Mramba azidi kumkandamiza Mkapa mahakamani

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,003
Mramba azidi kumkandamiza Mkapa mahakamani
Thursday, 23 August 2012 20:19
Tausi Ally
Mwananchi

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha Basil Mramba, jana aliendelea kumkandamiza aliyekuwa bosi wake na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akimhusisha moja kwa moja na kutolewa kwa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers.

Mramba aliyaeleza hayo jana wakati akijitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni na kwamba alitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo ili kutekeleza matakwa ya mkataba.

Alidai kuwa kifungu cha 4.3.1 kilichopo kwenye mkataba huo ulioingiwa kati ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Alex Stewart Government Business Assayers kinasema malipo yoyote yatakayolipwa na mkataba huo hayatotozwa kodi.
"Mimi nilichofanya ni kutekeleza matakwa ya mkataba huu kwa sababu Waziri wa Fedha pekee ndiye mwenye mamlaka ya kutekeleza mkataba huo," alidai Mramba.

Mramba alikiri kuruhusu gavana wa BoT kuilipa kampuni ya Alex Stewart, Dola za Marekani 1 milioni kama malipo ya awali, kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ukaguzi wa migodi ya madini, na kwamba fedha nyingine zingelipwa kwa awamu.

Mramba alisema aliruhusu malipo hayo kufanyika kutokana na kuwapo kwa barua ya Mei 13, 2003, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Rais, Patrick Mombo kwenda kwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini kuhusu mkaguzi wa dhahabu ikisema "Rais amekubali Waziri wa Fedha na BoT watafute njia ya kuilipa kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers".

"Maagizo yote mimi niliyachukulia kama ni ya Rais, alikuwa akiagiza watendaji wake kutekeleza majukumu yote,"alisema Mramba na kuongeza kuwa kwa kuzingatia makubaliano hayo alitafuta fedha hizo kupitia bungeni katika Bajeti ya Serikali ya 2003/04.

Kuhusu mkataba, Mramba alisema kuwa anachofahamu yeye sheria ya BoT inampa mamlaka Gavana kuingia mikataba na kuisaini na kwamba mikataba yote aliyoingia na watu wengine ni lazima kodi isamehewe.

Mramba aliiambia mahakama hiyo kuwa, kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers ilikuwa ikitaka malipo bila kodi na kwamba, wao walikubali kutomtoza kodi kutokana na ushauri kutoka kwa wataalamu akiwamo gavana kuwa wamsamehe kodi vinginevyo wangemlipa zaidi.

Hata hivyo, alisema mkataba baina ya BoT na kampuni hiyo haukuwahi kupitia katika kikao cha Baraza la Mawaziri. "Sikudhani kama angeweza kutiliana nao saini kwenye mkataba huo, bila Baraza la Mawaziri kuridhia,"alisema Mramba.
Ushauri wa TRA

Mramba alibainisha kuwa Bethar Soka ambaye alikuwa kwenye kamati iliyofanya mchakato wa kuitafuta kampuni hiyo ya ukaguzi wa dhahabu, aliomba kupata kauli ya TRA kama kampuni ya Alex Stewart Government Bussines Assayers isamehewe kodi ama la, Mei 26, 2003.

Alidai kuwa baada ya Soka kupeleka ombi hilo Mei 26, 2003, TRA katika majibu yao ya Juni 24, 2003 walisema kuwa hawapendekezi mkaguzi huyo wa dhahabu asamehewe kodi na kwamba barua hiyo ilipelekwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wakati BoT na kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers iliingia mkataba Juni 14, 2003.

"Inaonyesha barua hiyo ya TRA ilichelewa kwa siku 10, baada ya mkataba kusainiwa, hata hivyo, ushauri huu wa TRA hatukuuhitaji hata kama ungekuja haungekuwa na manufaa," aliongeza kudai Mramba.

Baada ya maelezo hayo, mmoja wa wanaosikiliza kesi hiyo, Hakimu Saul Kinemela, alimuuliza Mramba, Wizara ya Fedha iliomba ushauri huo TRA kwa kazi gani?

