Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere, Rais Samia umetuheshimisha

Ingawa sijasoma makala yako kwa urefu swali langu ni moja tu..

Huo Mkataba umeuona ?, Nadhani hapo ndio tutaondoa mzizi wa fitina na kujua ukweli na uongo ni upi, Na ili tusiibiwe issue sio kupiga chini mradi moja kwa moja bali ni kufunga mikataba ambayo ina tija kwetu...

Na hilo litawezekana tu kama kuna transparency
Kwan mkuu ww kuna mkataba uliokwishawah kuuona??Mbna unapose question kwenye mkataba huu Tu wa bagamoyo!!
 
Kama umesoma na kuelewa nilichoeleza katika pongezi hizi kwa dikteta Magufuli na hiki nilichoandika leo utaona wazi leo sipingi mradi wa umeme bali nimependekeza kuwa bandari ingeanza kisha umeme na SGR vifuate
@yeriko.hv Kati ya umeme na badari kipi kinafaida kubwa?? Eleza namna mladi wa bagamoyo utakovyo mnufaisha mtu alieoko uvinza au nyakahoza??
Think big yeriko au nawe umooo??
 
Marehemu, nasita kutamka, lakini siamini kama alikuwa sawasawa. Kilichokuwa kinanishangaza ni namna alivyokuwa mwongo na kuendesha nchi kwa kuwahadaa watu ambao kwa kiasi kikubwa, walikuwa na uelewa mdogo.

Wengine aliwadanganya, akawajaza ujinga wa ajabu, mpaka leo wametopea kwenye ujinga waliojazwa na marehemu. Na wanaamini kuwa marehemu alikuwa kiongozi mzuri sana.

Katika marais wote tuliowahi kuwa nao, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kuwa mwongo kama marehemu.

Aliwadanganya watu kuhusu madini, aliwadanganya watu kuhusu gas, aliwadanganya watu kuhusu korosho, aliwadanganya watu kuhusu hali ya uchumi wetu, aliwadamganya watu kuhusu mradi wa Bagamoyo. Ilikuwa vigumu sana kwake kuhutubia hata mara moja, bila ya kuongea uwongo.

Siamini kabisa kama alikuwa sawasawa.
mbaya kabisa akawadanganya na chadema kwenye siasa mpaka sasa wamekwenda na maji.

ukituliza kichwa chako sawa sawa unaiona bandari ya bagamoyo kama geti la uchumi labda,vipi bandari ya dsm unaiweka wapi??
 
Pale Twiga ni upuuzi mtupu. Hakuna mabadiliko chanya. Ungejua kilichomo kwenye mkataba usingesifu chochote. Hakuna anayeweza kuutoa hadharani ule mkataba, kutokana na aibu. Magufuli was a good president for the fools.
kwamba una guts zote za kuita watu fools!!!

mkuu kujiona una akili zaidi nao ni ugonjwa.
 
Hakuna mahali Lowasa alipowahi kusema atavunja mkataba wa Bandari ya Bagamoyo.

Asingevunja kitu kisichokuwepo. Hadi Dikteta Magufuli anaingia madarakani kulikuwa hakujaingiwa mkataba bali kulikuwa na majadiliano ya mkataba. Kilichokuwepo ni majadiliano na sio mkataba
Kama kulikuwa hakuna mkataba contraction ilikuwa ya nn?? Unanajua mkataba huo ulisainiwa lini na katika awam ipi??

Mkuu think big.. ndo maana mashart yake magumu
 
Nimkomoe nani? Nimkomoe marehemu? Kwani huo mradi ukiwa na manufaa au hasara, ataathirika marehemu? Yeye amemaliza safari yake, tuliobakia tuangalie kilicho chema kwaajili yetu na vizazi vijavyo.

