mchele, sukari, na kuku mmoja mmoja. (Hawa kuku walitolewa na mdau mmoja hapa JF, na mimi nilienda pamoja na ndugu yake.)


Pia tuligawa zawadi chache za nguo; baadhi nilinunua kutoka karume mtumba lakini nzuri, na wadau wengine pia walichangia. Kwa kifupi, kila kitu kilikwenda vizuri, na mimi nilienda na marafiki zangu wanne. Zoezi hili lilikamilika kwa 100%.


Miongoni mwa familia tulizotembelea, nilikutana na mama mmoja aliye na watoto watatu ambao wanalala chumba kimoja kidogo sana, wakiwa chini. Rafiki zangu na mimi tumejichangia ili wiki hii au ijayo tumnunulie godoro kwa ajili yao. Ikiwa kuna mtu ana kitanda cha 5/6 na anataka kushiriki kuwapa tabasamu, karibu sana. Pia kama ni fundi wa fanicha unaweza kututengenezea kwa bei rahisi, itakuwa sehemu ya sadaka yako, nitafurahi sana. Tunaweza kuwasiliana kupitia namba ya 0797779091 au PM ili kupanga namna ya kutoa msaada.


Pia, kuna mdau mmoja alinicheki awali akaniambia ana nguo na anataka nifuate ili atoe maelekezo. Nilipofika, hakupokea simu, baada ya kupiga mara kadhaa alizima simu. Baadaye sana alikuja kuniambia alipitiwa na kazi na kuahidi siku ya kwenda atakuja. Tukamsubiri sehemu fulani tulikaasana nikampigia anasema nipo karibu nakuja, karibu saa moja, kisha tukaacha tukaamua kuondoka hajatokea wala hakupiga simu hadi leo hadi leo sijajua lengo lake lilikuwa nini. Ni mwana JF mwenzetu, na bado hali hii nimebakiza kidogo na maswali.


Kwa jumla, zoezi hili limefanikiwa sana, na shukrani zangu kubwa kwa kila mdau aliyechangia.
 
Mkuu endelea kufanya kitu moyo unataka mimi pia huwa nafanya hivo mwaka huu imekuwa ngumu sana kwangu usikate tamaa endelea kuku
 
Back
Top Bottom