Mrejesho: Nimesaidiwa nauli ya chuo

Mrejesho: Nimesaidiwa nauli ya chuo

Huyo aliyekuuliza ati mwamaume unaomba alijua wewe ni mwanamke atumie fursa hiyo kukutongoza akukule kisa una shida.
Aisee dada zetu wanapitia changamoto kama hizo mkuu,Mungu awape hekima wawe na misimamo yenye busara zaidi
 
Pole sana msomi bahati mbaya mi sikuona Uzi wako uliyo omba msaada binafsi nimeguswa na shida yako naomba ukiweza kunitumia Namba yako inbox nikutumie mchango mdogo niliokuwa nao.
Hata namba ya mtu unaemwamini kuwa atakufikishia sadaka yangu.
Mwenyezi Mungu akujalie ufanye vizuri kwenye mtihani wako.
Amen mkuu,ndio nimemaliza leo mitihani
 
Good luck kijana
Mola awe nawe.

Nilisoma uzi wako.. Ila huo wa nauli sikuona.Waweza kutu PM wengine na mie.. siku moja chochote kitusaidia pahala

chuma cha mjerumani
Uliona juu ya nauli nakumbuka ulitaka kweli kujua anaendeleaje na maisha yake.
Amen mkuu, kiukweli haikuwahi kutokea situation kama hii ila Nashukuru MUNGU alitatua tatizo kupitia watu wake na leo ndio nimemaliza mitihani ubarikiwe sana mkuu
 
[HASHTAG]positive[/HASHTAG] #is [HASHTAG]normal[/HASHTAG] binadamu tunamatatizo kama Mimi tatizo langu kusahau.
MTU akikwambia atakupa Tafu uwe unamcheki PM ata salamu atakumbuka. Usikae kimyaa mdogo wangu.
Amen mkuu, shukrani hata kwa moyo uliounyesha kikukweli haikuwahi kunitokea hali kama hii hata siku moja huko nyuma ila sponsor wangu ambaye alijitolea kunililipia kila kitu kwa mwezi huu hakuwa vizuri kabisa nilijaribu njia zote mtaani hata kuuza simu yangu pia ilishindikana, Nashukuru kwa moyo uliokuwa nao mkuu Mungu akubariki sana nimemaliza leo mitihani mkuu
 
Kila lakheri, MUNGU akutangulie katika masomo yako, na hatimae ufikie malengo yako na wewe uweze kuwasaidia wengine wenye uhitaji.
 
Kila la kheri katika masomo yako ndugu. Kama ikitokea shida yeyote Mkuu nicheki inbox, tutagawana umaskini nitakachokuwa nacho
Ameen mkuu, shukrani sana naamini ilikuwa ni kipindi cha mpito tu,ubarikiwe sana kwa moyo uliokuwa nao mkuu, shukrani sana mkuu
 
Nimefarijika kuona hata sasa kuna watu bado wana mioyo safi ya kusaidiana. Ndio hivyo tu maisha bado hayajaninyokea ningetoa chochote kitu.
Usijali mkuu,Ipo siku tu,Kwa moyo huo tu uliounyesha MUNGU ameshakubariki ,sometimes maisha huwa yanapanda na kushuka mkuu coz hata mimi sikuwahi kufikiria kama siku moja ingetokea situation kama hii mpaka kukosa hata nauli tu
 
Back
Top Bottom