Akijibu swali hilo, Mramba alisema, "Siyo Wizara ya Fedha iliomba ushauri TRA, bali Soka aliomba ushauri huo kama mwanakamati iliyokuwa ikifanya mchakato wa kutafuta kampuni hiyo na kwamba Soka yeye alikuwa ni mtumishi wa wizara yake.

Alibainisha kuwa Soka asingeweza kumshauri Waziri, anayeweza kumshauri ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu.

Mbali na Mramba, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.

Jaji John Utamwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu itakapoendelea na utetezi.
Utetezi wa awali

Mramba (71) alianza kujitetea, Agosti 22, mwaka huu ambapo alidai kuwa Serikali iliiteua BoT ifanye kazi ya kutafuta kampuni inayoweza kufanya kazi hiyo hivyo ikaingia mkataba na kampuni iliyochaguliwa ya Alex Stewart Government Bussines Assayers.

Waziri huyo wa zamani aliongeza kudai kuwa aliyeagiza BOT kufanya kazi hiyo ya kumtafuta mkaguzi wa dhahabu ni Rais wa Awamu ya Tatu, Mkapa na kwamba wakati huo yeye akiwa Waziri wa Wizara ya Fedha alipewa jukumu la kuhakikisha gharama za kumlipa mkaguzi huyo zinapatikana ndani ya Serikali au BoT ama pengine popote.

Alifafanua kuwa kati yake yeye na gavana hakuna aliyekuwa na mamlaka juu ya mwingine na kwamba gavana alikuwa na wajibu wa kufanya mchakato wa kumtafuta mkaguzi wa dhahabu.

Mramba alisisitiza kudai kuwa yeye hakuhusika kwenye mchakato huo kwa kumtafuta wala kumleta hapa nchini wala kumtuma mwakilishi yeyote kumwakilisha kwenye kamati iliyoteuliwa kufanya mchakato huo bali alipewa agizo la kumlipa.

"Mimi kama waziri sikuwa na mtu wangu kwenye ile kamati, lakini Wizara ilituma mwakilishi, ambaye alikuwa mwanasheria Bethar Soka wakati wa kuhoji kampuni mbili ili wachague na kwenye kujadili vipengele vya mkataba,"alisema.

Inadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14, mwaka 2004, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa watumishi wa umma, walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao waliipatia msamaha wa kodi isivyo halali, Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.

Yale yale ya "I was just taking orders",hakuna anayetaka kuwa accountable.
 
Haya sasa sinema ndio hiyo imeanza ninamuona Mkapa akijiandaa kwenda mahakamani na wasaidizi wake.
 
Kwa maelezo hayo bado sijaona pa kumlaumu Mkapa labda kama wanajamvi mtasema hakukuwa na umuhimu wa kumleta huyo mkaguzi

Sema huyu Mramba na Betha Soka ndo nahisi wamepiga dili hapo ukizingatia Betha alishiriki kwenye kumtafuta huyo mkaguzi halafu Mramba anautetea msamaha huyo kwamba upo kisheria na pia inaonekana aliuratibu yeye mwenyewe kwa kumtumia Betha Soka
 
Hivi maamuzi yakiwa ya rais inamaanisha kwamba ndio manake yapo RIGHT!!!

Tuliona yale yale kwenye kesi ya Mahalu I think tuanze na huyu Mkapa kwanza ili hawa wanaofuata watueleze vizuri.
 
Kauli ya amiri jeshi mkuu huwa inatekelezwa mara moja bila kuhoji. Na ukitaka kushinda kesi kama ilivyokuwa kwa mzee wa Italy basi wewe taja amiri jeshi mkuu
 
Haya sasa sinema ndio hiyo imeanza ninamuona Mkapa akijiandaa kwenda mahakamani na wasaidizi wake.

Ha ha ha ha ah! Lakini MKAPA ana KINGA YA KUTOKUSHTAKIWA KWA MUJIBU WA "KATBA". Hivi hamuoni huu mchezo CCM wanaowafanyia watanzania?

