Mrejesho wa safari ya treni kwenda Moshi full bata

Kwani mkuu linaenda na kurudi? Au linaruka siku moja?
Mkuu tena hili limependwa sana na wafanyabishara wengi kwani limepunguza badget yao angalia hili

Anafanya kazi zake mchana anasafiri jioni Moshi(kashafunga kazi) anabooking class ya kulala (kaokoa hela ya guest tayari hapo) anafika asubuhi mapema ananunua biashara zake jioni anarudi nalo anafika asubuhi anafungua biashara zake akiwa hana hata chembe ya uchovu
Hiyo nifaida au hasara?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usafiri poa kabisa huu na hauna bugudha kama mabasi.
Nipo mkoani mwanza muda huu ila nipo mbioni kurudi Moro. Nikiifikiria safari yangu wakati wa kuja huku ilikuwa kero tupu. Nilipanda Abood kila mkikaribia mizani wanapunguza abiria kama 15 mnapakiwa kwenye bajaj kutangulizwa mbele, gari likitoka mizani linawakuta mbele mnapanda tena kuendelea na safari! maajabu gari iko levelsit lakini wakipima kwenye mzani eti linaonekana uzito umezidi!! Halafu sikufurahishwa na mwendo wa driver ulikuwa wa kibangebange utafikiri kabeba mihogo.

Nimepanga nikifika mwanza mjini nikaulizie usafiri wa "jongoo" 2nd class to moro ni bei gani na litachukua siku ngapi?

Hili la moshi mpaka nawaonea gere...!!
 
Sawa meneja mauzo TRC... Tumekupata.
Kwanza kabisa napenda kuishukuru serikali kwa kufufua shirika la reli Tanzania na pongezi kwa shirika hilo TRC kwani kazi waliyoifanya ni kubwa sana kulinganisha na watu wanavyoropoka tu bila kushuhudia kwa macho.

SAFARI ILIANZA SAA 11 JIONI NA KUWASILI MOSHI SAA 1 ASUBUHI NA DK 20.

Usafiri wa treni ni mzuri sana na wataalamu wa safari wanaweka usafiri wa treni kuwa wa pili kiusalama baada ya anga. Ndani ya treni ya Deluxe kuna furaha kuna fursa nyingi sana (nitazielezq kwa uchache)
Nilipanda daraja la pili kukaa 23500/= mpaka Moshi kulinganisha na basi zaidi ya 30000.

Kama ilivyo hakuna sehem inayokosa kaubaguzi na changamoto za hapa na pale. Wale waliopanda daraja la 3 kukaa ni marufuku kuzunguka zuka huko ndani bila sababu maalumu,labda unaenda polisi, toilet au duka la dawa na bafet. Wakati kwanzia la pili kukaa unaweza kwenda popote yan unaweza kutalii huko ndani bila shida.

Bafet kuna vinywaji vyote na vyakula vyote na bei ni kama ya mtaani kulinganisha na kusafiri kwa basi kwanzia wali nyama 3000 chips kuku 4000
Muda wowote unachimba dawa sio mpaka mfike sehem flani
Kama umeenda kula unashauriwa ukimaliza uondoke mana nafasi za kukaa ni chache sana na huwezi kukaa hapo ukizuga na soda au maji hapo wanaopewa kipaumbele ni wanaopiga vyombo tu mana sio take away ka maji na soda

Asee hapo kuna raha yake na mzuka wake ni kama pub flan hivyo japo kuna taa lakini watu hawaogopi kabisa kusasambua kubambia(hakuna kupiga picha lakini) nilipenda sana hii sehem,kuna watu wa kila aina na jamii tofauti wakibadilishana mawazo yan ni full mzuka sana.

CHANGAMOTO NI UKATAJI TIKETI KWA UPANDE WA DAR
Hapo lazma uwe na kitambulisho chochote au hata barua m/kiti wako wa mtaa kingine movement ya wasafiri kwa Dec ni kubwa sana TRC wanapaswa kujipanga vya kutosha kwan wanapaswa kuweka hata treni mbili yan kila siku kuwe na usafiri.

