Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Hili swala ni nyeti sana, tuache ushabiki wazazi wangetaka kujua mwenye ujauzito wa mdogo mtu wangesemaje? Mtoto akishazaliwa angefichwa babake au ingekuaje?
Leah alikua sahihi kabisa kushirikisha wazazi wa pande zote pia walezi/ waliowafungisha hii ndoa.
Mdogo mtu asingekua mjamzito ni kweli angemwondoa tu kisha wao wakayazungumza maisha yakaendelea bila wazazi wala ndugu.
Msimtetee huyu mharibifu jamani kama mna mabinti mtajaona siku wakijatendwa kama haya kua kumbe si vizuri.
Wewe ndiye uache kuchanganya vitu hapa jamvini. Matatizo yalikuwa:-
i. Fumanizi kati ya kidume na mkewe
ii. Kutundikwa mimba dogo na shemejie
iii. dogo kutembea na mume wa leah

Siamini katika masuala ya ujumla kila kosa lazima liwe na mshitaki na mshitakiwa. Hivyo leah hakuwa na mamlaka ya kushitaki kuwa dogo kapata mimba. Hayo yalikuwa ya kwao. Yeye alitakiwa avae i&iii tu

Jamaa kaichukulia poa sana hii issue kama vile ni sawa tu mume kuzaa na mke wa mdogo wake😡😡😡😡
Inategemea ni kabila ipo maana makabila mengine kama mke wako hakupata mtoto unaletewa mdogo wake au akifa dada dogo anachukua usukani.
 
Wewe ndiye uache kuchanganya vitu hapa jamvini. Matatizo yalikuwa:-
i. Fumanizi kati ya kidume na mkewe
ii. Kutundikwa mimba dogo na shemejie
iii. dogo kutembea na mume wa leah

Siamini katika masuala ya ujumla kila kosa lazima liwe na mshitaki na mshitakiwa. Hivyo leah hakuwa na mamlaka ya kushitaki kuwa dogo kapata mimba. Hayo yalikuwa ya kwao. Yeye alitakiwa avae i&iii tu

Inategemea ni kabila ipo maana makabila mengine kama mke wako hakupata mtoto unaletewa mdogo wake au akifa dada dogo anachukua usukani.
Hapo ndipo ufahamu wako ulipoishia?
 
Habari zenu wadau wa MMU,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru mods na members wenzangu wote kwa mawazo, ushauri na michango yenu katika thread niliyoleta huku kipindi cha nyuma yenye kichwa kisemacho "mume wangu amempa mimba mdogo wangu"

Nimepata muda wa kutosha kutafakari michango ya mawazo yenu namna ya kumaliza tatizo hili na MUNGU amekuwa upande wangu na nimefanikiwa kufikia muafaka.

Jana ndo ilikuwa siku ya kukutana tena kwenye kikao pamoja na wazazi wa pande zote mbili na safari hii tukihusisha na wachungaji wetu na tulikaa na kufikia muafaka kama ifuatavyo;

Katika kusikiliza maelezo ya pande zote mbili yaani kutoka kwangu na kwa watuhumiwa, mume wangu aliamua kujibu vibaya kikao baada ya kuona anaandamwa na maswali ambayo haya kumfurahisha.

Nasikitika kusema alidiriki kujibu kuwa kama kosa limeshatokea waamue haraka yeye ana mambo ya muhimu ya kufanya kuliko hili.

Akaenda mbali zaidi kuwa hata wao wanajiona ni watakatifu kumuandama na maswali wana nyumba ndogo kibao sema ni kwa vile hawaja kamatwa. Pamoja nahayo akaongeza kuwa hajawahi jutia kosa lake kwani yule si dada yake wala hana ukoo nae kwahiyo ilikuwa ni sawa tu.

Wazazi wake walijaribu kumkatisha asiendelee kuzungumza lkn hakujali akapaza sauti zaid hapo ikabidi wamuache tu aongee mpaka amalize, aliongea mengi na magumu sana sina ujasiri wa kuyaandika hapa kwakuwa hayatamkiki kwa mtu mwenye akili timamu.

Baada ya kumsikiliza kikao kiliniuliza nasemaje kuhusu ndoa yangu.

Sikuwa na la zaidi, niliwaambia kwakuwa kwake ni jambo la kawaida sana na mimi kwangu si la kawaida nisingeweza kuendelea kuishi na mtu mwenye mtazamo tofauti.