Mimi siendeshwi na ushabiki au chuki kwa msingi wowote ule, naangalia kilichomo kwenye hoja.
aaah weee usikimbie kisogo chako.

chuki kwa magufuli ni kiini cha upinzani wako kwake,mengine ni miamvuli tu ya kujifichia.
hauwezi kusema mtu alikuwa mwongo kupita kiasi,alidanganya wapi,kuhusu nini??
mtu akikwambia gari lako ni bovu,kufika safari uliyokuwa uende hakumfanyi yeye kuwa mwongo.

nakuulize swali rahisi tu,kwanini ujenzi wa bandari ya nne kubwa zaidi wakati tatu zilizopo hazijapewa uwezo stahiki!!!
 
NILIAMINI NIKO SAHIHI, LEO MAMA UMETUSHINDIA

Na Yericko Nyerere

Hureeeeee vita vyetu kwa maslahi ya Taifa tumeshinda! Asante Rais Mama Samia suluhu Hassan, nilimpinga Magufuli alipositisha mradi huu kwa hoja dhaifudhaifu na za uongo wa kiwango cha rami. Nikampinga baada ya kufariki baada ya wapambe wake kuendelea kukomaza shingo.

Now naweza kusema Mama umetuheshimisha sisi wataalamu tuliofanya kazi kubwa kujenga hoja na kushauri umuhimu wa mradi huu kwa maslahi ya Taifa kwa uchumi wa Reli ya SGR.

Naomba niwarejeshe nyuma miaka miwili iliyopita 22 December 2019 nilipoandika Makala nikipinga hotuba ya Rais Magufuli akikataa kuendelea na ujenzi wa Mradi ya Bandari ya Bagamoyo, nilipinga hoja alizozijenga Rais ili kuhalalisha katazo lake juu ya mradi husika.

Nilieleza wazi kwamba, Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake.

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili ya ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji katika ardhi kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

Chakusikitisha kwa nchi yangu, Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi Rais Magufuli kusitisha mradi, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5 za Kimarekani, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo kwakuwa ukihojihoji tu basi ukinusurika sana utaenda mochwari au Ubelgiji, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against na himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa hii tuliyonayo leo ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho kilikuwa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence). Lakini bahati mbaya muundo na aina ya uongozi wa Magufuli ulikiingiza katika siasa pale kilipofanywa kuwa decision maker wa nchi, lakini upande wa foreign assets ndio wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi...

Kwahatua hii naomba niseme wazi, Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere kule Rufiji ama ungeanza kabla ya SGR, Now sasa nasema taifa linakwenda kushinda vita vya kiuchumi afrika mashariki na kati.

Kuanzia sasa atakayempinga mama nitamloga nitamloga

Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
View attachment 1830718
Juzi mama aliongea na rais wa China kwa simu ya kiganjani. Leo mama kasema bandari inajengwa............??????!!!!!!!!##
 
Hii nchi hatuwezi kutoka kwenye mkwamo kwa kuogopa kuchukua maamuzi makubwa yenye maslahi mapana kwa Taifa eti kwa sababu uwekezaji unasimamiwa na sekta binafsi.

Hata Uganda wangekomaa na ujinga wa kusema eti wapate 50/50 na Total hakuna kitu wangefanya hadi leo.

Uchumi sio Kodi tuu bali value chain ya mradi husika,imagine tumepoteza mradi wa LPG Lindi dola za kimarekani bil.30,,hizi pesa zingeingia kwenye uchumi wetu leo tusingekuwa tunaongelea madarasani na vyoo vya watoto.

Uzuri wa miradi hii mikubwa inajenga taswira nzuri kwa wawekezaji wengine kwamba kumbe nchi ina stable economic policy na hivyo ingefungua fursa kwa wengine.

Nchi hii iko vizuri kiusalama na kwa hiyo ilotakiwa kuwa kitovu cha uwekezaji kwa EAC yote maana hatuna changamoto za kiusalama kama kwingine.

Mama Songs na miradi yote iliyokwama kwa miaka na miaka ,tukipata robo tuu kwenye kila mradi inatosha sana maana value chain yake itaifaidisha nchi kuliko kuangalia kodi za directly
 
Wewe na Lowasa aliekuwa waziri mkuu, ambae kipindi cha kampeni kupitia UKAWA alisema akishinda atavunja huo mkataba wa bandari ya bagamoyo nani wa kuaminiwa zaidi?

