Mradi wa Treni za Juu Dar Es Salaam

Mradi wa Treni za Juu Dar Es Salaam

Kwedu Kwazu

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
504
Reaction score
71

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’

Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Screen-Shot-2014-05-15-at-4.53.27-PM.png

Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.
 
Yani wewe hata waziri wa uchukizi hamfahamu!!!!!
 
...Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo....'

Mwakyembe huyu huyu wa Richmond?
 
Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika'

Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Screen-Shot-2014-05-15-at-4.53.27-PM.png

Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.
Mwakyembe ni waziri wa Afrika mashariki,sasa hivi yuko bize kushugulikia somalia ijiunge EAC
 
Vipi kule kwanda cha pikipiki za Honda? Ha ha ha ha
 
Tanzania tuna waza mambo yasiyowezekana kama machangudoa..kila siku unacheze mipini unajua kuna siku utahongwa vitz na nyumba
 
Kutoka chumbageni hadi sumbawanga kupitia chumbe....
 
Duu! Yaani huyu sijui ni mtu gn,au ndo umekurupuka sasa hivi kutoka usingizini!?
 
Hv strabag wameshindwa kazi au? Yan huyo wazir ye anawaza matreni ya umeme wakati ya mafuta tu yanatushinda. ----- kweli
 
Watanzania tunapenda picha jamani, tukiwekewa picha tu tushachanganyikiwa.
 
Saafi saana...waongeze miradi tu,vipi upembuzi yakinifu umeshafanyika???kama tayari nani alitoa pesa??wafadhili au pesa za ndani???na ule mradi wa ferry to bgmoyo?? Na ule mradi mkongwe wa since 1961 RUVU JUU na RUVU CHINI??jamani tusomeshe watoto wetu.
 
Back
Top Bottom