Mradi wa Treni za Juu Dar Es Salaam

Mradi wa Treni za Juu Dar Es Salaam

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’

Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Screen-Shot-2014-05-15-at-4.53.27-PM.png

Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.

Hizi za chini zimewashinda za juu wataziweza wapiiii hii nji ni zaidi ya shida.
 
Hadi ikifikia hivyo nitakuwa nina vilembwe tayari na kitukuu changu labda ndio kije kuwa rais hivi tuendelee kuota
 
Hv strabag wameshindwa kazi au? Yan huyo wazir ye anawaza matreni ya umeme wakati ya mafuta tu yanatushinda. ----- kweli
Hizo kweli ni ndoto za alinacha.

Strabag na mradi wao tu wa barabara ya chini, toka Kimara mwisho hadi katikati ya Jiji, huu ni mwaka wa tano, mradi huo haujakamilika, badala yake kila kukicha tunawashuhudia mafundi wa kampuni hiyo wakiendelea 'kuichimbachimba' upya barabara hiyo, ndiyo sasa mnakurupuka toka usingizini, mnatuletea huo mradi wa treni za 'angani'

Kweli nimeamini, fikra na mawazo ya viongozi wa TZ, inafaa hao watu nao watumbukizwe kuwa miongoni ya maajabu makubwa kabisa duniani!
 
Ule mradi wa SHUMAKE TRAIN ambao Mwakyembe alitapeliwa akasaini MKATABA HOTELINI marekani ..umefikia wapi ...?? Vituko havitaisha Nchi Hii ...Huyo Ndio Mwakyembe aliyechunguza wenzake ..heheh ..
 
Wanafunzi wa msingi wanaota, secondari wanaota, vyuoni wanaota, wanasiasa wanaota, wananchi wa kawaida wanaota, na VIONGOZI wa serikalini nao WANAOTA. Duh!
Kama ni habari za kweli, kwa nini miradi kama hii isianzishwe kwenye majiji mengine kama Mwanza au Mbeya??? Dar inaigharimu nchi bure, ilipofika inatosha, maana ni vurugu mechi mpaka sasa!!
Kama ni habari za kweli, hapo wataanza kufukuza watu kwenye makazi yao, na stori zingine kibao!! DART yenyewe kama haisomeki hivi, mara treni ya airport dar, mara treni za juu, kweli siasa ni kudanganya danganya tuu, duh!
USHAURI kwa serikali: Nendeni Angola-Luanda mkawaombe planning ya miji na mikakati ya utekelezaji, walikuwa na magofu miaka 20 ilopita, leo wameweza! Hii ni kutokana na picha nilizoziona humu JF za Luanda-Angola.
 
Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’

Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Screen-Shot-2014-05-15-at-4.53.27-PM.png

Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.

Kama yamesemwa haya, basi wa-Tz tunadungwa kweli dozi za uongo, nafikiri miili yetu ishapooza kwa madozi ya dizaini hii.
 
hivi watanzania sisi tuna matatizo gani?!kwa nini watawala wanatuchezea namna hii...hawaoni hata aibu kusema uongo!!ama kweli mbinguni tutakuwa depopulated
 
Flyovers kwenye makutano muhimu ya barabara tumeshindwa tunawaza treni za juu
 
hahahahahahahahaahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Ni bora viongozi wasioongea bali tunaona vitu wanavyofanya kuliko hawa wapiga porojo
 
Yani wewe hata waziri wa uchukizi hamfahamu!!!!!
Nafikiri mleta mada anakumbushia wakati ule huyu waziri aliposema haya, nami nakumbuka ahadi ilikuwa ni mradi huu kuanza kabla ya December 2014 yaani mwaka jana!

Alisema wenzake waliingia MKATABA na kampuni ya mkononi Richmond Kuleta Umeme ...lakini angalau MITAMBO ilikuja na kuonesha MITAMBO ni mizuri Leo Hii wenzetu wa marekani wameinunua na wanatuuzia Umeme .....
Yeye kaenda kuingia MKATABA wa treni hewa ..mradi wa milioni 300 dola ....,muwekezaji mwenyewe SHUMAKE ...ni ametangazwa Bankrupt ...ukishakuwa declared buncrupt ulaya hata kura hupigi ..huruhusiwi kuingia MKATABA wowote ...Mwakyembe Kama mwanasheria anajua Hilo .....na Zaidi alisainisha MKATABA HOTELINI ....na hata sio Ubalozini .....
Hii Nchi Kama alipopata kusema Cardinal Pengo .; " ukiona watu wanapinga ufisadi ...hawapingi kwa moyo ..,Bali wanapinga kwa kuwa wao wamekosa fursa ya kufanya ufisadi ...ukiwapa fursa nao watafanya Hivyo Hivyo "
Mwakyembe kadhibitisha Hilo
 
Back
Top Bottom