Mradi wa mwendokasi(DART) unaelekea kufa

Mradi wa mwendokasi(DART) unaelekea kufa

shalet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
3,441
Reaction score
3,613
Leo nikiwa naelekea muhimbili mmoja wa wafanyakazi wa udart alikuwa anaelezea machungu yake kutokana na dhuluma wanayofanyiwa. takribani wafanyakazi 52 wamesimamishwa kazi bila kulipwa mishahara ya miezi mitatu wanaambiwa kampuni haina pesa. mikataba yao ilitakiwa kuisha june ila mwezi huu wamepewa barua kuwa wasiende kazini kampuni haina cha kuwalipa.

wafanyakazi wote kasoro mmoja wamegoma kupokea barua ya kusimamishwa kazi mpaka wapewe haki yao huyu mmoja kapokea sababu hakuwa na mkataba. kwa sasa kesi iko kwa mkuu wa wilaya kwa usuluhishi na udart wameahidi kulipa hadi tarehe 16 ila kuna za chini chini hata hiyo tarehe hawawezi lipa sababu hawana pesa.

maswali yangu ni kwanini kampuni inajiendesha kwa hasara na abiria ni wengi kituoni, je 650 haitoshi kama nauli, je wanatumia gharama kubwa kulipia facilities za mradi, je walikopa sana kama uwekezaji hivo wanalipa riba ya mabasi yaliopaki hayatembei, au ni upigaji tu wa watanzania.

karibuni wadau wa mwendokasi.
 
Tangu lini hii serikali ikaweza kusimamia kitu bin uzuri acha tuu yafe ili angalao tupumue na hivyo vimwendo asi vyao nyoo
 
Ni kipindi cha mpito tu, Mambo yatakwenda sawa tu.
leo tu hali tete.. mvua kidogo hakuna magari, watu wa kutoka mjini kwenda kimara jioni hii ni adha tupu, wengine imeoidi wapande pikap na vieikuu kuzungukia morocco na makumbusho, jangwani hakupitiki
 
Udart hawakuwa na mtaji. Mabasi yamefadhiliwa na benki kwa mkopo wa zaidi ya 90%. So pesa zinazopatikana zinaishia NMB.
Kwetu kila kitu kinafail
Screenshot_2018-05-04-08-52-48.jpg
 
Kuna mtu ameandika
Wadada na wakaka wapenda kula chipsi wa dar wataacha mwenyewe maana kwa khali ya mwendokasi ilivyo ni kuparurana
 
Tunalazimisha biashara tuzizoziweza
Wapo wanaojua biashara tangu karne na karne
Biashara ni kuzalisha faida na sio mradi tu eti ni biashara tumeianzisha
Tutafeli sana katika haya
Biashara ya transport zote. Nina maana barabara, angani na majini ni ngumu sana kuiona faida kama akili ya ziada haijatumika
Yetu macho
 
Kuna mtu ameandika
Wadada na wakaka wapenda kula chipsi wa dar wataacha mwenyewe maana kwa khali ya mwendokasi ilivyo ni kuparurana
Hahahaha usinivunje mbavu aisee! Leo asubuhi saa kumi na moja na nusu nimepanda mwendokasi tumebanana mpaka balaa! Kuna mdada alikuwa nyuma yangu na ni mfupi kwangu, yaani rangi yake ya mdomoni yote amenifutia kwenye sare yangu ya kazini! Huu usafiri una changamoto sana
 
Back
Top Bottom