Nimemsikia Tido akiuelezea huu mradi katika kipindi cha Pongezi za mwaka mpya kilicho rushwa na Radio yao na aliielezea kuwa unategemewa kuanza majaribio katika mwezi huu wa January kwa Mkoa wa Dar kwa kuanzia na wale wanaohitaji watatakiwa kuwa na Decoder na alisema kwa kuanzia itakuwa na channel zisizopungua 40 ila alifafanua na kusema kuwa inategemewa kuwa na channel kama 200 hivi ambazo zitalipiwa kwa bei nafuu. ukilinganisha na DSTV.
nasikia wameanza kuuza vifaa vyao wanauza eflu 79000
Mimi sijauelewa bado ila ninayo decoder yake na ni nzuri tu japo ina channel nyingi zisizo na maana, na chache ninazozipenda, zinanitosha sana, ila inabidi wafanyie kazi foleni ya kulipia kwani kila mtu atakuwa na yake, bora waweke electronic mode ya kulipia
Kabla ya kwenda huko kote, TBC wangeanza kwanza na kurekebisha mitambo yao ya sauti au wale mafundi mitambo wa sauti wawajibike au wapige msasa ujuzi.
Yaani ikifika wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku mpaka inakuwa kero. Sauti mara ipande yenyewe mara ishuke bila ya mpangilio.
Na ikifika wasaa wa habari za uchumi na biashara yule bwana mdogo Stanley inakuwa kama vile anaongea lugha ya kigeni na kisha kufanyiwa dubbing. Mienendo ya midomo yake na matamshi ya maneno hata haviwiani.
Inakera
Superman,
Kosa ni kuwapa Wachina 65% ownership ya TBC na sisi kubaki na 35%. Huwezi tena kuiita hiyo Tanzania Broadcasting Corporation . Ni China Broadcasting Corporation.
Hizo gharama za digital tungeweza kuzimudu sisi wenyewe, ila siku hizi Tanzania mindset ya viongozi wetu ni kwamba "No we can't. Only foreigners can."
nope ni 70000 kwa decoder na elfu 9 ni malipo ya mwezinasikia wameanza kuuza vifaa vyao wanauza eflu 79000
Kwa hiyo dar mnapata hizo channel 30? Mbona hawa jamaa wa DSTV na wengine wa cables watakoma!
Haika, hebu tupe kwa undani kidogo. Decoder umenunua wapi? bei gani? unapata channel ngapi jumla? kwa jinsi ulivyoona, ni zipi ni nzuri??
Hizo decoder zinatembezwa maofisini nafikiri hata ukienda pale TBC mikocheni zipo.Bei yake ni elfu 70,000 na kulipia channel elfu 9000/= kwa mwezi.
channel wanazogawa ni 30 lakini nyingi zina kwikwi,hivyo zinazoonekana vizuri ni kama 15.
Channel nzuri ni bbc,aljazera,tbc,channel ten,tbn,citizen,bet,setanta,na stve