Mrejesho: Biashara ya madini aina ya dhahabu

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
885
Habari za mda huu mabilionea wa sasa na wajao. Tumaini langu mnaendelea vema na harakati za kutimiza ndoto zenu.

Ni kama mwezi nilikuja kuomba msaada kwa wajasiliamali wenzangu juu ya biashara ya dhahabu. Nishukuru watu walitoa uzoefu wao, wapo walionitaadhalisha juu ya songombingo zilizopo kwenye biashara hiyo.

Wa kukatisha tamaa hawakosekani nao hawakuwa haba, ila tu nishukuru wapo memba walonitia moyo kwa kunishauri nini hasa nikifanye nikiwa mgeni kwenye kada hii ya madini.

Kwa sababu mtaji wangu ulikuwa around 5ml, niliamua kuanza na million 2 kwanza ili niusome upepo nikiwa najifunza. Kusema ukweli katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia nilipoanza hali ya kibiashara siyo mbaya.

Nimeweza kuisogeza milion 2 hadi 3 ndani ya mwezi. Hivyo nimepata faida ya million moja. Hii ni hatua nzuri kwangu kwa siku za mwanzo.

Pamoja na hayo tahadhar mimeweza kuichukua na naendelea kuichukua. Nimejiwekea sheria sinunui mawe, bali nanunu dhahabu iliyochomwa na kui-grade, hivyo probability ya kupoteza hela ni ndogo.

Changamoto pia nakutana nazo kama kupungua sana uzito ukipeleka jikoni kuyeyusha, asilimia ya dhahabu kusoma chini na wachimbaji wanaokuja kuchukua advance kisha wanapotea mazima hivyo hela kupotea.

Karibuni mabroker wenzangu tu share ups and down za hii biashara.

Biashara ya madini ya dhahabu.

1619588442416.png
 
Mie namuomba mtu mwenye mtaji wa kununua machine hii aje tuyajenge tuingie porini na baada week moja atakuja na mrejesho wenye furaha.

Angalizo sihitaji pesa zako ila nataka ukanunue machine mwenyewe then njoo twende wote maeneo yenye dhahabu.
Screenshot_20200630-115838_eBay.jpg
Screenshot_20200630-115523_eBay.jpg
 
Mkuu hiyo Mashine inauzwa sh ngapi na matumizi yake hasa ni yapi
Machine hii inauzwa kati milion 14 hadi 15 inategemea na inatoka nchi gani japo zipo ndogo 8m had 10m pia.

Machine hii kazi yake kubwa ni kudetect mahali ilipo dhahabu na kutoa mchoro wa 3d kama ambavyo geologist huwa wanaichora so ukiwa na hii machine utamaliza kila kitu, lakini pia utachimba mahali ambako tayri unauhakika na mali iko umbali gani na kuna mwamba wa aina gani au maji yapo ya ujazo upi na mali ipo ya ukubwa gani.

Faida kubwa ya hii machine ukiwa nayo hata mtu anaemiliki costar hapa hafui dafu maana wachimbaji wadogo wataacha kwenda kwa waganga wa kienyeji tayari wewe utakuwa mganga wao hivyo kwa week kutengeneza 5m sio shida kwa kuwapimia maeneo ya kuchimbia.

Faida nyingine wewe mwenyewe ukiwa na hii machine na unajuwa kuitumia ipasavyo na ukaunda kikundi cha kuchimba baada kupima hapa nahisi baada miezi leizer atakuja kukusalimia.

Mfano kigogo kuna jamaa ana machine moja ina uwezo wa kupima kwenda chini 1m tu lakini kwa mwezi hakosi 4m na kuendelea je hiyo ya 50m kwenda chini na mapana inapima 3000m huoni kuwa hapa hii italipa zaidi lakini bado itafanya vitu vingi kitaalamu.

Karibu sana kwa mtu yeyote mwenye mtaji sitaki hela ila naitaka hiyo machine tu kanunue mwenyewe uje nayo utakuja useme kwa nini nilichelewa namna hii
 
Nimependa idea.
 
Nicheki inbox bro tuyajenge kama upo serious lakini.
 
Macho mdiliko na wangari naomba kuwajibu kwa namna ambavyo mmetafsiri ninyi na nilitakiwa nisiwajibu chochote kwa sababu ya ufinyu wa mawazo yenu ila kwa sababu leo ni jumapili nimepoz ngoja nipoteze mda kuwajibu hili.

Kwanza kabisa mdau aliweka uzi kutoa ushuhuda wa kile anachokifanya naweza kusema uzi huu haukuwa na lengo la kumpiga mtu kwa sababu tayari aliwahi omba kupata utaratibu namna ya yeye kwenda huko kufanya biashara hii,

Biashara hii kwa wale walioko maeneo ya migodin wataelewa nini naongea na hasa kwa upande wa dhahabu ni biashara ambayo ukiwa makini na ukabahatika kulenga eneo lina dhahabu unaweza amka kwenda chimbo huna hata mia na ukarudi una mamilioni hili sio hadithi na tumeshudia wengi, lakini biashara hii ukiingia kichwa kichwa hata kama ungekuwa unamiliki ndege sita unaweza poteza zote na ukabaki masikini.

Kwa maelezo ya mleta uzi kuwa yeye ananunua tayari ikiwa imechomwa na kuiuza kwa makota na wao wanapeleka sokoni hili lipo wazi kuna faida tena ya wazi bila kificho ila ni mbaya kununua ile haijachomwa hapo unaweza nunua udongo.

Hivyo kwa mtaji wake wa milioni tano na kusema kwa mwezi kaingiza faida ya milioni moja mbona ni ndogo sana hiyo kwa biashara ya dhahabu tena hapo anaenda taratibu na kwa umakini mkubwa asije kupigwa.

Kuhusu mimi ndama dume kuomba mtu mwenye machine na sio pesa hili kwa akili yenu fupi mkadhani mtu atapigiwa wapi labda kwa sababu sisi hatuendi kuchimba sisi tunaenda kuwapimia watu maeneo na kulipwa chetu,

Pili unaweza kujiuliza kuwa kma machine hii ingekuwa na faida kiasi hicho watu wengi si wangekuwa nayo? Naomba nikujibu hivi kuwa asilimia kubwa ya wachimbaji hawana shule hapa nazungumzia wachimbaji wadogo na hivi vifaa kwao hawana utaalamu navyo hivyo wanachimba kwa kubuni na kudhani lakini hawana uhakika na kile kilichopo so hapa ndio sehemu geologist hupiga pesa ukipima eneo na mchimbaji akaja kuchimba kapata kitu basi juwa wote watahamia kwako kwa gharama yeyote ili ukawapimie maeneo.

Lakini kama hujui mazingira ya migodin yakoje na hukawahi kufika na kuona na haiba ya watu au wachimbaji wadogo wanahitaji nini basi unaweza dhani ni uongo ila ukweli ni kwamba watu wametoka na kunawiri zaidi nyie endeeleeni kucheza forex tu .
 
Back
Top Bottom