Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,229
- Thread starter
-
- #21
Tatizo sio mtu kama Mramba au Dudumizi ,tatizo ni chama hivyo kilichombadilisha mtu ni Chama ,watu walimpigia kura kutokana na wanavyomjua na kuweka imani kwake kuwa mbunge wao ,bila ya shaka siku za mwanzo alionyesha kushirikiana na kusikiliza madai ya wananchi ,ila baada ya uzoefu kwenye Chama chake ndipo alipobadilika na kufuata aliyoyakuta na kuzoeleka kwenye Chama chake cha CCM hivyo unapokuja Uchaguzi hasa huu unaosababishwa na matatizo ya kiutendaji cha kubadilishwa ni kiti cha bunge kuondoshwa katika chama alichokuwepo mhusika na kupelekwa kwenye Chama kingine,hili ni lazima wananchi wajulishwe kuwa wasitake kubadilisha mtu bali wabadiliche chama.
Ila kwa kuwa tayari jina lake lina mawaa sasa (amechafuka kiasi cha kutosha), anaweza kuamua mwenyewe kuachia ngazi. Lakini alivyo king'ang'anizi kama viongozi wengine wa CCM hawezi kuchukua hiyo option!
Atastep down kivipi wakati sasaivi the Court is officially trying to determine whether or not he is guilty!! Ingekuwa Uwaziri or any other office, sawa.. lakini sio ubunge.. acheni jazba
Wakuu,
Nadhani Tanzania tufike mahali sasa tuubadilishe huu utamaduni haramu wa kwamba kiongozi wa umma akishtakiwa kwa kosa ni lazima tusubirie hukumu ya mahakama ndiyo tukose nae imani, huu ni utaratibu mbovu ambao utaendelea kutubomoa.
Nadhani inabidi tufikie mahali tuifanye nchi yetu au viongozi wetu wawe na nidhamu kama wa nchi ya Japan.
Wakuu mnakumbuka mwaka jana yule waziri wa kilimo wa Japan aliyetuhumiwa tu kwa ufisadi akajinyonga? Leo hii nidhamu ya viongozi wetu ingekua ya kiwango hiki sidhani kama hadi leo akina mramba,Rostam,lowasa,karamagi,mgonja nk wangekua hai.Tungekua tunaomboleza tu,au ungeitishwa msiba wa kitaifa
Wananchi wa Rombo au wadau wa hilo jimbo kwa Ujumla wana haki ya kuanzisha mjadala,maandamano,hoja,petition na kuchukua kila aina ya hatua ya kumtaka Mtuh. Basil Pesambili Mramba ajiuzulu.Hii ni hatua muhimu kwa wananchi wa Rombo ktk kuonyesha chuki dhidi ya ufisadi na kupinga matakwa binafsi ya Mbunge wao aliyejineemesha na kulirudisha taifa letu hatua kadhaa nyuma huku wananchi wake wakikosa huduma bora za afya,elimu,njaa,miundombinu duni,kukosa usalama mpakani hasa eneo la Tarakea,huduma duni za maji hususani kwa wananchi wa ukanda wa chini maeneo ya kiraeni,olele.mengwe chini nk. Huyu ndiye mbunge aliyesamehe kodi makampuni ya kizungu pasipokuangalia kwa mapana mateso ya wananchi wake.
Suala la kwamba mapaka ahukumiweni sawa na ni haki yake kama Raia wa kawaida,lakini case yake ni different as public figure.Tena ni mtu ambaye ameshtakiwa na jamhuri ambapo wananchi wa rombo ni sehemu ya hiyo Jamhuri
Basil Pesambili Mramba,Step Down Noow!
However the court asked the accused to deposit 3.9bn/- in cash with two sureties, and surrender their passports and not leave Dar es Salaam without permission.
Siku wakipata ruhusa kuenda au kuhudhuria kikao Cha bunge hawarudi tena.
halafu hilo dau lililowekwa hapo si la kawaida ,nafikiri kuna watu wana usongo nao,sasa hao wengine ambao ni wakali wa ufisadi sijui itakuwaje.
Napenda kuuliza kwa wanaofuatilia kwa ukaribu mashitaka ya watu hawa ,hivimashitaka yao na akina Jeetu Patel ni tofauti ,maana wengine tumo kwenye mkumbo ,labda itasaidia mkituwekea hapa japo kwa muhtasari ili tuweze kupima hili dau na uendeshaji mzima wa mchezo huu.
However the court asked the accused to deposit 3.9bn/- in cash with two sureties, and surrender their passports and not leave Dar es Salaam without permission.
Siku wakipata ruhusa kuenda au kuhudhuria kikao Cha bunge hawarudi tena.
halafu hilo dau lililowekwa hapo si la kawaida ,nafikiri kuna watu wana usongo nao,sasa hao wengine ambao ni wakali wa ufisadi sijui itakuwaje.
Napenda kuuliza kwa wanaofuatilia kwa ukaribu mashitaka ya watu hawa ,hivimashitaka yao na akina Jeetu Patel ni tofauti ,maana wengine tumo kwenye mkumbo ,labda itasaidia mkituwekea hapa japo kwa muhtasari ili tuweze kupima hili dau na uendeshaji mzima wa mchezo huu.
Field Marshall Es,
Mkuu naomba kidogo unipe darasa ktk sheria za Ubunge maanake nimeshindwa kuelewa CCM wanavyocheza mchezo...
Chukulia viongozi wote waliachishwa madaraka kwa sababu za Ufisadi.. toka kina Karamagi, Meghji, Msabah na wenigne wengi tu ambao wote walikuwa watuhumiwa ktk hujuma tofauti... Imekuwaje hawa watu wasiachishwe viti vyao vya ubunge ili uchaguzi mwingine ufanyike badala yake CCM wamewashikilia wakijua kabisa kwamba kama wakifukuzwa viti vya Ubunge kuna hatari ya chama kuvipoteza viti hivyo katika majimbo hayo..
Sasa ningependa kufahamu sheria ya Bunge ni wakati gani mbunge atavuliwa Ubunge ikiwa ametumia vibaya madaraka yake ktk serikali kuu, kwa sababu kuna connection kubwa sana kati ya Ubunge na Uwaziri.
Ingekuwa kama nchi nyinginezo ambazo Mbunge sio lazima awe na madaraka ktk serikali kuu ningeelewa lakini mfumo wa nchi yetu unamhusisha Mbunge toka chama tawala kuwa na madaraka ktk serikali kuu..
Hiyo mkuu wangu naifahamu pamoja na kwamba bado tuna tatizo la kikatiba kuhusiana na wagombea binafsi.. Tatizo langu ni pale Mbunge, kiongozi wa serikali anapohujumu maslahi ya Taifa na ikawa sababu ya kuvuliwa madaraka, lakini bado anaendelea kuwa bungeni kama mbunge..Kuna sheria moja inayosema kuwa mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa. Wakivuliwa uanachama automatically watakuwa wametoswa. Hiyo ni njia moja.
Zakumi,
Hiyo mkuu wangu naifahamu pamoja na kwamba bado tuna tatizo la kikatiba la wagombea binafsi.. tatizo langu ni pale Mbunge kiongozi anapohujumu nchi, maslahi ya Taifa akavuliwa madaraka hayo lakini bado anaendelea kuwa bungeni kama mbunge..
Ni wakati gani mbunge aliyehujumu uchumi wetu atawekwa kando ktk kifaa kikubwa cha serikali kama bunge na utunzi wa sheria.. mambo ambayo yanaweza kabisa kumpa nguvu bado kwa sababu bado amebeba lile jina la Mheshimiwa!..