Wachungaji walisema wao hawana mamlaka ya kuvunja ndoa ya kikristo lakini kwakuwa mwanaume ameongea maneno yenye dharau inaonesha hana moyo wa toba na angeendelea na uzinzi hivyo wanaungana na mimi katika maamuzi yangu.
Walinishauri nifuate taratibu za kisheria kuvunja ndoa.

Kwa upande wa mdogo wangu yeye alishanifuata zaidi ya Mara kumi kuniomba msamaha, sikuona sababu ya kutomsamehe nilimsamehe na jana niliuthibitisha msamaha wangu katika kikao lakini nilimtahadharisha kutoendelea na shemeji yake nae hakupingana nami katika hilo.

Mwanaume ameanza vitisho kwamba nijiandae kupambana.
Binafsi siogopi nipo tayari kupambana lakini sipo tayari kuendelea kuishi na mwanaume fedhuli kama yeye.

Hapo ndipo tulipo fikia na najiandaa kutafuta talaka kisheria.

Asanteni sana naamini hili limepita imebaki utekelezaji wa utenguzi wa ndoa.

Nakaribisha michango yenu ya mawazo..

Pia niwashukuru kwa kampani yenu katika kipindi kigumu
Usifanye hivyo Mkuu acha kabisa kutamka neno TALAKA ni hatari,yaani unaachana na mme wako sababu kamla mdogo wako?,mbona ni sawa mmeo kacheza uwanja wa nyumbani kuliko angekula mtu baki hapo ingekuwa vibaya sanaaaa,mdogo wako kakusaidia kazi za ndani,ni sawa sawa na kumpa mtoto mchanga ambebe wakati wewe unapika haina tofauti au siyo?,.Sababu ulichonacho wewe na mdogo wako anacho na vyote vina damu aina moja,USIACHIKE TAFADHALI TENA MPE ZAWADI MDOGO WAKO KWA KUKUCHUNGIA MALI ZAKO.
 
Kama kinaweza kusemwa hapa nisingekuwa na haja ya kukuomba unipm ndiyo maana nikasema hivyo leah2.
Sasa amekwambia sema hapa hapa na wewe unahororoja,sema upesi weweeee,domo zege ila kumtukana MH LOWASSA NDIO ULIKUA BINGWA Simiyu yenuuuuu?
 
Usifanye hivyo Mkuu acha kabisa kutamka neno TALAKA ni hatari,yaani unaachana na mme wako sababu kamla mdogo wako?,mbona ni sawa mmeo kacheza uwanja wa nyumbani kuliko angekula mtu baki hapo ingekuwa vibaya sanaaaa,mdogo wako kakusaidia kazi za ndani,ni sawa sawa na kumpa mtoto mchanga ambebe wakati wewe unapika haina tofauti au siyo?,.Sababu ulichonacho wewe na mdogo wako anacho na vyote vina damu aina moja,USIACHIKE TAFADHALI TENA MPE ZAWADI MDOGO WAKO KWA KUKUCHUNGIA MALI ZAKO.
Eti eeh! Kweli dunia ina watu wenye akili tofauti...malizia bia yako ukalale umeshalewa
 
Wewe ndiye uache kuchanganya vitu hapa jamvini. Matatizo yalikuwa:-
i. Fumanizi kati ya kidume na mkewe
ii. Kutundikwa mimba dogo na shemejie
iii. dogo kutembea na mume wa leah

Siamini katika masuala ya ujumla kila kosa lazima liwe na mshitaki na mshitakiwa. Hivyo leah hakuwa na mamlaka ya kushitaki kuwa dogo kapata mimba. Hayo yalikuwa ya kwao. Yeye alitakiwa avae i&iii tu

Inategemea ni kabila ipo maana makabila mengine kama mke wako hakupata mtoto unaletewa mdogo wake au akifa dada dogo anachukua usukani.
Subiri mkeo apewe mimba Na kakako ndo huo utaratibu utaufuata huyu kamua kama aonavyo yeye
 
Leah wewe ni mwanamke mzuri mwenye busara ninakuombea uweze kupata mwanamme mzuri wa kukuoa tena. Mimi ningekuwa niko teyari ningtupa karata yangu lakini kwa sasa siko teyari, Wanaume wote siyo wabaya ukiomba Mungu atakupa Mwanamme mzuri. Ninakushauri angalau utafute mwenye kadgree angalau. Education matters a lot in relationship To share your vision with your partner who is not educated becomes difficult sometimes. Ninakutakia kila la heri na ni tumaini langu kwamba the next husband will be super husband.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom