Mr Sugu na Mkoloni Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Mr Sugu na Mkoloni Wajiunga Rasmi na CHADEMA

wakati mwingine tusiangalie kujiunga tu bali ni nani anajiunga na chama fulani. hao jamaa wataweza kuleta ushawishi gani kwenye mabadiliko ya upigaji kura? jina tu si hoja bali elimu ya kutosha pia. siasa si mashairi useme utakaa chini na kuandika kisha uende studio kurekodi. lakini kama wana nia ya dhati basi wafanye hivyo.
Mkuu Kingi

Kujiunga na chama huwa hatuangalii majina wala elimu ya mtu, yeyote anayetimiza masharti ya chama anaweza kuwa mwanachama hata kama hajui kusoma wala kuandika, labda utuambie mtu kuchaguliwa kuwa kiongozi au mpigadebe rasmi wa chama hapo ndipo tunaweza kuangalia who is who.

Ingawa sijui elimu ya Mr. Sugu na Mkoloni lakini wanaonekana wanaimudu vilivyo fani yao, hivyo endapo watakuwa wapiga debe wa Chadema wanaweza kuleta changamoto katika kampeni na kuvutia wapiga kura wengi hasa vijana.

Wakati CCM wanawachagua Hadija Kopa na Komba kuwapigia debe sijui kama walifanya interview au kuitisha vyeti vyao lakini huwa wanaleta changamoto kubwa sana wakati wa kampeni.
 
hONGERENI SANA MAKAMANDA WAPYA, mjitofautisha na vijana wasomi watarajiwa wa UDOM. Mmeamua kwwa dhati kutetea hakki ya wengi katika mazingira hatari. Nimefarijika kuona mnaungana na wapiganaji wachache wa kweli. tuko pamoja katka vita hii ya ukombozi. Hakuna kurudi nyuma ni kusonga mbele.

Natamani Mrisho Mpoto aungane na makamanda hawa katika vita hii takatifu juu ya ufisadi. Nawaunga mkono asilimia mia.
 
Harakati za kumkomboa Mtanzania zinasonga! Aluta Continua!!
 
Jamani tupige kura mwaka huu kukiondoa madarakani hiki CHAMA CHAWALA, INAWEZEKANA!!!. CCM HAIKUBALIKI, TOKOMEZA CCM!!!
 
......thumb up my model artist Mr. II a.k.a Sugu na wengineo kwa kufanya ambacho wasanii wengi hapa Bongo wanashindwa kuthubutu kwa kuhofia mikwara ya manyang'au CCM. kwa miaka nenda rudi 'hakimiliki' imekuwa ni isue ya blaah blaah......in reality serikali kupitia wizara zake (Utamaduni, viwanda/masoko na sheria) lazima zishughulikie seriously lakini who cares....watawahitaji kutumbuiza kwenye matamasha yao na kampeni zao tu nothing else!!! kama serikali inatukana na kudharau waajiriwa wake kabisa (public servants) itakuwa wao wa informal sector? waungane na kina Mkoloni kupitia chama hiki makini kutetea maslahi yao na taifa kwa ujumla. kwa stahili yao ya kuuza viwanja vya wazi soon or later hata hiyo Leaders Club utasikia imeuzwa!!

........Stand up and fight for your rights.........if you wait them to leave the offices they never leave, let's kick their assholes out the office this November!!!!!!
 
Binafsi nakichukulia kitendo hiki cha Mr 2 na wenzake in a different perspective, kinawakilisha jamii kubwa ya watanzania ambayo sasa imeanza kuthubutu, ile hali ya woga taratibu inaanza kupungua. Ingawa wazazi wetu walio wengi wameshindwa kabisa kuishi bila CCM, sisi vijana tujaribu na nina imani kabisa huo ndio utakuwa mwanzo wa ushindi (dare to) inawezekana aluta continua.
 
Nawapongeza sana Wakina Sugu na wenzake kwa uamuzi ambao watu wengi sana wa kuona kuwa wengine wanajiunga katika CHADEMA. Tunahitaji watu na mabadiliko ya kweli katika siasa za Tanzania, watu hawa kweli wanaharakati kwa kujiunga CHADEMA
 
Bora wasanii wameonyesha uthubutu, kuliko wasomi wetu wa vyoo vikuukuu.

dat is true wakisubutu wasomo wa vyuo vikuuu tanzania ingebadilika ila ni wachache wengi wao sijui hawna uxhungu na nchi hii au wnasomea elimu ya sayansi ya siasa ya nini sasa, kama hawataki kujitokeza moja kwa moja
 
Hii ni habari mbaya sana kwa CCM kwani hizi ni ishara wazi kwamba kizazi kipya kiko tayari kufanya kile ambacho CCM imejiaminisha kwamba watanzania hawawezi kukifanya nacho ni kuing'oa CCM madarakani.

Kazi iliyopo sasa ni hawa wasanii kutumia vipaji vyao kuhamasisha vijana wengine kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura zitakazoing'oa CCM.

Ttanzania mpya bila CCM yawezekana
 
Kweli Kabisa Mmechagua chama Kizuri zaidi chenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo na kupigania haki ya watanzania
 
Wasanii maarufu wa muziki nchini Tanzania Joseph Mbilinyi aka Sugu lias Mr II, Fred Malick aka Mkoloni na Gerald Mwanjoka aka G. Solo wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kukabidhiwa kadi zao za uanachama. Tukio hilo limechukua nafasi katika Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Pichani ni wanamuziki hao na Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mnyika.

Mwanamuziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi Mr Sugu akipokea katiba ya CHADEMA, kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, baada ya kujiunga rasmi na chama hicho leo katika Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni, jijini Dar. Chanzo, habari Zaidi na picha:
BOFYA HAPA
 
Back
Top Bottom