Yaani in short, wakubwa wanapanga haya madudu strategically, waiibie nchi then issue zikifutuka kama hivi, wasingizie ilikuwa ORDER kutoka juu wakijua vizuri (si walipanga wenyewe) kwamba huyo wa juu ana KINGA. Mkapa mwenyewe, Mramba, Yona, et. al wanajuai vizuri sana wanachokifanya na tusitegemee lolote.

Issue ya Mahalu ilikuwa hivi hivi - KINGA YA KUTOSHTAKIWA kwa Rais Mstaafu. Ukiona Rais au Rais Mstaafu anapandishwa kizimbani ujue mchezo umeisha, hakuna kesi hapo.

KATIBA MPYA izuie kabisa hii kitu inaitwa KINGA KWA RAIS MSTAAFU - ni ufisadi mtupu.
 
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Mramba, amesema kutokana na mkataba uliosainiwa na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali na Kampuni ya Alex Stewart, hakuwa na njia yeyote ya kukwepa kuondoa kodi kwa kampuni hiyo.
Mramba pia aliieleza mahakama kuwa, alipokea barua iliyotoka kwa Katibu wa Rais Benjamin Mkapa kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na nakala iliyokwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo, Andrew Chenge, ikiwataka kutafuta fedha za haraka kwa ajili ya kuilipa kampuni hiyo.
Hayo aliyaeleza jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, John Utumwa, wakati akitoa utetezi katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7, inayomkabili yeye na wenzake wawili.
Mramba alieleza kuwa, mkataba uliotiwa saini kati ya BoT na kampuni hiyo ulikuwa unambana kwa mujibu wa sheria ya mkataba huo kwani asingetoa msahama wa kodi, serikali ilitakiwa kumlipa fedha nyingi mwekezaji huyo.
Akiongozwa na wakili wake, Hulbert Nyange, aliyetaka kujua kama maagizo hayo yote aliyachukuliaje kama Waziri wa Fedha, Mramba alidai kuwa yalitolewa na Rais Mkapa katika dokezo mbalimbali akitaka utekelezaji wa kuilipa kampuni hiyo ufanyike haraka iwezekanavyo.
“Mimi sikuruhusu malipo yoyote wala punguzo lolote ila kwa mujibu wa kifungu cha 4 (3), kinasema malipo yoyote hayatatozwa kodi kwa mujibu wa mkataba huo kati ya BoT na Kampuni ya Stewart,” alidai Mramba.
Wakili Nyange alitaka kujua kama ni kweli Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walitoa ushauri kwa Wizara ya Fedha kuwa wasitoe msahama huo, ambapo alidai kwamba hakuuona ushauri huo.
Aliongeza kuwa yeye hakupaswa kupewa ushauri na TRA, bali kupewa na katibu wake ingawa alikiri kuwahi kuona barua kutoka TRA baadaye, japokuwa ilikuwa imechelewa kwa muda wa siku kumi wakati yeye akiwa ameshaondoa kodi kwa kampuni hiyo.
“TRA hata wangeshauri kwa mujibu wa maagizo niliyoyapata, ingekuwa kazi bure, kwanza walishachelewa. Na hata hivyo tangu kupata Uhuru, sheria inatoa mamlaka kwa waziri wa fedha kusamehe kodi ilimradi msahama huo uwe na manufaa kwa wananchi wake bila kushauriana na mtu yeyote,” alidai Mramba.
Alipoulizwa kuwa inadaiwa alikurupuka baada ya kulala nyumbani kwake na asubuhi akaandika dokezo kwa serikali la kuondoa kodi hiyo, Mramba alisema hakufanya hivyo bali Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliagiza kufanya hivyo na kwamba yeye alitekeleza maagizo hayo.
Mramba, Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Fedha na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Grey Mgonja, walifikishwa mahakamani mwaka 2008 wakidaiwa kuwa kati ya Agosti 2002 na Juni 14, 2004, Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa watumishi wa umma, walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao waliipatia msamaha wa kodi isivyo halali, Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza. Kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 12 mwaka huu, ambapo Mramba ataendelea kutoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Tanzania Daima
 
Dah! Huyu huyu Mramba kwenye taarifa nyingine iliyoandaliwa na Tausi Ally, tumeona akisema Betha Soka ndiye aliyewasiliana na TRA kutafuta kifungu kinachotoa msamaha wa kodi.

