Mramba Aachie kiti Cha Ubunge!

Wakuu,

Nadhani Tanzania tufike mahali sasa tuubadilishe huu utamaduni haramu wa kwamba kiongozi wa umma akishtakiwa kwa kosa ni lazima tusubirie hukumu ya mahakama ndiyo tukose nae imani, huu ni utaratibu mbovu ambao utaendelea kutubomoa.

Nadhani inabidi tufikie mahali tuifanye nchi yetu au viongozi wetu wawe na nidhamu kama wa nchi ya Japan.

Wakuu mnakumbuka mwaka jana yule waziri wa kilimo wa Japan aliyetuhumiwa tu kwa ufisadi akajinyonga? Leo hii nidhamu ya viongozi wetu ingekua ya kiwango hiki sidhani kama hadi leo akina mramba,Rostam,lowasa,karamagi,mgonja nk wangekua hai.Tungekua tunaomboleza tu,au ungeitishwa msiba wa kitaifa

Wananchi wa Rombo au wadau wa hilo jimbo kwa Ujumla wana haki ya kuanzisha mjadala,maandamano,hoja,petition na kuchukua kila aina ya hatua ya kumtaka Mtuh. Basil Pesambili Mramba ajiuzulu.Hii ni hatua muhimu kwa wananchi wa Rombo ktk kuonyesha chuki dhidi ya ufisadi na kupinga matakwa binafsi ya Mbunge wao aliyejineemesha na kulirudisha taifa letu hatua kadhaa nyuma huku wananchi wake wakikosa huduma bora za afya,elimu,njaa,miundombinu duni,kukosa usalama mpakani hasa eneo la Tarakea,huduma duni za maji hususani kwa wananchi wa ukanda wa chini maeneo ya kiraeni,olele.mengwe chini nk. Huyu ndiye mbunge aliyesamehe kodi makampuni ya kizungu pasipokuangalia kwa mapana mateso ya wananchi wake.

Suala la kwamba mapaka ahukumiweni sawa na ni haki yake kama Raia wa kawaida,lakini case yake ni different as public figure.Tena ni mtu ambaye ameshtakiwa na jamhuri ambapo wananchi wa rombo ni sehemu ya hiyo Jamhuri

Basil Pesambili Mramba,Step Down Noow!
 
Tatizo sio mtu kama Mramba au Dudumizi ,tatizo ni chama hivyo kilichombadilisha mtu ni Chama ,watu walimpigia kura kutokana na wanavyomjua na kuweka imani kwake kuwa mbunge wao ,bila ya shaka siku za mwanzo alionyesha kushirikiana na kusikiliza madai ya wananchi ,ila baada ya uzoefu kwenye Chama chake ndipo alipobadilika na kufuata aliyoyakuta na kuzoeleka kwenye Chama chake cha CCM hivyo unapokuja Uchaguzi hasa huu unaosababishwa na matatizo ya kiutendaji cha kubadilishwa ni kiti cha bunge kuondoshwa katika chama alichokuwepo mhusika na kupelekwa kwenye Chama kingine,hili ni lazima wananchi wajulishwe kuwa wasitake kubadilisha mtu bali wabadiliche chama.

Mkuu Mwiba,

Tuko pamoja,lazima wananchi wa Rombo wabadilishe Chama.na ni rahisi sana kwa wapiga kura wa Rombo kubadilika.Cha msingi ni vyama makini vya upinzani kuimarisha sera zao kwa hilo jimbo.

Itakua rahisi kwa chama au mgombea atakua na ilani ya pekee kwa kila kata au Tarafa katika hilo jimbo,na utaratibu wa kampeni ukiratibiwa vizuri hawa majambazi hayawezi kurudi tena Bungeni.

Kuna maeneo ambayo ni kiini cha mabadiliko ya kisiasa katika hilo jimbo hasa Tarakea ambao mara nyingi wanakua neutral ukilinganisha na maeneo kama Mkuu kwa Basil Mramba.Kinachohitajika ni kampeni zuri na chama au mgombea mwenye kutumia lugha rahisi katika kuwashawishi wapiga kura

CHADEMA ilishawahi kuwa na mbunge katika hilo Jimbo 1995-2000 alikua Alfred justine Salakana.

Upinzani wana karata nzuri sana ya kulichukua hilo jimbo,tena inabidi au ikishindikana inabidi wananchi wahamasishwe kuanzia sasa ili ikifika 2010 yeye au chama chake kitakua hoi katika uchaguzi mkuu
 
Ila kwa kuwa tayari jina lake lina mawaa sasa (amechafuka kiasi cha kutosha), anaweza kuamua mwenyewe kuachia ngazi. Lakini alivyo king'ang'anizi kama viongozi wengine wa CCM hawezi kuchukua hiyo option!

Sasa unataka aamue mwenyewe au unataka kumuamulia aamue mwenyewe?

King'ang'anizi hapa nani yeye au wewe unayeng'ang'ania ajiuzulu kwa kuamua mwenyewe, ingawa kiukweli ni wewe ndiye unayeamua hivyo?
 
Atastep down kivipi wakati sasaivi the Court is officially trying to determine whether or not he is guilty!! Ingekuwa Uwaziri or any other office, sawa.. lakini sio ubunge.. acheni jazba
 
Kama Tetes za Manji kunywa sumu ni kweli,basi nidhamu ya Japan niliyoiongelea imeanza kurejea
 
Atastep down kivipi wakati sasaivi the Court is officially trying to determine whether or not he is guilty!! Ingekuwa Uwaziri or any other office, sawa.. lakini sio ubunge.. acheni jazba

Mkuu,

Ubunge ni ofisi ya umma na ina heshima yake.Anayekaa katika hiyo ofisi amepewa dhamana.

Pia,hadi yeye kupewa uwaziri alioubaka ni kwamba mojawapo ya qualification ilikua ni lazima awe mbunge.Na ubunge huo hakuupata kwa kuteuliwa,alipigiwa kura,wananchi wanmshinikize ajiuzulu.

Waajiri wake ni wananchi,hakuna haja ya kusubiri awe guilty bali ameidhalilisha ofisi ya umma ikiwepo ubunge ambao ulikua msingi,na heshima ya kumpatia huo uwaziri.

Wabunge wanalipwa kutokana na kodi za watanzania wakiwepo wapiga kura wake,leo hii kwa sababu ya uzembe wake na upuuzi amejikuta akijitetea mahakamni badla ya kuwa bungeni au katika ofisi za ununge,au jimboni kwake akiwatetea na kuwawakilisha wapiga kura wake.

Wananchi wa Rombo wanyo haki ya kisiasa na hamasa ya kijamii ya kumkataa,ya kumtaka ajiuzulu
 
Kikatiba atakapokutwa na hatia, hatakuwa na ujanja! Lakini sasa bado ni mbunge
 
Clearly Ben is unfamiliar na warombo.. They have a very very cohesive mentality. Bora mamfiche mwizi wao kuliko kuside na mtu ambae sio mrombo.. Ndio maana wezi wa magari wanaokimbiliaga kule (ambao ni warombo) nivigumu sana kuwakamata.. wananchi dont snitch.. So i dont think warombo watademand anything at all... Tusubiri tuone.. To them they are Warombo first, catholic 2nd and Tanzanian last..

Kwasasa kustep down ni busara binafsi..kama hataki, hakuna cha kudemand.. acheni sheria ichukue mkondo wake alafu baadae ndio atalazimika sasa kututokea.
 
Wakuu,

Nadhani Tanzania tufike mahali sasa tuubadilishe huu utamaduni haramu wa kwamba kiongozi wa umma akishtakiwa kwa kosa ni lazima tusubirie hukumu ya mahakama ndiyo tukose nae imani, huu ni utaratibu mbovu ambao utaendelea kutubomoa.

Nadhani inabidi tufikie mahali tuifanye nchi yetu au viongozi wetu wawe na nidhamu kama wa nchi ya Japan.

Wakuu mnakumbuka mwaka jana yule waziri wa kilimo wa Japan aliyetuhumiwa tu kwa ufisadi akajinyonga? Leo hii nidhamu ya viongozi wetu ingekua ya kiwango hiki sidhani kama hadi leo akina mramba,Rostam,lowasa,karamagi,mgonja nk wangekua hai.Tungekua tunaomboleza tu,au ungeitishwa msiba wa kitaifa

Wananchi wa Rombo au wadau wa hilo jimbo kwa Ujumla wana haki ya kuanzisha mjadala,maandamano,hoja,petition na kuchukua kila aina ya hatua ya kumtaka Mtuh. Basil Pesambili Mramba ajiuzulu.Hii ni hatua muhimu kwa wananchi wa Rombo ktk kuonyesha chuki dhidi ya ufisadi na kupinga matakwa binafsi ya Mbunge wao aliyejineemesha na kulirudisha taifa letu hatua kadhaa nyuma huku wananchi wake wakikosa huduma bora za afya,elimu,njaa,miundombinu duni,kukosa usalama mpakani hasa eneo la Tarakea,huduma duni za maji hususani kwa wananchi wa ukanda wa chini maeneo ya kiraeni,olele.mengwe chini nk. Huyu ndiye mbunge aliyesamehe kodi makampuni ya kizungu pasipokuangalia kwa mapana mateso ya wananchi wake.

Suala la kwamba mapaka ahukumiweni sawa na ni haki yake kama Raia wa kawaida,lakini case yake ni different as public figure.Tena ni mtu ambaye ameshtakiwa na jamhuri ambapo wananchi wa rombo ni sehemu ya hiyo Jamhuri

Basil Pesambili Mramba,Step Down Noow!

You mean you want to suspend the rule of law? Then how will we decide when will a person step down? By mob justice perhaps? What's next, stoning?

Mimi ningependa kuona Mramba na wenzake waupate nmkono wa sheria.Ningependa sheria yetu iwe ya kutegemeka.Lakini nisingependa kuona watu wanatetea summary execution.Kwa sababu hata kama ni kweli Mramba ana hatia, kumfanyia some summary execution kuta bastardize any sense of justice, na hata watetezi wake wataweza kusema kaonewa (remember argument ya "Natural Justice" ya Lowassa ilivyotia doa tume ya Mwakyembe?)

The rule of law has it's price, and one of the price is due diligency and thoroughness. Kama tunaendesha mambo kwa jazba tu hata wewe mwenyewe unayeshabikia watu kuhukumiwa na vyombo vilivyo nje ya mahakama watu wanaweza kukuanzishia kampeni, wakakuandika vibaya kwenye magazeti, waka-photoshop picha zako, wakafoji ushahidi, ukahukumiwa kwenye vyombo vya habari na kupigwa mawe na wananchi.

Unependa hilo?
 
However the court asked the accused to deposit 3.9bn/- in cash with two sureties, and surrender their passports and not leave Dar es Salaam without permission.

Siku wakipata ruhusa kuenda au kuhudhuria kikao Cha bunge hawarudi tena.
halafu hilo dau lililowekwa hapo si la kawaida ,nafikiri kuna watu wana usongo nao,sasa hao wengine ambao ni wakali wa ufisadi sijui itakuwaje.

Napenda kuuliza kwa wanaofuatilia kwa ukaribu mashitaka ya watu hawa ,hivimashitaka yao na akina Jeetu Patel ni tofauti ,maana wengine tumo kwenye mkumbo ,labda itasaidia mkituwekea hapa japo kwa muhtasari ili tuweze kupima hili dau na uendeshaji mzima wa mchezo huu.
 
Ujue hilo dau ni bonge la kitendawili.

Ukiweza kuweka bail unathibitisha wewe ni fisadi.

Ukishindwa unaenda rumande.
 
However the court asked the accused to deposit 3.9bn/- in cash with two sureties, and surrender their passports and not leave Dar es Salaam without permission.

Siku wakipata ruhusa kuenda au kuhudhuria kikao Cha bunge hawarudi tena.
halafu hilo dau lililowekwa hapo si la kawaida ,nafikiri kuna watu wana usongo nao,sasa hao wengine ambao ni wakali wa ufisadi sijui itakuwaje.

Napenda kuuliza kwa wanaofuatilia kwa ukaribu mashitaka ya watu hawa ,hivimashitaka yao na akina Jeetu Patel ni tofauti ,maana wengine tumo kwenye mkumbo ,labda itasaidia mkituwekea hapa japo kwa muhtasari ili tuweze kupima hili dau na uendeshaji mzima wa mchezo huu.

kifupi ni tofauti,,,,,wao kina mramba wanashtakiwa kwa kutumia vinaya madaraka...kina jitu ni mambo ya EPA
 
These people are smart..kama ni cash wana millions of dollars wote..Kisu mbaya.. lakini hapa watachangisha mtaniambia.. Hawataki kuozea rumande lakini vile vile watataka kuonyesha kuwa wao hawana hela zakifisadi..
 
CCM ndio wanatakiwa kumuondoa kwenye nafasi hiyo next CC, ninaamini kuwa watamtema kwa sababu kumbuka kua huyu ni mtu wa mkapa, ambaye mtandao never liked him lakini walilazimishwa na kisumo kumrudisha cabinet, ingawa ilikuwa clear toka mwanzoni kwamba hawamtaki na kwamba the first chance wanamtupa nje, they did.

sasa watch ninaamini kwa 100%, wanakuja kumtosa na ubunge pia kwenye next cc na nec, na sio siri kwamba watamfunga maana ana masoo mengi sana, na ninaamini kwamba anyetafutwa hapa ni b tu hawa ni ngazi tu!
 
Field Marshall Es,
Mkuu naomba kidogo unipe darasa ktk sheria za Ubunge maanake nimeshindwa kuelewa CCM wanavyocheza mchezo...
Chukulia viongozi wote waliachishwa madaraka kwa sababu za Ufisadi.. toka kina Karamagi, Meghji, Msabah na wenigne wengi tu ambao wote walikuwa watuhumiwa ktk hujuma tofauti... Imekuwaje hawa watu wasiachishwe viti vyao vya ubunge ili uchaguzi mwingine ufanyike badala yake CCM wamewashikilia wakijua kabisa kwamba kama wakifukuzwa viti vya Ubunge kuna hatari ya chama kuvipoteza viti hivyo katika majimbo hayo..

Sasa ningependa kufahamu sheria ya Bunge ni wakati gani mbunge atavuliwa Ubunge ikiwa ametumia vibaya madaraka yake ktk serikali kuu, kwa sababu kuna connection kubwa sana kati ya Ubunge na Uwaziri.
Ingekuwa kama nchi nyinginezo ambazo Mbunge sio lazima awe na madaraka ktk serikali kuu ningeelewa lakini mfumo wa nchi yetu unamhusisha Mbunge toka chama tawala kuwa na madaraka ktk serikali kuu..
 
Mkuu hivi sijasema hapa kwamba hati ya kuwafukuza hao wakulu ccm tayari iko mezani kwa muungwana, wanamsubiri tu asue sue kwanza lakini liko mezani kwake mkuu, subiri tu iko siku utalisikia hilo nalo linakuja,

mkuu maneno yote huanzia kule cc, ambako inatakiwa mjumbe mmoja tu alidhamiria kukusimamia kidete utemwe, sasa hapo itokee bahati na wewe uwe na mjumbe mkali pia otherwise unatemwa, kama walivyomtema mbunge nyimbo kwa kusaidia upinzani kwenye uchaguzi wa Tunduru.

kwenye serikali sina uhakika, ila ninajua kwenye ccm ni wajumbe wa cc tu kukulia deep unatoswa!
 
Field Marshall Es,
Mkuu naomba kidogo unipe darasa ktk sheria za Ubunge maanake nimeshindwa kuelewa CCM wanavyocheza mchezo...
Chukulia viongozi wote waliachishwa madaraka kwa sababu za Ufisadi.. toka kina Karamagi, Meghji, Msabah na wenigne wengi tu ambao wote walikuwa watuhumiwa ktk hujuma tofauti... Imekuwaje hawa watu wasiachishwe viti vyao vya ubunge ili uchaguzi mwingine ufanyike badala yake CCM wamewashikilia wakijua kabisa kwamba kama wakifukuzwa viti vya Ubunge kuna hatari ya chama kuvipoteza viti hivyo katika majimbo hayo..

Sasa ningependa kufahamu sheria ya Bunge ni wakati gani mbunge atavuliwa Ubunge ikiwa ametumia vibaya madaraka yake ktk serikali kuu, kwa sababu kuna connection kubwa sana kati ya Ubunge na Uwaziri.
Ingekuwa kama nchi nyinginezo ambazo Mbunge sio lazima awe na madaraka ktk serikali kuu ningeelewa lakini mfumo wa nchi yetu unamhusisha Mbunge toka chama tawala kuwa na madaraka ktk serikali kuu..

Kuna sheria moja inayosema kuwa mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa. Wakivuliwa uanachama automatically watakuwa wametoswa. Hiyo ni njia moja.
 
Zakumi,
Kuna sheria moja inayosema kuwa mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa. Wakivuliwa uanachama automatically watakuwa wametoswa. Hiyo ni njia moja.
Hiyo mkuu wangu naifahamu pamoja na kwamba bado tuna tatizo la kikatiba kuhusiana na wagombea binafsi.. Tatizo langu ni pale Mbunge, kiongozi wa serikali anapohujumu maslahi ya Taifa na ikawa sababu ya kuvuliwa madaraka, lakini bado anaendelea kuwa bungeni kama mbunge..
Ni wakati gani mbunge aliyehujumu uchumi wa nchi atawekwa kando ktk kifaa kikubwa cha serikali kama bunge na utunzi wa sheria.. mambo ambayo yanaweza kabisa kumpa nguvu kwa sababu bado amebeba lile jina la Mheshimiwa!..
 
Spika Sitta azungumzia ubunge wa Mramba

2008-11-26 10:10:25
Na Theodatus Muchunguzi, Arusha

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta, amesema kuwa licha ya Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba, kukamatwa na kufunguliwa mashitaka, ataendelea kuwa mbunge hadi Mahakama itakapotoa uamuzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Akizungumza na Nipashe mjini Arusha jana, Sitta alisema kuwa alipata taarifa za kukamatwa kwa Mramba, lakini akasema kuwa ataendelea kuwa mbunge hadi hapo itakapothibitika.

``Atajitetea na sisi tutasikia mahakama itakavyosema. Bunge haliwezi kumhukumu mbunge kabla tuhuma dhidi yake hazijathibitika,`` alisema Sitta, ambaye anahudhuria mkutano wa wabunge wa mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).

Alisema chini ya katiba ya Tanzania , mbunge akifungwa kifungo cha kuanzia miezi sita moja kwa moja anapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge.

Kwa mujibu wa Sitta, ikiwa Mramba atapata dhamana ataendelea kuhudhuria vikao vya Bunge wakati kesi dhidi yake ikiendelea.

Wakati huo huo, Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa yeye na wenzake wataendelea kufuatilia kama serikali itawakamata na kuwafikisha mahakamani watu wote ambao wako katika orodha ya tuhuma za ufisadi.

Akizungumza mjini hapa jana baada ya kusikia taarifa za kukamatwa kwa Mramba Waziri wa zamani wa wizara za Fedha na Nishati na Madini, Daniel Yona, Dk. Slaa alisema: ``Nitaridhika ikiwa wale wote tulio na taarifa zao wanashitakiwa na sitaridhika ikiwa orodha yote ya majina niliyonayo hawatashitakiwa.``

SOURCE: Nipashe
Swali kwa mh. je atawahudumia wananchi wake na je atasafirije nje ya Dar kwenda Bungeni Dodoma?
 
Zakumi,

Hiyo mkuu wangu naifahamu pamoja na kwamba bado tuna tatizo la kikatiba la wagombea binafsi.. tatizo langu ni pale Mbunge kiongozi anapohujumu nchi, maslahi ya Taifa akavuliwa madaraka hayo lakini bado anaendelea kuwa bungeni kama mbunge..
Ni wakati gani mbunge aliyehujumu uchumi wetu atawekwa kando ktk kifaa kikubwa cha serikali kama bunge na utunzi wa sheria.. mambo ambayo yanaweza kabisa kumpa nguvu bado kwa sababu bado amebeba lile jina la Mheshimiwa!..

Mkandara:

Kufa kujuana (period). Mramba alikuwa nje ya system tayari, lakini alirudi tena kwa sababu ya kujuana.

Ubunge wake ulishawahi kutenguliwa na mahakama kuu kwa makosa ya taratibu za uchaguzi.

Nadhani umefika wakati sio kurudisha miiko ya Azimio la Arusha bali kuhakikisha kuwa kosa moja linatoa mtu nje system katika maisha yake yote.

Mwizi ni mwizi tu.
 
Back
Top Bottom