Mradi wa maji uliojengwa na China wafufua mashamba ya Kenya

Mradi wa maji uliojengwa na China wafufua mashamba ya Kenya

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212
1748481415498678.jpeg


Kando ya kingo za Mto Nzoia magharibi mwa Kenya, mabadiliko ya kimya kimya yanaendelea kuonekana na kukita mizizi. Mashamba ambayo hapo awali yalikuwa matupu, yakikauka kwa ukame na kuathiriwa na mafuriko yasiyotabirika, sasa yamenawiri huku yakiwa yamesheheni safu zilizostawi za mazao, kutokana na maji yanayotiririka kutoka kwenye mifereji mipya ya umwagiliaji iliyojengwa.

Kiini cha mabadiliko haya ni Mradi wa Umwagiliaji wa Lower Nzoia, ambao ni mkubwa zaidi na wa aina yake nchini Kenya, uliojengwa na Shirika la Sinohydro la China. Mto Nzoia wenye urefu wa kilomita 250 ni mto mkubwa unaomwaga maji yake kwenye Ziwa Victoria na unasaidia mamilioni ya watu magharibi mwa Kenya.

Kwa mkulima wa eneo hilo Henry Odhiambo, mabadiliko haya yanayoonekana zaidi kwake ni ya binafsi sana. Baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi nchini Sudan Kusini, aliacha kazi yake na kurudi nyumbani kwao katika Kaunti ya Siaya, akivutiwa na mradi huu ulioleta mabadiliko.

"Niliacha kazi yangu Sudan Kusini kasha nikarurudi nyumbani kufanya shughuli za kilimo," Odhiambo anasema, akiwa amesimama katikati ya safu safi za mboga za mnanaa. "Eneo hili, ambalo hapo awali lilikuwa vichaka vitupu na kupuuzwa, sasa limehuishwa. Tuna maji, tuna mazao, na hivi karibuni, tutakuwa na mapato thabiti."

Kwa miongo kadhaa, jamii zilizo kando ya Mto Nzoia zimeishi maisha yasiyo na uhakika. Uwezo wa ardhi iliyodhoofika kutokana na kutegemea kwake kilimo kinachotegemea mvua, huku hali ya hewa isiyotabirika ikiacha familia katika mazingira magumu. Leo, kutokana na ushirikiano wa kimataifa na miundombinu ya kisasa, matumaini yanaota mizizi tena kwenye udongo wa hapa.

Mradi huu si mradi wa kawaida wa miundombinu. Ni njia ya kuokoa maisha kwa zaidi ya kaya 12,000 za wakulima, ukikusudiwa kumwagilia hekta 8,000 za mashamba, 4,000 katika awamu yake ya kwanza, iliyopangwa kukamilika mwishoni mwa mwaka jana, na nyingine 4,000 zitafuata.

"Hili ni zao la kwanza," Odhiambo anasema, akielekeza kwenye mashamba yake ya mboga. "Baada ya hapa, tutabadilisha na mazao mengine kwa mzunguko ili kuboresha udongo na kuongeza mapato yetu. Hiki si kilimo tu; bali ni biashara sasa."

Waziri wa maji, usafi wa mazingira na umwagiliaji wa Kenya Eric Mugaa anasema, katika nchi nyingine nyingi za Afrika, ukosefu wa umwagiliaji pia husababisha changamoto kubwa ya uzalishaji kwenye kilimo na usalama wa chakula. Ingawa kilimo ni sekta muhimu nchini Kenya, asilimia 5 tu ya ardhi yote ya kilimo nchini humo ndio inayomwagiliwa.

Kwa utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji, wakulima wengi huko Siaya kando ya mto walikuwa na matumaini sawa na ya Odhiambo.

"Kabla ya mradi huu, tulilazimika kununua mboga na vyakula vingine," Florence Aoko Oduor anasema. "Sasa, tunaweza kulima mazao yetu wenyewe. Yanalisha familia zetu na mifugo yetu. Maji yamebadilisha kila kitu."

Oduor anasema kwamba kwa sasa wana maji mengi, mfereji uliojengwa na Wachina karibu na nyumba yake utamwezesha kubadilika kutoka kilimo cha kujikimu hadi mradi wa kilimo wenye faida.

Peter Onyango Okola, afisa wa kijiji huko Siaya, anaongoza kundi la wakulima zaidi ya 650 ambao wameona matokeo ya mradi huo.

"Sasa tunapata maji kupitia mfereji, ambao umebadilisha kila kitu," anasema. "Mashamba yetu hayako tena chini ya udhibiti wa hali ya hewa. Hii itaboresha usalama wa chakula na kuleta ajira kwa familia nyingi."

Kiini cha mafanikio ya mradi huu kinatokana na mbinu kamili ya kilimo cha kisasa. Miriam Otipa, mtaalamu mwandamizi wa kilimo wa mradi huo, anaelezea kwamba hii sio tu kuhusu kuongeza uzalishaji wa chakula bali ni kuhusu kuwaunganisha wakulima na masoko endelevu.

"Kwa miaka mitano iliyopita, tumewaelimisha wakulima na kuwapanga katika vikundi," anasema. "Sasa wanachagua mazao kulingana na udongo unaofaa, na kuhakikisha mavuno ya juu."

Ili kuleta fursa za soko za kutegemeka, mradi umeshirikiana na wakala ambaye huwapa wakulima mbegu, mbolea na bidhaa za ulinzi wa mazao, na baadaye hununua mavuno hayo kwa ajili ya kuuza katika mji wa karibu na Kisumu.

"Wakulima hawalimi tena kwa ajili ya kula tu. Wanalima ili kupata mapato," Otipa anasema. "Kwa umwagiliaji, wanaweza kuvuna hadi mara tatu kwa mwaka, ikilinganishwa na mara moja tu kwa kilimo kinachotegemea mvua. Hii ina maana chakula zaidi, mapato zaidi na fursa zaidi."

Kwa mradi ulioanza mwaka 2018 ukilenga kupunguza mafuriko na kuongeza ekari za ardhi inayomwagiliwa magharibi mwa Kenya, kuundesha kiufundi halikuwa jambo dogo. Francis Mburu, mhandisi mkazi wa mradi wa umwagiliaji, anakumbuka vikwazo vilivyowakabili wakati wa ujenzi.

Mifereji ya maji ilileta kikwazo kimoja katika utekelezaji wa mradi. Usanifu wa awali ulijumuisha mifereji tisa tu ya maji, ambayo haikutosha.

"Tuliongeza idadi hiyo ya mifereji hadi 76," Mburu anasema. "Jambo hili limetatua masuala ya magogo ya maji na kulinda miundombinu ya mifereji."

Wang Jianfei, mhandisi wa China wa mradi huo, anasema umeleta ajira, umeongeza mapato ya wenyeji na hata kupunguza uhalifu. "Tunashuhudia jamii iliyo salama na yenye matumaini zaidi ikiibuka."
 
Back
Top Bottom