Naona kwa hapa Mramba ameamua kujitwika msalaba kwa kusema sheria inamruhusu kusamehe kodi kwa manufaa ya umma.

Huku kugongana kwa kauli zake ndiko kunanipa wasiwasi kama hakunufaika na hujuma hiyo
 
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Mramba, amesema kutokana na mkataba uliosainiwa na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali na Kampuni ya Alex Stewart, hakuwa na njia yeyote ya kukwepa kuondoa kodi kwa kampuni hiyo.
Mramba pia aliieleza mahakama kuwa, alipokea barua iliyotoka kwa Katibu wa Rais Benjamin Mkapa kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na nakala iliyokwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo, Andrew Chenge, ikiwataka kutafuta fedha za haraka kwa ajili ya kuilipa kampuni hiyo.
Hayo aliyaeleza jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, John Utumwa, wakati akitoa utetezi katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7, inayomkabili yeye na wenzake wawili.
Mramba alieleza kuwa, mkataba uliotiwa saini kati ya BoT na kampuni hiyo ulikuwa unambana kwa mujibu wa sheria ya mkataba huo kwani asingetoa msahama wa kodi, serikali ilitakiwa kumlipa fedha nyingi mwekezaji huyo.
Akiongozwa na wakili wake, Hulbert Nyange, aliyetaka kujua kama maagizo hayo yote aliyachukuliaje kama Waziri wa Fedha, Mramba alidai kuwa yalitolewa na Rais Mkapa katika dokezo mbalimbali akitaka utekelezaji wa kuilipa kampuni hiyo ufanyike haraka iwezekanavyo.
“Mimi sikuruhusu malipo yoyote wala punguzo lolote ila kwa mujibu wa kifungu cha 4 (3), kinasema malipo yoyote hayatatozwa kodi kwa mujibu wa mkataba huo kati ya BoT na Kampuni ya Stewart,” alidai Mramba.
Wakili Nyange alitaka kujua kama ni kweli Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walitoa ushauri kwa Wizara ya Fedha kuwa wasitoe msahama huo, ambapo alidai kwamba hakuuona ushauri huo.
Aliongeza kuwa yeye hakupaswa kupewa ushauri na TRA, bali kupewa na katibu wake ingawa alikiri kuwahi kuona barua kutoka TRA baadaye, japokuwa ilikuwa imechelewa kwa muda wa siku kumi wakati yeye akiwa ameshaondoa kodi kwa kampuni hiyo.
“TRA hata wangeshauri kwa mujibu wa maagizo niliyoyapata, ingekuwa kazi bure, kwanza walishachelewa. Na hata hivyo tangu kupata Uhuru, sheria inatoa mamlaka kwa waziri wa fedha kusamehe kodi ilimradi msahama huo uwe na manufaa kwa wananchi wake bila kushauriana na mtu yeyote,” alidai Mramba.
Alipoulizwa kuwa inadaiwa alikurupuka baada ya kulala nyumbani kwake na asubuhi akaandika dokezo kwa serikali la kuondoa kodi hiyo, Mramba alisema hakufanya hivyo bali Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliagiza kufanya hivyo na kwamba yeye alitekeleza maagizo hayo.
Mramba, Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Fedha na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Grey Mgonja, walifikishwa mahakamani mwaka 2008 wakidaiwa kuwa kati ya Agosti 2002 na Juni 14, 2004, Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa watumishi wa umma, walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao waliipatia msamaha wa kodi isivyo halali, Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza. Kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 12 mwaka huu, ambapo Mramba ataendelea kutoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Tanzania Daima

Janja yake, simple. Tulishatangaziwa kuwa "tumwache apumzike" anaweza sije kutoa ushahidi na mahakama zetu zisimfanye chochote. Pili Balali eti alikufa! Amepanga utetezi mzuri sana.
 
Back
Top Bottom