Mrejesho kuhusu online dating

thewajibu

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2017
Posts
236
Reaction score
312
Kwanza kabisa nianze kwa kusema naunga mkono kutafuta mchumba mtandaoni kwa sababu huu ndo wakati wake kama wazazi wetu walipopiga safari ndefu kuwatafuta wenzi wao mbaali wengine hata wakikutana na wachawi na bwimbwanga usiku kucha sasa tumeshatoka huko..

Pili wanawake tunaowaona mitandaoni ni walewale tunaopishana nao mtaani, madukani, kwenye daladala na kwingine tofauti hatujui wanawaza nini lakini wakiwa kwenye dating site huelezea hisia zao. Huenda hata binti mrembo uliekaa nae siti moja leo huenda ni mwana jf mzuri tu.

Tatu naunga mkono kuoa mwanamke bara lolote nchi yoyote au kabila lotote kwa sababu siwezi mpangia mipaka mungu kwamba anipe mke kutoka mahali fulani tu watu wote ni wake naruhusiwa kuchagua popote na nchi yoyote.

Mrejesho wa victoriahearts.com siku kazaa zilizopita mtu mmoja alitaka kujua wapi anaweza kupata mzungu wa kuoa mmoja kampendekezea tovuti hiyo niseme tovuti hiyo ni waongo kwa sababu kwanza mtandao huo umefichwa unaendesha huduma kutoka wapi

Pili nilipojiunga huko kufanya utafiti nilipata jumbe nyingi sana za mahaba kutoka kwa wasichana nilichoshangaa watawezaje kumpenda mtu ambaye hata hajaweka profile pic baadae nikagundua ni mchezo wa kutafuta pesa kila ujunbe wanakata 2 credit kutuma email 10 credit kuangalia video credit kazaa pia na nilikuwa na credit 20 ambazo ilibidi nizitumie kutuma message tu ili zisiishe bila utafiti wangu kukamilika

Pia ilinibidi kutojibu kila ujumbe isipokuwa wa mtu mmoja pekee ili nikamilishe mpango wangu mwisho nikamwomba jina fb akasema hana skype hana email hamna nikagundua huenda nachati na mtu aliye kwenye ajira yake.

Nikapita reddit na quora ndipo nikakuta watu walioibiwa mamia kwa maelfu ya dola kwenye mtandao huo bila mafanikio yoyote tafadhari usiuunguze pesa yako hapo.

Hitimisho: Hata hivyo kuna dating site za ukweli ambazo unaweza kupata mwenzi wako lakini kutongoza hakukwepeki kwenye site hizo utakuta kila mwanamke wazungu, wachina, waarabu nk wanaopenda kuolewa Africa Wanaopanga kuja kujitolea Africa ni wewe na voko zako hata hivyo utalazimika kupekuwa mamia kwa maelfu ya profile kumpata.
 
watu siku hiz hawaogopi hawa wanawake wa mitandaoni siku hiz kuna matukio mengi ya ajabu siku utakapokuja katwa nyeti au kuibiwa kabisa ndo utajifunza
kukatwa nyeti hata jirani yako anaweza fanya hivyo mkuu ukifuata masharti ya uchumba haiwezi tokea
 
natoa hizo dating site lkn pm pekee kwa sababu si kila mtu anazihitaji hapa
 
eharmony.com imefungisha ndoa 600000 4% ya ndoa USA wamekutana hapa lkn kuona picha lazima uwe umelipia. internationalcupid.com ni ya bure ugumu wake watu ni wengi sana kwa sababu hawalipii utapekuwa sana kumpata k
 
huo mtandao wa victoriahearts.com wengi wa wanawake wapo Russia na Ukraine sijui kwa nn
 
Wakuu ingieni pia www.dating.mobi wako njema sana pia.Pale hata kuweka picha yako lazima wa confirm kama ni wewe kweli.Hakuna kuweka picha ya mtu mwingine kule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…