Ifike wakati mashabiki wajinga wa chadema mjue kwamba kwenye huo mkataba kama kuna madudu atakae umia siyo Magufuli bali ni bibi, babu, baba, mama na koo zenu huko vijijini.
Kama akili yake ndo ilipoishia sasa ulitaka asemaje?

Swala ni kuvunja mkataba au kuuboresha?
 
NILIAMINI NIKO SAHIHI, LEO MAMA UMETUSHINDIA

Na Yericko Nyerere

Hureeeeee vita vyetu kwa maslahi ya Taifa tumeshinda! Asante Rais Mama Samia suluhu Hassan, nilimpinga Magufuli alipositisha mradi huu kwa hoja dhaifudhaifu na za uongo wa kiwango cha rami. Nikampinga baada ya kufariki baada ya wapambe wake kuendelea kukomaza shingo.

Now naweza kusema Mama umetuheshimisha sisi wataalamu tuliofanya kazi kubwa kujenga hoja na kushauri umuhimu wa mradi huu kwa maslahi ya Taifa kwa uchumi wa Reli ya SGR.

Naomba niwarejeshe nyuma miaka miwili iliyopita 22 December 2019 nilipoandika Makala nikipinga hotuba ya Rais Magufuli akikataa kuendelea na ujenzi wa Mradi ya Bandari ya Bagamoyo, nilipinga hoja alizozijenga Rais ili kuhalalisha katazo lake juu ya mradi husika.

Nilieleza wazi kwamba, Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake.

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili ya ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji katika ardhi kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

Chakusikitisha kwa nchi yangu, Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi Rais Magufuli kusitisha mradi, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5 za Kimarekani, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo kwakuwa ukihojihoji tu basi ukinusurika sana utaenda mochwari au Ubelgiji, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against na himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa hii tuliyonayo leo ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho kilikuwa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence). Lakini bahati mbaya muundo na aina ya uongozi wa Magufuli ulikiingiza katika siasa pale kilipofanywa kuwa decision maker wa nchi, lakini upande wa foreign assets ndio wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi...

Kwahatua hii naomba niseme wazi, Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere kule Rufiji ama ungeanza kabla ya SGR, Now sasa nasema taifa linakwenda kushinda vita vya kiuchumi afrika mashariki na kati.

Kuanzia sasa atakayempinga mama nitamloga nitamloga

Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
View attachment 1830718
What a load of rubbish. Mbunge Godbless tunammiss sana kwa busara zake, hapa angetusaidia

Eti:
............Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote ISIPOKUWA ARHI na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na UTAALAM........

Hapa unamaanisha kuwa ardhi haina thamani, kwa sababu hizo $10billion zingerudi kwenye mapato ya kodi unazoziita ZA UBIA. If it is so simple kwa nini hawakubaki huko huko kwao? Ni kwa sababu hawana ardhi ndiyo maana wakaja hapa. Kwa nini hawakuenda Argentina au Mongolia au Finland? Kwa sababu hawana Bandari ya Bagamoyo. Ardhi is a rare commodity, to them, si ya kubeza.

Umesema wangeleta utaalamu? Mbunge Lema hizo uwa anaziira PowerPoint presentations.

Anawejeza $10 billion, payback period within 3 years kama bandari itachakarika kama wanavyodai, miaka 99 ya nini? TPA sasa hivi wanakusanya kiasi hicho kila mwaka.

Huko nyuma mikataba ya PowerPoint presentations inetuumiza sana. Makaburu walipoweka "investment" kufufua TBL walipata majumba ya thamani uzu guni, wakayauza kwa mabalizi na kuwejeza Treasury bills zeny yield ya 60% wakati huo, hela yao yote inaudible within 18 months,not 99 years. TTCL walitaka kufanya hivyo hivyo, na Barrick Gold, tukagutu Magufuli akawa firm.

Tunaisubiri kwa hamu hii bandari tuoneshwe PowerPoint presentations.
 
