Kama ukifuga kienyeji unaweza usipande majani maalumu kwa chakula chao, lakini ukitaka kufuga kisasa na kwa malengo maalumu ya biashara ni lazima upate mbegu nzuri za majani. mbuzi wanakula aina nyingi za majani miti, hivyo eneo lenye vichaka linafaa sana kwa mbuzi,na ndo maana unaona sehemu kame mbuzi wanaishi.
Mkuranga kuna chatu wale wadogo, ni vizuri kuchoma hilo eneo ili kuwafukuza kama wapo, mimi walinyonga mbuzi 11 hivi wakati naanza. Na kama utafuga huria, inabidi uwe makini, mbuzi wanazurura sana kwa hiyo eka 30 kwa mbuzi huria inabidi usiwe na jirani mkorofi. Vijito vyenye maji ya kudumu kule Mkuranga vina mamba na chatu hukaa kando ya vijito hivyo.
bado vibaka sio wengi inategemea uko Mkuranga ipi. Mhimu, mtafute LAT akupe majina ya mbegu bora za majani ili uoteshe ktk shamba hilo.