MWK, Sheria ilibadilishwa na mafisadi waliopeana ruhusa ya kukupua mali za Watanzania kila kona ya Tanzania. Walikubaliana kwamba watakaposhtukiwa kama wanaiba na kusaini mikataba mibovu basi wakirudisha walichokipata karika ufisadi wao mambo yote yatakuwa shwari.
Huu ni usanii wa hali ya juu, wabunge wa CCM wangechachamaa wahusika wote wa kashfa ya EPA, Richmond n.k. waswekwe rumande wakati uchunguzi unaendelea basi nina hakika hilo lingetokea.
Wabunge wamebwabwaja hakuna chochote kilichofanyika watuhumiwa wote bado wako huru wakiendelea kufaidi mapesa yao ya ufisadi.
Nilishangaa kusikia bunge limeahirishwa hadi April. Mtaahirishaje bunge wakati nchi imegubikwa na kashfa nzito nzito chungu nzima, kwani wasingweza kuitisha kikao cha dharura cha bunge hata cha mwezi mmoja ili kuhakikisha watuhumiwa wote wanaswekwa ndani!? Usanii kila kona, halafu Chiligati atakwambia wao CCM ndio waliwawajibisha mafisadi! wakati bado wako uraiani wanapeta!
Yaani utawaweza,
hakusubiri hata afikishe post 20 ili aanze ufisadi!?!
mimi nashuhudia explosion tu hapa.... maana the first posts tu huyo kishaanza ohhh walongalongaji... mara mwanakijiji ndiye mwafrika wa kike ili mradi explosions tu! grrrrrrrrr
.
MWANAKIJIJI acha utoto ukiona unashindwa hoja unakimbilia kubadili jina na kutumia la kike ili upewe huruma(Mwafrika wa Kike)
MKANDARA.
Mwafrika wa kike ni yule yule Mwanakijiji ana utoto wa kuingia na majina mengine kama KOBA, MADELA-WA MADILU, MWAFRIKA WA KIKE n.k
turudi kwenye mada vyombo vyote vya habari vya kimataifa vimesema Bush anakuja Tz ili kufuata masilahi ya nchi yake na kusisitiza kuwa AFRICOM ni agenda kuu ya ziara ya bush.
kwanini yuko Arusha kwenye Tanzanite? Ukimwi uko Bukoba vipi hajaenda uko?
Mwanakijiji au Mwafrika wa kike.
mtafute professor JOEL BARKAN ...
Wananchi,
Kwanza nakubali kabisa ni muhimu hela ZIRUDI. Kama watachukuliwa hatua au la hilo litafuatia na sidhani ni jukumu la tume kuwaambia watafanya nini mbeleni.
Ila hatua waliofikia ni ya kupongezwa, Serikali haifanyi mambo kwa kukurupuka. Kumbuka ukisharudisha hela ni ushahidi tosha kuwa uliiba. Sasa tatizo ni nini hapo, au ndo ile dhana yetu kuwa lazima tupinge tuu hata kama ni jambo zuri?.
Lipi la maana kulweka Lupango aliyeiba au kurudisha?, mie naamini kuwa kama ameiba basi akiwa na uwezo wa kurudisha ni nzuri sana tena AKIRUDISHA NA RIBA kuliko kumfunga na watoto wakaendelea kukaa chini mashuleni na wagongwa kufa kwa kukosa madawa mahospitalini.
Asanteni sana
FD
Hivi sasa ndiyo kwanza nimemaliza kusikiliza tarifa muhimu kwamba ile Tume ya Rais ya EPA ya kuchunguza ubadhirifu wa fedha za malipo ya akaunti ya madeni ya nje pale BoT imeeleza kuwa imefikia mahali pazuri kutoa taarifa yake.
Tume hiyo katika taarifa yake imesema imeweza kusaidia kurejeshwa kwa kiasi kikubwa cha fedha zilizolipwa kitapeli kwa kampuni za kisanii.
Imesema kuwa mali zisizohamishika zimekamatwa maeneo mengi ya Dar na miji mingine, kuhusu mali zilizo ne ya Tanzania, tume hiyo imesema kuwa nazo zitapatikana karibuni kabla ya kukabidhi ripoti kamili kwa Rais Jakaya Kikwete..
Mwenyekiti amesema wananchi wote wanaombwa kutoa taarifa kwa tume hiyo kwa kutumia namba za simu zifuatazo
+255 784 994881
+255 784 231928
+255 784 785742
Haya jamani mambo yetu yale, kama mnafahamu mali za mafisadi wale wa BoT semeni ili turejeshe serikalini na ziuzwe kama hazihamishiki ili pesa zinazopatikana zikajenge barabara, kununua dawa, kuboresha elimu na dawa hospitalini.
