Mrejesho: Kilimo cha mpunga Bahi

Kwa hesabu zako wastani wa kulima kwa heka ni kama TZS 600,000 kwa gunia 10 za debe 7 ambazo kila debe ni kama kg20 so ni sawa ni sawa na tani 1 na nusu.Kwa hivyo wastani wa kulima ni laki 4 kwa tani moja ?(KILIMO CHA KWENYE MAKARATASI) Je naweza tumia hii kama makadirio au muongozo?

Na ukileta sokoni ukauzi kila kilo TZS 12000 unapata threefolds in 120 days?
 
Nimepitia maswali na majibu humu nimeona bora kilimo cha nyanya mara pengine kuliko mpunga. Sijawahi kulima mpunga, ila mwaka jana nilijaribisha kulima nyanya kwa eneo km nusu eka. Nikapata tenga 142. Niliuza kwa bei tatu. Nilianza kwa sh 60000, baadae ikashuka kidogo 55000, bei ya mwisho nikauza 45000. Mwisho nikitoa gharama zote nilibakiwa na mil5+
 
Nimelima heka 4 msimu huu huko morogoro nimeambulia gunia 9 tu. Nikipiga hesabu ya gharama niliyotumia kwenye kilimo nasikia hasira tu.

Ila sijakata tamaa hapa nabadilisha uelekeo tu naenda kulima mbeya safari hii ila nitaongeza idadi ya heka.

Kuna sehemu wanapaita Kapunga ndio Nina mpango wa kwenda kulima msimu ujao.
 
Ulitumia gharama kias gan kulima
 
Mimi Nalima Viaz mviringo Njombe lkn Miaka ya nyuma nmewahi enda kulima mpunga chimala-kapunga. Nilicho gundua n kwamba mpunga unapolima inatakiwa uwe na alternative mvua ikifel unafungulia maji ya kumwagilia hapo 100% unatoboa. Generally agriculture pays!!
 
Kama umeweka picha ya magunia 50 haina shida kabisa mkuu
 
Daah yaani mkuu kigwangala anatisha.

Niliona na ana ng'ombe pia anapiga mnada.


Wenzetu wanafaulu coz wana mitaji ya kutosha aisee.
Yes mitaji mikubwa pia ana wasiwasi hata akipoteza mil 100 kwasababu baada ya miezi mi5 kashaipata tena ila sie hatuwezi kuwekeza hata mil 5 kwenye kilimo maana ukipoteza kuipata tena ni issue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…