FURSA KWENYE TRENI HII HAPA
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweka ATM mule ndani au Mawakala wa mitandao. Yan mtu anapiga kilaji mpaka ela inakata ana ela kwenye acc yake ya bank au mtandaoni anatoaje ili aendelee kutumia? Kilichobak hapo ni kubadilishana elfu 10 kwa elfu 8
Cha kusikitisha hii mitandao inapaswa kujiongeze waweke huduma ya "lipa kwa..." Na matangazo ya kutosha.

NENO LANGU KWA TRC DAR - MOSHI
ningependa kuwashauri watenganishe muziki wa bafet na wa kwenye behewa mana kuna mzuka wake.
KARIBUNI WADAU KUBORESHE SHIRIKA LETU View attachment 1327496View attachment 1327497View attachment 1327510View attachment 1327512

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazingatie usafi wa vyoo.
20191221_173334.jpeg
20191221_174418.jpeg
20191221_173430.jpeg
20191221_185909.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu una-assume kwamba nimeuliza swali wakati najua jibu.., nimeuliza kutaka kujua muda wa train na basi kwa safari hizo ili nifanye upembuzi yakinifu.., sababu muda pia ni muhimu sana kwa watu na sio wote wanaenda kuchukua mizigo, ingawa all in all train itasaidia sana kama wataongeza mabehewa ya mizigo sababu ni cost effective na itapunguza uharibifu wa barabara...
Bus masaa 10. Treni masaa 14.
Faida za treni
1.masaa 14 usiku umelala ukifika asubuhi unafanya kitu chochote utakacho. Bus utafika jioni au usiku biashara zimefungwa.
2. Treni utafanya utakacho asubuhi,mchana then jioni unaondoka. Bus utalala ukiamka ndio uanze shughuli zako ukimaliza hamna bus hadi Kesho tena ndio utaweza kuondoka.
Treni inaokoa muda kiujumla
 
Honestly natamani sana kulipanda. Christmas ya 2019 nilikaushia ikapita. Ya mwaka huu haitapita hivihivi
At first nilikua nauponda huu usafiri ila later niliupenda balaa baada ya kuona clips mbalimbali. This December ni must

Sent using Jamii Forums mobile app

For the first time nimepanda hii delux kipindi kile ndo inaingia nilitoka mwanza kuja dar second class ilikuwa ni 47500 behewa zima tulikuwa 9 tu watu wakaja kuongezeka tulipofika tabora

Jaribu mkuu ni usafiri mzuri sana kama unapenda adventure na kujua maeneo nilipita kilosa sehemu ambayo sikujua kama ntakuja kupita very amazing try it

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama mtu sio mtumiaji wa pombe atakaa wapi? Au kuna mahali pakunywea kwa watumiaji tu? Na jee hapo uliposema kuna chumba una lala kabisa ila ni watu sita ni mchanganyiko wa ke na me au? Natamani kweli kulipanda

Kuna bafeti kama bar kwa upande wa first class ile ya kulala chumba jinsia haichanganywi kama wanaume wanaume na wanawake pia hukaa peke yao

Ila hii first class sio nzuri kama unapenda kujichanganya na ku enjoy chukua second class

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu pitia njia ya Arusha mpka moshi ulipande hakuna usumbufu
Usafiri poa kabisa huu na hauna bugudha kama mabasi.
Nipo mkoani mwanza muda huu ila nipo mbioni kurudi Moro. Nikiifikiria safari yangu wakati wa kuja huku ilikuwa kero tupu. Nilipanda Abood kila mkikaribia mizani wanapunguza abiria kama 15 mnapakiwa kwenye bajaj kutangulizwa mbele, gari likitoka mizani linawakuta mbele mnapanda tena kuendelea na safari! maajabu gari iko levelsit lakini wakipima kwenye mzani eti linaonekana uzito umezidi!! Halafu sikufurahishwa na mwendo wa driver ulikuwa wa kibangebange utafikiri kabeba mihogo.

Nimepanga nikifika mwanza mjini nikaulizie usafiri wa "jongoo" 2nd class to moro ni bei gani na litachukua siku ngapi?

Hili la moshi mpaka nawaonea gere...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mk
Kwanza kabisa napenda kuishukuru serikali kwa kufufua shirika la reli Tanzania na pongezi kwa shirika hilo TRC kwani kazi waliyoifanya ni kubwa sana kulinganisha na watu wanavyoropoka tu bila kushuhudia kwa macho.

SAFARI ILIANZA SAA 11 JIONI NA KUWASILI MOSHI SAA 1 ASUBUHI NA DK 20.

Usafiri wa treni ni mzuri sana na wataalamu wa safari wanaweka usafiri wa treni kuwa wa pili kiusalama baada ya anga. Ndani ya treni ya Deluxe kuna furaha kuna fursa nyingi sana (nitazielezq kwa uchache)
Nilipanda daraja la pili kukaa 23500/= mpaka Moshi kulinganisha na basi zaidi ya 30000.

Kama ilivyo hakuna sehem inayokosa kaubaguzi na changamoto za hapa na pale. Wale waliopanda daraja la 3 kukaa ni marufuku kuzunguka zuka huko ndani bila sababu maalumu,labda unaenda polisi, toilet au duka la dawa na bafet. Wakati kwanzia la pili kukaa unaweza kwenda popote yan unaweza kutalii huko ndani bila shida.

Bafet kuna vinywaji vyote na vyakula vyote na bei ni kama ya mtaani kulinganisha na kusafiri kwa basi kwanzia wali nyama 3000 chips kuku 4000
Muda wowote unachimba dawa sio mpaka mfike sehem flani
Kama umeenda kula unashauriwa ukimaliza uondoke mana nafasi za kukaa ni chache sana na huwezi kukaa hapo ukizuga na soda au maji hapo wanaopewa kipaumbele ni wanaopiga vyombo tu mana sio take away ka maji na soda

Asee hapo kuna raha yake na mzuka wake ni kama pub flan hivyo japo kuna taa lakini watu hawaogopi kabisa kusasambua kubambia(hakuna kupiga picha lakini) nilipenda sana hii sehem,kuna watu wa kila aina na jamii tofauti wakibadilishana mawazo yan ni full mzuka sana.

CHANGAMOTO NI UKATAJI TIKETI KWA UPANDE WA DAR
Hapo lazma uwe na kitambulisho chochote au hata barua m/kiti wako wa mtaa kingine movement ya wasafiri kwa Dec ni kubwa sana TRC wanapaswa kujipanga vya kutosha kwan wanapaswa kuweka hata treni mbili yan kila siku kuwe na usafiri.

FURSA KWENYE TRENI HII HAPA
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweka ATM mule ndani au Mawakala wa mitandao. Yan mtu anapiga kilaji mpaka ela inakata ana ela kwenye acc yake ya bank au mtandaoni anatoaje ili aendelee kutumia? Kilichobak hapo ni kubadilishana elfu 10 kwa elfu 8
Cha kusikitisha hii mitandao inapaswa kujiongeze waweke huduma ya "lipa kwa..." Na matangazo ya kutosha.

NENO LANGU KWA TRC DAR - MOSHI
ningependa kuwashauri watenganishe muziki wa bafet na wa kwenye behewa mana kuna mzuka wake.
KARIBUNI WADAU KUBORESHE SHIRIKA LETU View attachment 1327496View attachment 1327497View attachment 1327510View attachment 1327512

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umenena.ila kuna wapinga kila jambo hata vivuli vyao watakuja kuleta maneno.wapotezeee
 
Back
Top Bottom