Hongereni sana wakuu!
Hongera pia kwa wote wanaopenda mabadiliko. Imekuwa ni jambo la kawaida katika nchi yetu wengi kushabikia CCM kwa kuwa wanaamini watafaidika kwa namna mbalimbali. Ndio maana hata wasomi wetu, wafanyabiashara hata watu walio nchi za nje kwa utashi wao wa ubinafsi wamekuwa mstari wa mbele kushabikia na kuchangia CCM wakiamini kuwa nao hawatasauliwa kwenye kupewa kipande cha keki. Ukweli wa nini wanakishabikia wanaujua wenyewe. Sijashawishika bado kuamini kuwa hao wote wanadhani CCM inafanya vyema katika kuongoza taifa hili, na kwamba hakuna watanzania wenye uchungu na kuhitaji mabadiliko, au hivyo ndivyo tulipaswa kuwa hata kama tungekuwa na viongozi bora. Kwa mantiki hiyo hata wasanii wetu wengi wamekuwa wakiingizwa kwenye mkumbo huo.
Kwa upande mwingine, mtu anayeeleza ukweli kadri anavyouona amekuwa adui mkubwa wa CCM na wapambe wao. Ukiona mtu yuko tayari kuueleza ukweli huo hadharani na mchana kweupe, ni lazima tumheshimu huyo mtu, na kukubali kuwa anatumia kichwa chake kufikiri, na sio kusaidiwa na wengine kufikiri. Ndio maana mimi nawaheshimu sana watu wote ambao wako mstari wa mbele kuleta mabadiliko katika nchi yetu. Mabadiliko ni jambo la lazima sio la hiari.
Nawapongeza sana wakuu hao waliojitoa mhanga kuutetea ukweli. Tunajua kuna gharama za kuingiza mchanga kwenye keki ya CCM, lakini ni gharama ambayo ni haki kuipigania, hii nchi ni yetu sote na sisi tunahitaji kuleta mchango wa kuiendeleza.