Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Narudi tena kuomba ufafanuzi kwa wadau. Naomba kueleweshwa hapa. Kisheria, mali ambayo mwanandoa amekukuta nayo say kiwanja/ shamba haihesabiki kama sehemu ya mali ya wanandoa? Kuna ahadi fulani husemwa kanisani (baadhi ya dini za kikristo) kuwa " nakushirikisha kwa mwili wangu na Mali zangu za duniani" hii huwa ni Mali zipi kama sio ulizonazo kabla ya ya ahadi?. Tafadhali naomba ufafanuzi kwa wajuzi.
 
pole sana. ila kesi kama yako mahakama ya wilaya ndio mpango mzima. haki ingetendeka vzr. kuliko za mwanzo. ila mungu atakusaidia ndiyo dunia.
 
pole sana. ila kesi kama yako mahakama ya wilaya ndio mpango mzima. haki ingetendeka vzr. kuliko za mwanzo. ila mungu atakusaidia ndiyo dunia.[/QUOTE
Asante ndugu yangu nina mpango wa kuomba wapeleke kesi mahakama ya wilaya nikiona wanazingua
 
Mali alizokukuta nazo ukiwa umezipata kabla ya ndoa hazimhusu, hizo ni mali zako mwenyewe na ni bora ukazichukua mapema ziwe chini ya himaya na uthibiti wako kabla hazijapotea.Hii hahitijiki kusubiri talaka itoke.
 
Hiyo ndoa yako ngumu kama ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, pole sana dada....I think sometimes wanaume tuna roho ngumu sana...ingawa hatuwezi kuhukumu moja kwa moja upande mmoja, mmeo tungemsikia nae tungeweza ku-balance mzani!
 
kwanza pole sana dada......komaaa tuu......huyo member aliekusaidia ni wa jinsia gani?:wacko:
 
Habari za asubuhi wana JF

Mwezi wa saba nilipost mkasa kuhusu matatizo na mume wangu https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/876139-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu-10.html

Baada ya kupata ushauri kutoka kwa wana JF, ndugu zangu na upande wa mume niliamua kuongea naye kuhusu tabia zake, lakini hakuweza kubadilika. Siku moja aliondoka kwenda Msata kama alivyodai mwezi mzima bila kuaga wala kujua naishije pale nyumbani. Siku zote hizo hakuwa anapiga simu mpaka mimi ndio nimpigie.

Nilichukua uamuzi wa kumuomba baba yake amuite ili tuweze kuyaongea kama familia zote mbili. Baba aliitisha kikao cha kukutana na familia za pande zote lakini alikataa kuja na kusema mimi niondoke pale nyumbani na asinikute maana ataniumiza.

Nikaamuakupeleka shauri baraza la kata kwasababu imeshindikana kwa ngazi ya familia. Kata nako aliitwa mara tatu lakini hakufika. Kumbe siku zote hizo yuko hapahapa Dar anaishi na yule mwanamke ambaye alimtambulisha polisi kama mke wake na pia alishawahi kumleta pale myumbani.

Mimi nikachukua uamuzi wa kuondoka pale nyumbani chini ya mjumbe na mjomba wake nikaenda kwa dada yangu. Siku hiyo naondoka nilikutana naye njiani anarudi nyumbani akiwa na yule mwanamke, kumbe alimuambia mjomba wake akiondoka tu mke wangu uniambie mimi niko karibu nitakuja.

Alipofika pale nyumbani siku ileile aliondoka na vitu vyote pale nyumbani na akaweka mpangaji baada ya siku mbili yeye akaondoka akarudi kwa yule mwanamke. Jana baraza la kata limenipa barua ya kwenda mahakamani kudai talaka na madai mengine baada ya huyu mwanaume kushindwa kutoa ushirikano baraza la kata.

Nimeshafungua kesi mahakama ya mwanzo na leo ndio taandikiwa wito wa kumuita mahakamani. Pamoja na kupangisha nyumba ambayo tumejenga wote bila ridhaa yangu pia aliondoka na gari yangu.

Nawashukuru sana wana JF kwa michango yenu, pia na member mmoja ambaye amekuwa msaada mkubwa kwangu mpaka nafikia hatua hii. Michango yenu ni muhimu sana hasa kipindi hiki cha kudai haki yangu.

Asanteni sana

Mungu awabariki sana

Sasa kuwa mjanja usikubali kudanganywa maana, mwanaume alikuacha hivyo ww bado unampenda so chunga sana usidangaywe kurudiana maana hakuna mme hapo, ukikubali, pia kubali kufa au kuchanganyikiwa ili lengo lake litimie, hapo unatakiwa ukumbuke yy hakupend sasa, kw hiyo akitaka kuludiana jua hapo ni gelesha tu mama'; kuwa mjanja hiyo hatua uliyofikia usiubali ushauli oote ule kwa mtu yyte
 
Dada yangu; Gari hilo litakuwa sehemu ya mgao na nyumba pia itakuwa sehemu ya mgao. lakini kama mna watoto nyumba haitagawanywa kwa mtu yoyote yule. Mahakama itaamua ni nani ataishi na watoto kweny hiyo nyumba. Ila kama hakuna watoto, itagawanya au wafanye estimates halafu huyo jamaa akulipe portion of you contribution. trust me; gari hilo litakuwa sehemu ya division coz lilinunuliwa wakati mko kwenye ndoa regrdless where the cash/proceeds come from. I was in the same situation; Trust me, wakati mahakama watakapo toa samons, najua huyu jamaa hatofika mahakamani. you will come back n tell me. Kwa hiyo jiandae jinsi ya kukabiliana na huyo jamaa endapo kama atakataa/kutotoa ushirikiano kuja mahakamani.

kasema gari alimkutanalo KABLA HAWAJAOANA' so halipo ktkt mgao kabisa. iyo gari nyingine ni ya ofisi so haihusiki pia.over!
 
Pole sana hivi dunia ya leo mwanamke wa nje ni wa kuchanganya mpaka umtende mke yote hayo
Kwasababu umeshapita baraza kesi iko wazi talaka itatolewa na kama Nyumba mliipata mkiwa kwenye ndoa itagawanywa kwa wote ikijumuishwa na mali nyingine mlizochuma mkiwa ndani ya ndoa, kama mna watoto basi itaachwa kwaajili ya watoto.
Dunia itamfunza.
 
Back
Top Bottom