Nawatakieni kila jema.
Usanii mwingine hata unavuka maelezo ya kawaida. Yaani ni lini sheria za nchi zilibadilishwa na kuruhusu watuhumiwa wa wizi kurudisha mali na sio kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.
Ina maana leo wale watuhumiwa wa wizi wa kuku na simu walioko Keko wanaruhusiwa kuachiwa huru as longer as wanarudisha kile walichoiba?
yaani wamerudisha mali ili yaishe kimya kimya. Basi si waambiwe tu warudishe mali yaishe. Maana kutakuwa na umuhimu gani wa kuwafikisha mahakamani wakati wamesharudisha mali?
Tuwe 'Optimistic'. Kama sikosei, JK aliipa tume/kamati kazi ya kuchunguza hili na kuhakikisha 1. Fedha zilizoibwa zinarudi, na 2. kuwachkulia hatua wote walihusika na wizi huo wa fedha za umma. Fedha kuanza kurudi kwa 'wenyewe' ni hatua nzuri, na bila shaka hatua hii itafuatiwa na kufikishwa katika sheria wahusika. Huenda kuanza kuwachukulia hatua mapema kutaharibu ushahidi au kuzorotesha upatikanaji wa fedha zetu.
Tazama chini hapo, halafu niambie umeshapata jibu au bado?
Ahsante JK kwa uongozi wako, wenye macho tunauona na wenye masikio tunausikia. uzi huo huo, tunakuombea Mwenyeezi Mungu akuepushe na mahasidi wasioona unachokifanya kwa roho zao mbaya na akuepusha na fitna na majungu na visasi vya hao unao-washughulikia.
Haya wale wanaolonga longer humu waanze kuonyesha uzalendo wao, namba hizo.
Ahsante JK kazi tunaiona. Wengine waanze kukaa mkao wakula zamu yao inakuja.
Hivi sasa ndiyo kwanza nimemaliza kusikiliza tarifa muhimu kwamba ile Tume ya Rais ya EPA ya kuchunguza ubadhirifu wa fedha za malipo ya akaunti ya madeni ya nje pale BoT imeeleza kuwa imefikia mahali pazuri kutoa taarifa yake.
Tume hiyo katika taarifa yake imesema imeweza kusaidia kurejeshwa kwa kiasi kikubwa cha fedha zilizolipwa kitapeli kwa kampuni za kisanii.
Imesema kuwa mali zisizohamishika zimekamatwa maeneo mengi ya Dar na miji mingine, kuhusu mali zilizo ne ya Tanzania, tume hiyo imesema kuwa nazo zitapatikana karibuni kabla ya kukabidhi ripoti kamili kwa Rais Jakaya Kikwete..
Mwenyekiti amesema wananchi wote wanaombwa kutoa taarifa kwa tume hiyo kwa kutumia namba za simu zifuatazo
+255 784 994881
+255 784 231928
+255 784 785742
Haya jamani mambo yetu yale, kama mnafahamu mali za mafisadi wale wa BoT semeni ili turejeshe serikalini na ziuzwe kama hazihamishiki ili pesa zinazopatikana zikajenge barabara, kununua dawa, kuboresha elimu na dawa hospitalini.
Nawatakieni kila jema.
Hali kadhalika kwa EPA, makampuni yanajulikana na humo inawezekana kabisa kuwa wamo waliokopa kwa nia safi na wamo waliokopa kwa nia ya kutorudisha, huwezi ukakurupuka na kuwakamata uwasweke ndani, utapata faida gani ukisha wasweka? Utakosa pesa na utaendelea kuwalisha bure jela. At the same time ukitumia busara kidogo utazipata pesa zitakazoweza kupatikana, utazipata mali utazoweza kuzishika na kuna uwezekano mkubwa wengi wakaanza kurudisha, na hili la kuzipata fedha na mali ndio kipaumble. Na yote hayo lazima ayashughulikie kisheria, akienda kimsobe-msobe kama unavyotarajia, atajikuta hana alichofanya ila ni hasara juu ya hasara.
Surely; at this stage, ambapo bado kamati teule inafanya kazi, bado tunaweza kutoa hukumu dhidi yao?
Tumeshapewa hadidu za rejea.
Kama waliambiwa wahakikishe hela zilizochukuliwa zinarejeshwa, how else would the kamati have gone about it?
kinachogomba hapa ni kwa vile hatujui hao watu walikuwa identified vipi; waliambiwaambiwaje warudishe, na wamarushishaje.
Naamini maswali hayo yatajibiwa pindi ripoti nzima ya kamati ikisomwa.
