Mtukudzi
Senior Member
- Nov 14, 2013
- 103
- 408
Mh. Samia Suluhu aliposema KAZI IENDELEE alimaanisha mambo yote 'mazuri' yaendelee kama ilivyokuwa kwa hayati JPM. Tunatambua kuwa mojawapo ya 'kazi' ambazo zilikuwa zikiendelea kwa kasi hapa nchini ni pamoja na 'kuunga juhudi' za Mh. Rais. Sasa inakuwaje kazi hizi haziendelei?.
Je mratibu/waratibu wametingwa na shughuli za bunge au tuwaeleweje sasa? Kufuatia hotuba ya Madam President, kuna watu hasa viongozi wa vyama vya upinzani wamejitokeza hadharani kuonyesha wazi wanaunga mkono juhudi za Mh. Samia. Kwa nini waratibu wa zoezi la kuunga mkono juhudi hatuwaoni Channel Ten live kunako ofisi za Lumumba wakiendelea na kazi yao?.
Tumewaona Mh. Mbowe akikiri kuwa amelazimika kutoka Dubai kuja kutoa ushuhuda wa matendo makuu ya Madame President. Siyo huyo tu, Sugu amesema amesitisha azma yake ya kuhamishia biashara zake South Africa kwa kuwa Rais Samia amemkosha. Lema yuko tayari kurejea Tanzania.
Chonde chonde waratibu timizeni wajibu wenu. Unafuu wa safari hii waungaji mkono hawana gharama yoyote na hapahitajiki matumizi ya vitisho na ushawishi kama ambao Mh. Lema alidai kuwahi kufanyiwa na Mh. Bashiru Aly. Mkichelewa sana watajitokeza waratibu fake wawafanyie utapeli waungaji mkono.
Kazi iendelee..!