Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Hongera boss.

Ila sisi vijana huwez kutuona kwenye thread kama hizi, ila za mateso mtu anayopitia ndipo utakukuta huko, au tuliyempekua tukakuta sintofahamu( utapeli) ndio utatukuta huko, pengine hapa tumekupekua thread zote na comment zako zote humu tukakuta hauna chembe ya utapeli, kwahio huwez kutuona wengi ndio mana unaona ndani ya masaa 17 kuna comment 5 tu.

Ila naamini ume inspire wale wenye mlengo wa kuingia huko kwenye dhahabu.

Wangari Maathai umeona hii?
Chief umenena kisawasawa
 
Hongera sana mkuu mm n mpambanaji mwenye mtaji mdogo tu ila najitahid kusafir hapa napale na biashara pia nanunua mazao Kama ufuta korosho sometimes mahindi.

Je nataka kujua boss kwa mtu Kama mm ambaye nataka kufanikiwa pia nilete biashara gan hapo chunya machimbon ambayo inaujitaj Sana kwa wachimbaj na wanunuz kama nyie?

Naomba Sana mkuu nijibu hili nijue najipangaje.
 
Hongera sana mkuu mm n mpambanaji mwenye mtaji mdogo tu ila najitahid kusafir hapa napale na biashara pia nanunua mazao Kama ufuta korosho sometimes mahind

Je nataka kujua boss kwa mtu Kama mm ambaye nataka kufanikiwa pia nilete biashara gan hapo chunya machimbon ambayo inaujitaj Sana kwa wachimbaj na wanunuz kama nyie ?

Naomba Sana mkuu nijibu hili nijue najipangaje
Machimboni mkuu biashara zinazotembea Sana ni pombe na migahawa. Wachimbaji Wana kanuni ya kutumia pesa yote aliyopata siku hiyo kwenye vilevi na wanawake...

Nguo pia zinatembea ziwe za dukani au mitumba, hasa mitishet na majins. Pia zipo biashara ndogondogo kama kutembeza tikiti.

Tikiti ni Bonge la biashara mkuu maana wewe unanunua jumla ukifika mgodini unakuwa unakata vipande angalau nane na kimoja unauza miatano.

Faida unaweza lingana na mtaji na yanaenda sana kwa jua kali, hivyo unaweza jikuta kila baada ya siku tatu unashusha mzigo.

Mkuu biashara zipo lukuki Kama magenge ya kuuza mbogamboga na matunda. Fanya utembelee ili upate exposure zaidi mkuu.
 
Hongera sana mkuu kwa Biashara ya Madina minimum kwa kuanzia mtaji ni kama kiasi gani, na je changamoto kwa beginner mara nyingi huwa ni nini.
 
Iko ivii mkuu angalau ukiwa na milioni nne utaanza vizuri, ila mda mwingine inategemea na sehemu unaponunulia
Shukran mkuu. Je kwa mtu ambaye hana hufaham wowote na mambo ya Madini na anataka kufanya biashara unamshauri kitugani Cha kuzingatia.
 
Machimboni mkuu biashara zinazotembea Sana ni pombe na migahawa. Wachimbaji Wana kanuni ya kutumia pesa yote aliyopata siku hiyo kwenye vilevi na wanawake...

Nguo pia zinatembea ziwe za dukani au mitumba, hasa mitishet na majins. Pia zipo biashara ndogondogo kama kutembeza tikiti.

Tikiti ni Bonge la biashara mkuu maana wewe unanunua jumla ukifika mgodini unakuwa unakata vipande angalau nane na kimoja unauza miatano.

Faida unaweza lingana na mtaji na yanaenda sana kwa jua kali, hivyo unaweza jikuta kila baada ya siku tatu unashusha mzigo.

Mkuu biashara zipo lukuki Kama magenge ya kuuza mbogamboga na matunda. Fanya utembelee ili upate exposure zaidi mkuu.
Asante kwa majibu mujarab chief

Mwezi wa nane baada ya msimu wa ufuta nitakuja chunya mkuu nifanye utafit
 
Back
Top Bottom