Mrejesho: Forex ya Ontario

Majaribu2013

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
952
1,043
Kijana mdogo ONTARIO aliyejizolea jina kubwa na hata kubadili jina lake na kuwa Mkuu na Chief akiiitwa na watu wa rika mbalimbali wazee kwa vijana. Kijana huyu ameleta sauti za matumaini kubwa miongoni mwa watu wengi, binafsi nampongeza sana kwa jitihada alizozionyesha.

Bila shaka mpaka sasa zaidi ya watu 500 watakuwa wamepata mafunzo kutoka kwa kampuni yake ya TMT (The Million Team). Nashukuru kuwa amewahi kuleta ushahidi wa mafanikio hapa jukwaani japo angali kwa watu wachache.

Uzi huu unalenga kuitisha mrejesho huru usiofungamana na UPANDE wa TMT bali uwe huru kwa maana ya kwamba wanufaika wote watupw mrejesho. Bahati nzuri asilimia zaidi ya sabini ni wanachama humu. Natarajia kuwa zaidi ya wanufaika mia tatu wamo humu. Idadi hii ni kubwa sana nilitarajia tuanze kuona thread za members wengi zikibadilika humu kutoka kulia maisha magumu na kulia kwa furaha za mafanikio.

Hebu ninaomba wanufaika wote tuje hapa tutoe mrejesho huru usiopendelea, kama umenufaika au umenusurika. Mrejesho huu pia unaweza kutoa taswira juu ya biashara hii kwa wakati ujao. Kumbuka watu wengi wakiishia kulalamika kwa kuliwa serikali sikivu ikisikia itajua ni utapeli na itafunga, hivyo natumaini pia kuwa mrejesho huu utanufaisha TMT kwa kuchukua hatua za kuboresha ama kuharibu kutokana na ubora kuzidi.

Asante
Majaribu2013
Mtoto wa Ontario.
 
Back
Top Bottom