Faidi ipi sasa wewe MpK leo accacia umepata faida gani.. Shule 3 zilizojengwa karibu na mgodi.. Mali hiyo ingekuwa tumejenga wenyewe hata kwa pesa za mkopo ingekuwa na maana kinacho chosha zaidi hata ujuzi hutopati kupitia ujenzi huo.. Je in 10 year tunaweza jenga kama hiyo ya bagamoyo pale Tanga kutumia watu wetu. Je kwanini pesa hizo zosingeendeleza bandari ya Tanga kwanini kuwe na bandari za Dar na Bagamoyo karibu swali lengine bandari ya Dar kazi yake itakuwa ni nini. Tanga ndio ingekuwa inafaa zaidi kwasababu ni karibu na mikoa mingi ya kaskazi na kati.
Mkiwa mnashabiki kitu naomba muwe subjective na objective simultaneously sio kuwa na shauku na hisia tuu.
Nna uhakika location ya bagamoyo wameifanya kutokana na strategic kulingana na upembuzi waliofanya wataalamu wangeweza kwenda kokote.

Habari ya accacia hapo nakuunga mkono ila ni tofauti kwa kuwa mradi wa madini huwa unafika muda madini yanaisha tofauti na bandari na strategic location kijiografia haina mwisho. Huwezi kufananisha swala la madini na bandari kuna walafi wachache wamefikiri kwa kutumia matumbo yao hawakuwaza kizazi kijacho cha taifa hili kwenye madini.
 
Mkuu sa iv watu wote waliokuwa adui wa serikal ni marafik wa serikal subr tu uone huko mbele
Inaonekana hao watu ndiyo wazalendo wa kweli. Hawaangalii chama bali wanaangalia maslahi ya nchi.

Mama Samia, nina imani kubwa ana uzalendo wa hali ya juu. Anaangalia zaidi Taifa kuliko matakwa ya wajinga waliopo ndani ya chama chake.

Mimi kwangu kilicho muhimu siyo CCM wala CHADEMA au CUF au ACT, kilicho muhimu ni Taifa letu.

Kama kutakuwa na kiongozi mzuri ndani ya CCM hii mbaya, kiongozi asiye mnafika na mwongo kama alivyokuwa marehemu, nitamwunga mkono kiongozi huyo.
 
Mama kawekwa mfukoni na uncle aliyesema msibani Hana ugomvi na marehemu. TATIZO. Bora wamchukue mfumgwa wao tu.
 
Inaonekana hao watu ndiyo wazalendo wa kweli. Hawaangalii cha bali wanaangalia maslahi ya nchi.

Mama Samia, nina imani kubwa ana uzalendo wa hali ya juu. Anaangalia zaidi Taifa kuliko matakwa ya wajinga waliopo ndanibya chama chake.

Mimi kwangu kilicho muhimu siyo CCM wala CHADEMA au CUF au ACT, kilicho muhimu ni Taifa letu.

Kama kutakuwa na kiongozi mzuri ndani ya CCM hii mbaya, kiongozi asiye mnafika na mwongo kama alivyokuwa marehemu, nitamwunga mkono kiongozi huyo.
Sawa
 
Akiandika yericko mwisho kabisa anatangaza kitabu na bei zake utasikia ujajsusi wa kidola
 
Wachina hadi leo hii wanahaha na mkataba mbovu wa Hong Kong - (UK wa miaka 100), sisi tutaweza kuwanusuru vizazi vijavyo kwa mkataba ambao unaangalia maslahi ya familia ya Jakaya Kikwete?

Huo mkataba lazima uwekwe wazi vinginevyo utaleta shida sana hapa Tanzania. Hatuwezi kukubali kuburuzwa na watu ambao akili zao zimeshikiliwa na ma-NGO's.

BTW priority ya SSH ni economic rights and justice ya ulimwengu tunaomba aachie uongozi wa Tanzania. Hatuwezi kuwa na kupe anayewafyonza Watanzania kwa maslahi ya wengine.
Uliwahi kudai Mkataba wa ununuzi wa Ndege na ujenzi wa kiwanja Cha Ndege chato?
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom