Mrejesho wa safari ya treni kwenda Moshi full bata

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,997
Kwanza kabisa napenda kuishukuru serikali kwa kufufua shirika la reli Tanzania na pongezi kwa shirika hilo TRC kwani kazi waliyoifanya ni kubwa sana kulinganisha na watu wanavyoropoka tu bila kushuhudia kwa macho.

SAFARI ILIANZA SAA 11 JIONI NA KUWASILI MOSHI SAA 1 ASUBUHI NA DK 20.

Usafiri wa treni ni mzuri sana na wataalamu wa safari wanaweka usafiri wa treni kuwa wa pili kiusalama baada ya anga. Ndani ya treni ya Deluxe kuna furaha kuna fursa nyingi sana (nitazielezq kwa uchache)
Nilipanda daraja la pili kukaa 23500/= mpaka Moshi kulinganisha na basi zaidi ya 30000.

Kama ilivyo hakuna sehem inayokosa kaubaguzi na changamoto za hapa na pale. Wale waliopanda daraja la 3 kukaa ni marufuku kuzunguka zuka huko ndani bila sababu maalumu,labda unaenda polisi, toilet au duka la dawa na bafet. Wakati kwanzia la pili kukaa unaweza kwenda popote yan unaweza kutalii huko ndani bila shida.

Bafet kuna vinywaji vyote na vyakula vyote na bei ni kama ya mtaani kulinganisha na kusafiri kwa basi kwanzia wali nyama 3000 chips kuku 4000
Muda wowote unachimba dawa sio mpaka mfike sehem flani
Kama umeenda kula unashauriwa ukimaliza uondoke mana nafasi za kukaa ni chache sana na huwezi kukaa hapo ukizuga na soda au maji hapo wanaopewa kipaumbele ni wanaopiga vyombo tu mana sio take away ka maji na soda

Asee hapo kuna raha yake na mzuka wake ni kama pub flan hivyo japo kuna taa lakini watu hawaogopi kabisa kusasambua kubambia(hakuna kupiga picha lakini) nilipenda sana hii sehem,kuna watu wa kila aina na jamii tofauti wakibadilishana mawazo yan ni full mzuka sana.

CHANGAMOTO NI UKATAJI TIKETI KWA UPANDE WA DAR
Hapo lazma uwe na kitambulisho chochote au hata barua m/kiti wako wa mtaa kingine movement ya wasafiri kwa Dec ni kubwa sana TRC wanapaswa kujipanga vya kutosha kwan wanapaswa kuweka hata treni mbili yan kila siku kuwe na usafiri.

FURSA KWENYE TRENI HII HAPA
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweka ATM mule ndani au Mawakala wa mitandao. Yan mtu anapiga kilaji mpaka ela inakata ana ela kwenye acc yake ya bank au mtandaoni anatoaje ili aendelee kutumia? Kilichobak hapo ni kubadilishana elfu 10 kwa elfu 8
Cha kusikitisha hii mitandao inapaswa kujiongeze waweke huduma ya "lipa kwa..." Na matangazo ya kutosha.

NENO LANGU KWA TRC DAR - MOSHI
ningependa kuwashauri watenganishe muziki wa bafet na wa kwenye behewa mana kuna mzuka wake.
KARIBUNI WADAU KUBORESHE SHIRIKA LETU
IMG_20200103_191004_0~2.jpeg
1579262247627.jpeg
1579262313796.jpeg
1579167347724.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
muda basi vs train ni masaa mangapi ?

Hii sana sana wakitaka kusaidia watu ni kuongeza mabehewa ya mizigo, pia kumbuka hauna haja ya kushukuru sana hii ni haki yako wewe unayetoa kodi na kama uwezekano upo wapate faida kwenye mizigo na nauli bado wapunguze kulingana na kipato cha mlalahoi,
 
Unaenda kupumzika unakimbilia wap? Kwanini uwe na haraka kama unaoga nje?

Wasafiri wote wanaenda kupumzika ? Au unadhani mahitaji yako ni sawa na ya kila mtu ?
Unasahau needs and wants zinatofautiana na katika hizo needs muda pia ni determinant..

By the way jifunze kujibu maswali..., swali ni muda wa train na basi upoje sio kuwahi au kuchelewa kwa mtu aendae kupumzika
 
Mkuu tena hili limependwa sana na wafanyabishara wengi kwani limepunguza badget yao angalia hili

Anafanya kazi zake mchana anasafiri jioni Moshi(kashafunga kazi) anabooking class ya kulala (kaokoa hela ya guest tayari hapo) anafika asubuhi mapema ananunua biashara zake jioni anarudi nalo anafika asubuhi anafungua biashara zake akiwa hana hata chembe ya uchovu
Hiyo nifaida au hasara?
Wasafiri wote wanaenda kupumzika ? Au unadhani mahitaji yako ni sawa na ya kila mtu ?
Unasahau needs and wants zinatofautiana na katika hizo needs muda pia ni determinant..

By the way jifunze kujibu maswali..., swali ni muda wa train na basi upoje sio kuwahi au kuchelewa kwa mtu aendaye kupumzika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tena hili limependwa sana na wafanyabishara wengi kwani limepunguza badget yao angalia hili

Anafanya kazi zake mchana anasafiri jioni Moshi(kashafunga kazi) anabooking class ya kulala (kaokoa hela ya guest tayari hapo) anafika asubuhi mapema ananunua biashara zake jioni anarudi nalo anafika asubuhi anafungua biashara zake akiwa hana hata chembe ya uchovu
Hiyo nifaida au hasara?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu una-assume kwamba nimeuliza swali wakati najua jibu.., nimeuliza kutaka kujua muda wa train na basi kwa safari hizo ili nifanye upembuzi yakinifu.., sababu muda pia ni muhimu sana kwa watu na sio wote wanaenda kuchukua mizigo, ingawa all in all train itasaidia sana kama wataongeza mabehewa ya mizigo sababu ni cost effective na itapunguza uharibifu wa barabara...
 
Samahani kwa kukuelewa vibaya mkuu. Pia mm kabla sijasafiri nilikua na godoro la nchi 10 ft 5 kwa 6 nilienda kwenye transport mbalimbali kuuliza garma ya kulibeba nikaambiwa bei ya mwisho ni 30k

Nimeenda TRC bei ilikua ni 11k tu angalia tofauti ingine tena hiyo kwenye mizigo
Mkuu una-assume kwamba nimeuliza swali wakati najua jibu.., nimeuliza kutaka kujua muda wa train na basi kwa safari hizo ili nifanye upembuzi yakinifu.., sababu muda pia ni muhimu sana kwa watu na sio wote wanaenda kuchukua mizigo, ingawa all in all train itasaidia sana kama wataongeza mabehewa ya mizigo sababu ni cost effective na itapunguza uharibifu wa barabara...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom