MONA WA KYEN
JF-Expert Member
- Dec 23, 2016
- 340
- 271
Wakuu naamini mnaendelea vema na majukumu
nakumbuka mapema mwezi januari nilileta uzi hapa kuhusu kuhitaji msaada kwani tulikuwa na safari ya kwenda india kumsindikiza ndugu yangu aliekuwa na tatizo la figo.
Ninapenda kuwashukuru wanajamii forum wote kwa michango yenu mizuri ya mawazo yenye tija katika ule uzi. Kiufupi utaratibu wa serikali ni kwamba alitakiwa kwenda mgonjwa na donor halafu baadae ndo angetakiwa kwenda msindikizaji ambaye ndie mimi.
KUELEKEA INDIA
Katika safari hii ya india walienda yule ndugu yangu pamoja na donor wake. siku hiyo waliondoka ghafla kwani walikuwa wamechelewa ndege kutokana na utaratibu wa serikali kuwa mrefu kidogo na wao kuchelewa kuukamilisha mapema pamoja na changamoto mbalimbali za wafanyakazi wa wizara ya afya waliokuwa wanashughulikia hilo swala lao.
Katika hiyo siku waliondoka ghafla na nilitamani sana kuprint angalau comment zenu hapa nimpe aende nazo lakini ilishindikana kwani tangu anatoka wizarani siku hiyo ilikuwa tunakimbizana na wakati kumsaidia asichelewe ndege.
KUWASILI INDIA NA KWENDA HOSPITALI
walifika salama salimini huko india na walifanyiwa vipimo upya huko hospitali ya APPOLO NEW DELH India na ikawa imehakikiwa kuwa alikuwa na tatizo la figo na alitakiwa kubadilishiwa nyingine kama vipimo vya hospitali za hapa nyumbani Tanzania vilivyoonesha.
Wakati nikisubiri kwenda nilijulishwa na wao kuwa ubalozi wa Tanzania kule India uliwataarifu kuwa asingehitajika msindikizaji kwani kuna ma-nesi wa kutosha kuwahudumia kwa hiyo safari yangu ya India ikawa imeisha pale.
OPARESHENI
Ndugu yangu alifanyiwa oparesheni kwa mafanikio makubwa.
KUWASILI NYUMBANI NA HALI YA MGONJWA
Ndugu zangu hawa donor pamoja na alikuwa mgonjwa wote waliwasili nyumbani tarehe 25/04/2017, akitanguliwa na donor maana hali yake pamoja na mgonjwa ilionekana kutengemaa.
Ninapenda kumshukuru Mungu sana kwa ajili ya ndugu yangu huyu kwani maendeleo yake ni mazuri mno na vidonda alivyokuwa navyo miguuni hapo mwanzo vimekauka kabisa. anaonekana mwenye furaha iliyopitiliza tofauti na mwanzoni alikuwa ni mtu mwenye hasira kila dakika. Afya yake imeimarika sana kiukweli tumefarijika mno na hali yake.
Ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa wanajamvi wote kwa ushauri wenu, ninapenda kuishikuru serikali kwa msaada wao mkubwa maana gharama za zaidi ya milioni mia moja tusiweza kuzimudu. asanteni sana wote waliohusika Mungu awabariki