Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere, Rais Samia umetuheshimisha

Mama hataki dhulma.

Hatuna shida na mkataba maana hata yule dhalimu hakutuonesha mkataba wa ununuzi wa ndege, SGR, mwendokasi, ujenzi wa barabara na madaraja, flyover, stigilazi goji, ujenzi mjibwa chato, n.k
Ati EEE? Msifieni Tu huku mnamlamba kisogo
 
NILIAMINI NIKO SAHIHI, LEO MAMA UMETUSHINDIA

Na Yericko Nyerere

Hureeeeee vita vyetu kwa maslahi ya Taifa tumeshinda! Asante Rais Mama Samia suluhu Hassan, nilimpinga Magufuli alipositisha mradi huu kwa hoja dhaifudhaifu na za uongo wa kiwango cha rami. Nikampinga baada ya kufariki baada ya wapambe wake kuendelea kukomaza shingo.

Now naweza kusema Mama umetuheshimisha sisi wataalamu tuliofanya kazi kubwa kujenga hoja na kushauri umuhimu wa mradi huu kwa maslahi ya Taifa kwa uchumi wa Reli ya SGR.

Naomba niwarejeshe nyuma miaka miwili iliyopita 22 December 2019 nilipoandika Makala nikipinga hotuba ya Rais Magufuli akikataa kuendelea na ujenzi wa Mradi ya Bandari ya Bagamoyo, nilipinga hoja alizozijenga Rais ili kuhalalisha katazo lake juu ya mradi husika.

Nilieleza wazi kwamba, Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake.

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili ya ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji katika ardhi kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

Chakusikitisha kwa nchi yangu, Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi Rais Magufuli kusitisha mradi, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5 za Kimarekani, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo kwakuwa ukihojihoji tu basi ukinusurika sana utaenda mochwari au Ubelgiji, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against na himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa hii tuliyonayo leo ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho kilikuwa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence). Lakini bahati mbaya muundo na aina ya uongozi wa Magufuli ulikiingiza katika siasa pale kilipofanywa kuwa decision maker wa nchi, lakini upande wa foreign assets ndio wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi...

Kwahatua hii naomba niseme wazi, Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere kule Rufiji ama ungeanza kabla ya SGR, Now sasa nasema taifa linakwenda kushinda vita vya kiuchumi afrika mashariki na kati.

Kuanzia sasa atakayempinga mama nitamloga nitamloga

Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
View attachment 1830718
Leo katika taarifa ya habari ya Channel Ten nimemsikia Rais mtarajiwa wa awamu ya tano Ngoyai Lowassa akisema kwamba Serikali yake itaangalia jinsi ya kuuvunja mkataba wa bandari ya Wachina Bagamoyo.8

Amesema haoni mantiki ya kutumia mabilioni kujenga bandari moja Bagamoyo wakati bandari za Tanga na Mtwara ziko ovyo.

Kama kawaida wananchi wa Tanga wamesema kura zao zote ni kwa UKAWA na adui CCM lazima asome namba mwaka huu.

VIVA UKAWA!
 
Sasa nisimuamini kwanini wakati yeye ndio akikuwa rais?
Ndio akili mlishikiwa na jiwe kila alichokuwa anawaambia mnaamini tuu,na kwa hilo alifanikiwa kweli kuwalisha matango pori

Nb:rais ni malaika nin,hata angetaka kukuinamisha ungekula kwasababu ni raisView attachment 1830836
IMG_20210415_161255.jpg
 
Marehemu, nasita kutamka, lakini siamini kama alikuwa sawasawa. Kilichokuwa kinanishangaza ni namna alivyokuwa mwongo na kuendesha nchi kwa kuwahadaa watu ambao kwa kiasi kikubwa, walikuwa na uelewa mdogo.

Wengine aliwadanganya, akawajaza ujinga wa ajabu, mpaka leo wametopea kwenye ujinga waliojazwa na marehemu. Na wanaamini kuwa marehemu alikuwa kiongozi mzuri sana.

Katika marais wote tuliowahi kuwa nao, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kuwa mwongo kama marehemu.

Aliwadanganya watu kuhusu madini, aliwadanganya watu kuhusu gas, aliwadanganya watu kuhusu korosho, aliwadanganya watu kuhusu hali ya uchumi wetu, aliwadamganya watu kuhusu mradi wa Bagamoyo. Ilikuwa vigumu sana kwake kuhutubia hata mara moja, bila ya kuongea uwongo.

Siamini kabisa kama alikuwa sawasawa.
Halafu kuna watu mpaka ss hivi bado wanaendelea kumwamini sijui aliwalisha nin,mmojawapo alieshindwa kuficha mahaba yake kwa mwendazake ni huyu bwana anaejiita Crimea nadhan ana kamtt kwa mwendazake
 
Ingawa sijasoma makala yako kwa urefu swali langu ni moja tu..

Huo Mkataba umeuona ?, Nadhani hapo ndio tutaondoa mzizi wa fitina na kujua ukweli na uongo ni upi, Na ili tusiibiwe issue sio kupiga chini mradi moja kwa moja bali ni kufunga mikataba ambayo ina tija kwetu...

