Mrejesho: Mboga yangu ya jana

Mrejesho: Mboga yangu ya jana

The List

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2017
Posts
1,741
Reaction score
4,944
Wengi mmeniomba sana tena sana kwamba nilete mrejesho tukio liliendaje, kuhusu binti aliyekula laki nne yangu ndani ya mwezi bila kumega. Na mm bila hiana ninawapa MAAJABU aliyokuja nayo.

Baada ya kufika tu kiumbe yule alifika kwa table na kama gentleman nikampokea mixer mate kidogo(ingawa nilinyonya kwa hasira nusu nimkaushe maji mwilini). Baada ya kinywaj na kuagiza msos sababu eneo lile lilikuwa na band pale alisimama kwenda kucheza. Wakati huo naendelea kupewa ushauri na ndugu zangu(JF) namna ya kumu assasinate huyu kiumbe.

Chakula kikafika tukala huku akijiongelesha ongelesha tu mm moyoni nimejaaa hasira nikiwaza pesa zangu. Ktk stori kwny hali ya kushangaza alianza kunieleza vitu ambavyo sikufikir kuvisikia kwake?akaanza na historia za macharii waliomtenda, na kusema ANANIPENDA SANA MM na kwamba NI MWANAUME WA KIPEKEE MAISHANI MWAKE. Wakati akieleza hayo mara akaniambia kuwa kwakuwa sijawai kufika kwake siku iyo angependa tukalale kwake, OMG moyo ukalipuka!!! Kikubwa mtoto akasema gharama za vyakula na vinywaj atalipia yeye. Kimkojo cha furaha kidogo kitoke.

Kwa maongezi yake yale nikajikuta moyo wng unamuelewa sana huyu mwanamke, na stori zake mpaka analia nikajikuta nalia nae na mm. Kwa kweli kwa hasira za kuzungushwa na kupigwa virungu vya tarakimu 5 ziliisha kabisa. Tulimaliza kula tukacheza muziki kisha tukamaliza payment(akalipa yeye kama 210000 maana alinirudishia na ya taxi. Sikujivunga nikachukua na kuweka mfukoni apo nikapiga hesabu imebaki namdai kama 190,000.

Basi tukachukua ndinga pale kuondoka kama saa nane kasoro mpakaa kwake akampa wa taxi kama 30000 ivi. Yaani apo kidume sielewi elewi. Mara ndani mzee, mara bafuni mtoto maasharah habibu raalata. Wazee kuna viumbe vilvyobarikiwa.

Mambo yakaanzia kule mpaka kitandani. Yaani nilikuwa nimetulia kiumbe anawajibika. Acha kabisa wazee mengine tukiandika tutapigwa ban!!.

Asubuhi kani suprise huyu mtoto zaid baada kutoa nguo mpya tshirt, jeans, boxer na rabba mpya adidas new, yaani nikaambiwa hizo za jana acha nizifue. Hela yangu imerudi yote na bonus juuuu.

Sasa hapa nipo kwenye gari narudi geto maana nina michongo ya kipesa leo nafikiria alichoniambia jana yule mtoto ANATAKA AHAMIE KWANGU AU MIMI NIHAMIE KWAKE NA KWAMBA ANATAKA JUMAPILI NIKAMUONE MAMA YAKE MKUBWA ALIYEPO MJINI APA. MTOTO ANATAKA JIBU LEO

wakuu nishaurini asee maana naona kama nauziwa tango pori au ni ndoto au mazingaombwe fulani, vipi mtoto ahamie geto na nikajitambulishe jumapili iyo???
 
Tuliza munkari mkuu, nenda taratibu kabla kufanya uamuzi. Hivyo vimambo vya cku moja visije kuharibia maisha yako yote ukajaregret! Nenda taratibu
 
Ndege mjanja hunaswa kwenye Tundu bovu. Itafakari saana kauli hii....
Sijakuelewa mkuu, una maana gani asee. Niweke wazi na ushauri yaani mwenyew naona mauza uza tu
 
We jamaa, kirahisirahisi hivyo? Msomane kwanza

Kada wa kwenye CCM mpya
Mkuu ndio mwenyew nashindwa uyu manzi!!jana nilipania nimtafune kulipizia hela yangu kumbe yenyew ina habar kama hizi za kuish pampja
 
Kinachonishangaza kaletewa raba,jinz,tshirt na demu ambae sidhani kama alikuwa hata anajua saizi ya vitu anavyovaa jamaa
Usishangae hilo dingi, huyu manzi nimeanza kuifatilia mwezi na kitu saiv na mpaka jana kuonana apo katikati nishaonanaa na outing kidogo., ingawa kitisheti killipwaya kidogo lakini imefit
 
Mkuu ulikua Bar gani...? Calabash au...?
Kama niliwaona hivi.
1502514998245.png


Mkuu chimbo unalijua hili
 
Kijana usiharakishe kwenda kwa wazazi wake. Swali la msingi la kujiuliza ni je, uko tayari kuwa mume na kuwajibika kama mume? Maana ukishaoa inabidi uwe na uwezo wa kutimiza majukumu ya ndoa (si ngono). Sasa kama ulishajiandaa kisaikolojia, na una chochote kitu cha kumtunza ,swali la pili huyo binti umejipa muda wa kumjua na kuona kama anafaa kuwa mke wako? Maana si kila binti anaweza kuwa make wako japo kila mwanamke anafaa kuolewa.
Ndoa ni issue mtambuka kaka jiridhishe ndg yangu ILA USIOGOPE WALA KUOGOPESHWA HAKUNA EXPERIENCE YA MAISHA YA NDOA KILA NDOA INA CHANGAMOTO YAKE TOFAUTI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom