Mramba Aachie kiti Cha Ubunge! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mramba Aachie kiti Cha Ubunge!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ben Saanane, Nov 26, 2008.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Nov 26, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa nianze kwa kupongeza hatua moja ya kumfikisha Mhe.Mramba na Mhe.Daniel Yona mahakamani ili kujibu mashitaka yao ya matumizi mabaya ya madaraka yaliyolisababishia taifa letu hasara kubwa

  Mramba ni mbunge wa kuchaguliwa na wapiga kura wa Jimbo la Rombo.kiti cha ubunge wa jimbo la Rombo ni ofisi ya umma.Hadi sasa mhe.Mramba ameonyesha utovu mkubwa wa nidhamu katika ofisi ya umma,hafai kuwa na mamlaka katika ofisi ya umma.Leo hii wananchi wa jimbo la Rombo watanufaika vipi na mbunge wao kama haruhusiwi hata kutoka nje ya Dar es salaaam?

  Anahimiza vipi shughuli za maendeleo?

  Pia,katika sifa zilizomfanya Mramba kuwa waziri au kupewa dhamana kubwa kama hiyo katika ofisi nyeti na inayogusa maisha ya kila siku ya mtanzania ni pamoja na kupigiwa kura na wananchi wa jimbo la Rombo.Hii ilikua ni heshima kubwa si kwake pekee bali hata kwa wananchi na wapiga kura wake wa jimbo la Rombo.Leo hii mramba kutumia mamlaka na dhamana aliyopewa vibaya imegeuka kuwa dharau,aibu na kejeli kwa wapiga kura wake.


  Mramba amewadhalilisha wapiga kura wake,ni jukumu la kila mwananchi na mpiga kura wa jimbo la Rombo kumkataa Mramba na mambo yake yote.Kumkubali Mramba maanke ni kumkubali na aibu zake zote.Mambo aliyoyatenda akiwa waziri wa fedha,ni matusi makubwa kwa wapiga kura wake ambao wapo walio wengi wamezongwa na umaskini,waliokosa elimu nk. Leo hii hospitali kuu ya jimbo lake Huruma hospital ina upungufu mkubwa wa madawa,vitanda nk.Sasa leo mbunge anapandishwa kizimbani kwa kutumia mamlaka vibaya ili kujinufaisha yeye na wazungu huku wananchi wake wakiwa katika hali ya umaskini wa kutisha na mateso makali

  Ni jukumu la watu woote wenye maslahi katika jimbo la Rombo kokote waliko huko Tanzania na duniani kuungana bega kwa bega kwa kumshinikiza mtuhumiwa Basil Pesambili Mramba aachie ngazi ili kuunga mkono juhudi za kupambana na ufisadi. warombo kuweni sehemu ya vita dhidi ya ufisadi kwa kumkataa Basil Mramba kuwa mbunge wenu

  Onyesheni dira ya Tanzania tuitakayo


  Basil Pesambili Mramba Step Down Nooow!
   
 2. m

  mnyama Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani Daniel Yona siyo Mbunge? Mbona umemuongelea tu Mramba? Sheria ikoje kuhusu mbunge akituhumiwa? anasimamishwa ubunge au anaachia ubunge? Ni fikiri tuangalie sheria kuliko matakwa binafsi
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sasa tunasubiri tui kiti kipiganiwe rasmi. Kwani kimsingi kiko wazi tayari. Dhamana ya wananchi inapotea upon conviction of course. JF lawyers hebu tuelekezeni ni cha kufanya nataka niende kupigania jimbo hilo. Nipe na requirements na formalities za kugombea. HAIHITAJIKI FEDHA BALI FOCUS, muda wa kampeni za hela umepita baada ya operations sangara. Haraka kidogo tafadhali.
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  It is until he si proved to be guilty. Hizo ni tuhuma tu, zikithibitika wala kutakuwa hakuna haja ya kampeni yoyote, Spika atatangaza tu kuwa kiti chake kiko wazi.
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  DY siyo mbunge. Jimbo lake la Same Mashariki lilikwapuliwa na Anna Kilango Malecela.
   
 6. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  1. Mramba ana kesi mahakamani, hajawa proven gilty in a court of law.

  2. Pande mbili zenye haki ya kumtaka Mramba ajiuzulu ni watu wa Rombo waliomchagua na watu wa CCM waliompa tiketi ya uwakilishi.

  Let's be fair.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ila kwa kuwa tayari jina lake lina mawaa sasa (amechafuka kiasi cha kutosha), anaweza kuamua mwenyewe kuachia ngazi. Lakini alivyo king'ang'anizi kama viongozi wengine wa CCM hawezi kuchukua hiyo option!
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pundit Mramba anaweza kulazimishwa na Sisiem ama wapiga kura wake aachie ofisi (of course, hata kama hajapatikana na hatia) ila akipatikana hatia sio jambo la wapiga kura ama Sisiem tena, ila naturally anakosa sifa za kuwa mbunge.
  But Mramba won't give up without a fight!
  I think he is going to fight for his 'innocence'....pia atapigania imani ya wapiga kura wake.
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe mkuu...


  Lakini kimaadili amepotoka,, kitendo cha kufikishwa mahakamani kwa kutuhumiwa tu kinatosha kumfanya yeye mwenyewe 'ajipime' kisha achukue uamuzi stahili.

  Enzi ya Mwalimu si ilikuwa ukituhumiwa tu umekwenda na maji? Unakumbuka hadithi ya mke wa Kaizari alivotuhumiwa uzinzi? Si aliachwa kwani ilisubiriwa awe proved?
   
 10. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sasa mpaka ashikwe usiku ready handed na wananchi wenye hasira kali ndo akubali?
   
 11. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Watuhumiwa wa Richmond lini?
   
 12. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyu Mramba ana uzoefu wa kuendesha kesi za kung'ang'ania kiti cha ubunge kwa miaka. Kumbukeni kesi ya Mramba na Ngalai miaka ya 80/90. Kagumu kweli haka kazee kwenye siasa za ulaji, ila kwa picha za jana kamezeeka sasa
   
 13. Kaka Mkubwa

  Kaka Mkubwa Senior Member

  #13
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  asipohudhuria vikao vitatu vya bunge bila ya spika kuwa na taqarifa nje.
   
 14. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Spika anasubiri taarifa gani wakati mtu hawezi kufika hata kibaha
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duu watu mna usongo balaa!!

  Ila bwana haya majambazi yanaudhi sana bora yanyanganywe vyeo na yakirudi mitaani 'kiaina' kwa kutu yeyusha na kupindisha sheria tuyapigie kelele za mwizi na kuyawasha kiberiti kama vibaka wengine wa simu na miwa!
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ataomba ruhusa ya mahakama kuhudhuria vikao vya bunge na most probably atapewa ruhusa.Kushtakiwa si kuonekana na hatia.Bado ni mbunge na wananchi waliomchagua wanayo haki kuwakilishwa na mbunge wao.
   
 17. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #17
  Nov 26, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pundit,

  Ndiyo maana nimesizitizia watu wa Rombo na wenye maslahi katika jimbo hilo hata kama hukumpigia kura
   
 18. RR

  RR JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Mkuu unadhani hawa watu wakinyangwanywa vyeo inatosha? .........the chaps are rich.
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio mtu kama Mramba au Dudumizi ,tatizo ni chama hivyo kilichombadilisha mtu ni Chama ,watu walimpigia kura kutokana na wanavyomjua na kuweka imani kwake kuwa mbunge wao ,bila ya shaka siku za mwanzo alionyesha kushirikiana na kusikiliza madai ya wananchi ,ila baada ya uzoefu kwenye Chama chake ndipo alipobadilika na kufuata aliyoyakuta na kuzoeleka kwenye Chama chake cha CCM hivyo unapokuja Uchaguzi hasa huu unaosababishwa na matatizo ya kiutendaji cha kubadilishwa ni kiti cha bunge kuondoshwa katika chama alichokuwepo mhusika na kupelekwa kwenye Chama kingine,hili ni lazima wananchi wajulishwe kuwa wasitake kubadilisha mtu bali wabadiliche chama.

  Ikiwa itatumika system hii basi hawa watu wataanza kuwahiwa ndani ya Chama chao na yale mambu ya kusema huyu ni mwenzetu yataondoka ,tunaona leo hii watu wabebakwa na nyara za serikali(Fedha zilizochotwa) na wengine wamejiuzulu lakini Chama chao bado kinawakumbatia ,ila mambo yanapokuja juu utawasikia wasemaji wa Chama wakimtenga mtu huku wakisema Chama hakihusiki ni yake menyewe ,hapa huwa wanawawekea mtego wapiga kura ili waendelee kuwachagua na kuihifadhi nafasi ya chama chao Bungeni.

  Hivyo kama wananchi wataamshwa na kutakiwa kubadilisha Chama na sio mtu basi mafisadi wataanza kutimuliwa mapema ndani ya vyama vyao ili kulinda heshima ya Chama.Heshima ya Chama Cha CCM imepotea na hadhi yake kushuka vibaya sana ,ila bado wananchi huwa wanategwa na kauli za hili si la Chama ila ni lake mwenyewe ,huku utawasikia wakisema CCM ndio Baba.
   
 20. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Ndugu Mnyama, inaonesha wewe ni mgeni na wanasiasa wa Tanzania! Daniel Yona siyo mbunge kwa sasa. Aliwahi kuwa Mbunge wa same Mashariki kipindi cha Nkapa. Kwa sasa mbunge wa jimbo hilo ni Mama Anne Kilango Malecela
   
Loading...