Na hilo litawezekana tu kama kuna transparency
Akikujibu kwa ufasaha hapa,nitag . Swali la msingi sana. Hili ndilo ilitakiwa liwe la kwanza ajiulize na apate majibu kabla ya kuja hapa jukwaani. Mwisho wa siku wachina sio watu kabisa kwenye hizi nchi za Africa. Tusije tugeukana baadae baada ya kujua hamna tunachonufaika zaidi ya sifa tu kwamba tuna bandari kubwa
 
Miradi ya namna hiyo ipo kwenye mataifa mengi. Timu ya wataalam ilizunguka kwenye mataifa mengi kuangalia namna miradi ya namna hiyo jinsi inavyomilkiwa na inavyoendeshwa. Kwa kiasi kikubwa ilikuwa copy and paste. Mradi huu ulifanyiwa kazi na wataalam wengi kwa muda mrefu. Marehemu, sijui aliusoma kwa siku ngapi, akaufuta haraka haraka.

Alichokiona ni hiyo ya TRA kutofanya makusanyo ya moja kwa moja kwenye bandari. Na kingine ilikuwa ni umiliki wa miaka 99, akasema wamepewa wachina, jambo ambalo halikuwa kweli. Umiliki utakuwa kwa 3 entities - Tanzania, China na Oman.

Kwenye gas aliharibu kabisa, baadaye akadanganya kuwa gas wamepewa Wachina. Lakini wakati huo huo alimtuma Mwanasheria Mkuu kwenda kuwabembeleza wawekezaji warudi, wakakataa. Huku anawabembeleza, huku anasema gas imeuzwa. Sasa makampuni yaliyokuwa yanamiliki vitalu vya gas yataanza ujenzi wa LNG plant, uwekezaji wa dola bilioni 30, mwaka 2023. Kama gas iliuzwa China, hao wanakuja kuchimba gas gani?

Kwenye madini, Kabudi alifanya mabadiliko ya sheria ya madini, mabadiliko ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa very unprofessional. Kwenye mabadiliko yale, walisema in case of any dispute, makampuni yatalazimika kutumia mahakama za ndani. Lakini makubaliano na Barrick yanasema:

1) kama kuna dispute, pande mbili zitajitahidi kumaliza kwa njia ya maelewano.

2) wakati wa dispute, Serikali haitaruhusiwi kusimamisha uzalishaji

3) ukipita mwezi mmoja bila pande mbili kukubaliana, mahakama ya biashara ya Singapore itatarifiwa, nayo itatoa uamuzi, na uamuzi wake hautakatiwa rufaa popote

Masharti haya ni aheri hata yale yaliyokuwemo kwenye MDA wakati wa Kikwete. Hapa walionufaika ni Barrick.
Unatumia nguvu sana kumwelewesha huyo punguani,bado mahaba yake yapo kwa mwendazake haamini kilichotokea march 17
 
Lowasa wakati wa kampeni kupitia UKAWA alisema akishinda urais, mkataba wa hiyo badandari atauvunja na Yeriko alishangilia kauli hiyo ya Lowasa
Uongo huo mkatabata gani angwvunja wakati hadi leo hakuna mkataba uliosainiwa badala yake ni mapendekezo tu ndio yalisitishwa na Dikteta Magufuli?
 
Uongo huo mkatabata gani angwvunja wakati hadi leo hakuna mkataba uliosainiwa badala yake ni mapendekezo tu ndio yalisitishwa na Dikteta Magufuli?
Kwahiyo wewe na Lowasa aliekuwa waziri mkuu nani muongo?

Unaweza kutuwekea hayo mapendekezo hapo?
 
Andiko la Yericko akimpongeza Magufuli kwakushinda vita ya uchumi.

Kama umesoma na kuelewa nilichoeleza katika pongezi hizi kwa dikteta Magufuli na hiki nilichoandika leo utaona wazi leo sipingi mradi wa umeme bali nimependekeza kuwa bandari ingeanza kisha umeme na SGR vifuate
 
Kwahiyo wewe na Lowasa aliekuwa waziri mkuu nani muongo?

Unaweza kutuwekea hayo mapendekezo hapo?
Hakuna mahali Lowasa alipowahi kusema atavunja mkataba wa Bandari ya Bagamoyo.

Asingevunja kitu kisichokuwepo. Hadi Dikteta Magufuli anaingia madarakani kulikuwa hakujaingiwa mkataba bali kulikuwa na majadiliano ya mkataba. Kilichokuwepo ni majadiliano na sio mkataba
 
Hakuna mahali Lowasa alipowahi kusema atavunja mkataba wa Bandari ya Bagamoyo.

Asingevunja kitu kisichokuwepo. Hadi Dikteta Magufuli anaingia madarakani kulikuwa hakujaingiwa mkataba bali kulikuwa na majadiliano ya mkataba. Kilichokuwepo ni majadiliano na sio mkataba
Uzi wake uko hapa!

Inawezekana wakati anaongea hayo wewe ulikuwa unatumbua hela alizokuja nazo kuinunua UKAWA hivyo usingeweza kusikia.

Tuaachane na hayo! Je, unaweza kutuwekea hayo makubaliano hapa ili tuone uongo wa huyo dikteta wako?
 
Hakuna mahali Lowasa alipowahi kusema atavunja mkataba wa Bandari ya Bagamoyo.

Asingevunja kitu kisichokuwepo. Hadi Dikteta Magufuli anaingia madarakani kulikuwa hakujaingiwa mkataba bali kulikuwa na majadiliano ya mkataba. Kilichokuwepo ni majadiliano na sio mkataba
Kwa hiyo wewe sababu ya kuunga mkono mradi huu ni kumkomoa magufuli? Haya ni maajabu
 
Back
Top Bottom