Na ninaamini itasoma hivi..." ..kamati teule iliagizwa kuhakikisha kuwa fedha zinarejeshwa..kwa kuzingatia agizo hilo, kamati ilipata nyaraka husiak kutoka ndani ya BoT na kupata majina ya watu/kampuni zilizopata fedha hizo haramu na kiasi kilichochukuliwa. kamati iliwaandikia wito wahusika ambapo walifika ofisi ya tume mmoja baada ya mwingine na kupatiwa taarifa kamili ya kuhusika kwao. Kisha tume iliwataka warejeshe fedha hizo kama hatua ya kwanza. wahusika walipewa siku... kufanya marejesho. fedha zilirejeshwa na kuwekwa kwenye account maalum iliyofunguliwa na tume kwa ajili hiyo...
Mapendekezo.
Pamoja na ripoti hii, tume inakabidhi kwa Mh Rais vielelezo vyote na nyaraka zote husika na kupendekeza vitumike kuwachukulia hatua za kisheria wahusika..."
Tume haina mamlaka ya kuwafungulia mashtaka hao jamaa; ila ina mamlaka ndani ya hadidu za rejea kuwataka warejeshe fedha. Kama hilo ni kosa basi wa kulaumiwa ni yule aliyewapa hizo hadidu.
Ila kwa msimamo wa kisheria, kurejesha kwao hizo fedha kni sawa na confession; kesi ikifika mahakamani there is no way watakataa kuhusika
So, by far, tume inaenda vizuri
Lets just give them time guys
go to court! wanaoushahidi wa makampuni yote, wanajua ni kiasi gani kimechotwa, wanajua ni kampuni gani imegushi, wanajua ni nani alikuwa ofisa wa hiyo kampuni, wanajua kampuni iliandikishwa vipi n.k kwanini hawaendi mahakamani?
Hilo ndilo kubwa. Nje ya Mahakama kinachofanyika ni kujitolea. Vinginevyo tufunge Mahakama kama watu wanaweza kufanya majadiliano na wahalifu without court sanction or jurisdiction. Watu wanapovunja sheria hawapelekwi kwenye kamati, wanapelekwa Mahakamani.
Natumaini haitasomeka hivyo.
Hatua gani tena za kisheria? Yaani hatua za kisheria zichukuliwe baada ya adhabu kutolewa? Bado sijaelewa kwanini licha ya ushahidi kuwa uliofanyika ni uhalifu; ripoti ya Ernst and Young siyo tu imeonesha kiasi kilichokombwa lakini pia imeonesha nani amekomba kiasi gani. Kwanini hatuendi Mahakamani?
Ndio maana miezi michache iliyopita kulikuwa na makala inasema "Kwanini Rais hakuamuru hivi?" Kwa sababu siyo kile alichoamuru rais, bali kile asichoamuru ndicho kinanipa ki"dhungudhungu"
Hilo laweza kuwa kweli lakini wanarudisha baada ya tishio la hatua za kisheria (legal threat)?; wanarudisha baada ya kupewa kinga ya kutoshtakiwa (immunity deal)?; wanarudisha kama alama ya kukubali makosa ili yaishe; wanarudisha kama alama ya uzalendo wao?
Kimsingi nje ya kuta za mahakama, kinachoendelea ni mazingaombwe ya daraja la kwanza.
FD yaani unasema mtu akisahihisha alichofanya asiadhibiwe? au mtu anapoadhibiwa mojawapo ya adhabu ni restitution? Kwanini tutangulize restitution before convictions?
go to court! wanaoushahidi wa makampuni yote, wanajua ni kiasi gani kimechotwa, wanajua ni kampuni gani imegushi, wanajua ni nani alikuwa ofisa wa hiyo kampuni, wanajua kampuni iliandikishwa vipi n.k kwanini hawaendi mahakamani?
.
Mwanakijiji,
Ninamaanisha acha warudishe kwanza kisha mambo mengine tutaangalia baadaye. Kwa mtazamo wangu na uzito wa suala lenyewe, wakirudisha na RIBA na kisha biashara zao kutaifishwa ina settle kabisa. Yeah Restitution ni muhimu kabla ya conviction.
Ingawa tunavunja sheria lakini angalia kwa macho mawili huu mfano:
Jamaa wameiba, fedha zipo out of GOVT reach, ukamshitaki na kumfunga miaka 10 nadhani au 30 max. hela billion 130 ukazikosa.
AU
Jamaa wameiba wakasema fedha wamezificha au kuwa na hisa kampuni za nje ambazo hatuna utaratibu wa kubadilishana mali au watu, LAKINI wameamua kuzirudisha na RIBA nzuri tu.
Utaamua lipi kati ya hayo kwa manufaa ya Taifa?