Mporomoko wa vyuo vikuu Tanzania?

Mporomoko wa vyuo vikuu Tanzania?

Izc

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2015
Posts
546
Reaction score
368
Wasalaam wanajukwaa.

Katika orodha ya vyuo bora Africa iliyotolewa mwaka huu 2016 na mtandao wa Times Higher Education (THE), Tanzania haina chuo hata kimoja katika orodha hiyo tofauti na miaka ya nyuma.

Orodha ya Times Higher Education duniani inapima vitu kama
=>mafunzo,
=>utafiti,
=>na mtazamo wa kimataifa.
Kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaotoka nje na wafanyakazi.

Nico Cloete, mkurugenzi wa taasisi ya Higher Education Trust na mratibu wa utafiti wa elimu ya juu na Advocacy Network in Africa, anasema taasisi hizo nne katika orodha ya Afrika - Cape Town, Makerere, Nairobi na Ghana - "zimeidhinisha mipango ya kuwa vyuo vikuu vinavyoongoza kwa utafiti" nchini mwao na vimeshuhudia "ongezeko kubwa kwa wanaofuzu kwa ushahada ya uzamifu na kuunda taasisi za utafiti katika miaka mitano iliopita".

Je, sisi kama Tanzania tunakwama wapi? Na nini kifanyike ili elimu ya vyuo vikuu vyetu ipande katika viwango vya kimataifa?

Top 30 African universities: Times Higher Education reveals snapshot university ranking

Je unavitambua vyuo vikuu bora duniani? - BBC Swahili
 
Tupandishe alama za ufaulu katika masomo yetu.

A ya advanced level subjects ianzie 80 badala ya 75.

Tena ikiwezekana A ianzie 90 kabisa.

Tupandishe viwango vya kwenda chuo kikuu,kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita kutoka E mbili mpaka D mbili,D inayodondokea kati ya 50-59!.

Kwa wale wa diploma to degree tupandishe GPA kutoka 2.7 mpaka 3.5 au ikiwezekana 4.0 kabisa.

Ila tukiona GPA hiyo ni kubwa sana na kiwango cha elimu yetu kimepanda kuliko nchi yoyote duniani isipokuwa wanafunzi wanaofika huko vyuo vikuu ni wachache basi tutaishusha mpaka 3.0 au kadri ya tunavyotaka.

Bila kusahau wahitimu kwa wanafunzi wa hivyo vyuo vikuu wanatakiwa watiwe moyo kushinda kwenye mitandao wakivipigania vyuo vyao walivyosoma kwamba ni bora kuliko vyuo vingine,almaarufu vyuo vya "kata".

Ili la kushindanisha vyuo lina faida mno na litasaidia/linasaidia kukuza elimu yetu.

Walimu pia wasiongezewe mishahara na ikiwezekana ipunguzwe,wakigoma tutawaleta walimu kutoka marekani waje watufundishe.
Ni hayo.
 
Tubane matumizi, tuimarishe viwanda, walimu wasipandishwe madaraja, hii itasaidia kuipa elimu heshima
 
Tutoe elimu bure,tuongeze madawati,walimu wasiajiriwe tena aswa wa arts coz wanafunz wameshaelewa vya kutosha,tusiongeze mishahara kwa walimu,tununue ndege za kutosha itasaidia kuipaisha elimi yetu hadi nje ya mipaka ya tz
 
Wasalaam wanajukwaa.

Katika orodha ya vyuo bora Africa iliyotolewa mwaka huu 2016 na mtandao wa Times Higher Education (THE), Tanzania haina chuo hata kimoja katika orodha hiyo tofauti na miaka ya nyuma.

Orodha ya Times Higher Education duniani inapima vitu kama
=>mafunzo,
=>utafiti,
=>na mtazamo wa kimataifa.
Kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaotoka nje na wafanyakazi.

Nico Cloete, mkurugenzi wa taasisi ya Higher Education Trust na mratibu wa utafiti wa elimu ya juu na Advocacy Network in Africa, anasema taasisi hizo nne katika orodha ya Afrika - Cape Town, Makerere, Nairobi na Ghana - "zimeidhinisha mipango ya kuwa vyuo vikuu vinavyoongoza kwa utafiti" nchini mwao na vimeshuhudia "ongezeko kubwa kwa wanaofuzu kwa ushahada ya uzamifu na kuunda taasisi za utafiti katika miaka mitano iliopita".

Je, sisi kama Tanzania tunakwama wapi? Na nini kifanyike ili elimu ya vyuo vikuu vyetu ipande katika viwango vya kimataifa?

Top 30 African universities: Times Higher Education reveals snapshot university ranking

Je unavitambua vyuo vikuu bora duniani? - BBC Swahili
Tatzo siasa hadi kwenye elimu we huge sema umepunguza GPA toka 3.5_3.0 ambapo bado ni upper second MI naona vyema changes ziwepo ktk nyanja ya utawala tuwape na wengne tuone
 
Waende zao kwani sisi tumefanya utafiti nchini kwao kujua ukweli?
Kwa upande mwingine Watz tuweke mkakati wa kuendeleza vipaji vya wabunifu, COSTEC mpo?
 
Kupata rank kubwa vigezo hasa huwa RESERCH AND PUBLICATIONS, INTERNATIONAL STUDENTS na Kiwango cha elimu yaani graduates wa hapo akili zao wakienda field.

Sasa sisi research majanga, wanafunzi wa nje wanakuja wachache kwasababu nafasi yetu hatupo hata top 30, nani aje?
Wanafunzi wakigraduate hawatoki nje ya nchi kufanya kazi, na wakienda kiwango chao cha ufanisi ni kidogo.
What do you expect
 
Tupandishe alama za ufaulu katika masomo yetu.

A ya advanced level subjects ianzie 80 badala ya 75.

Tena ikiwezekana A ianzie 90 kabisa.

Tupandishe viwango vya kwenda chuo kikuu,kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita kutoka E mbili mpaka D mbili,D inayodondokea kati ya 50-59!.

Kwa wale wa diploma to degree tupandishe GPA kutoka 2.7 mpaka 3.5 au ikiwezekana 4.0 kabisa.

Ila tukiona GPA hiyo ni kubwa sana na kiwango cha elimu yetu kimepanda kuliko nchi yoyote duniani isipokuwa wanafunzi wanaofika huko vyuo vikuu ni wachache basi tutaishusha mpaka 3.0 au kadri ya tunavyotaka.

Bila kusahau wahitimu kwa wanafunzi wa hivyo vyuo vikuu wanatakiwa watiwe moyo kushinda kwenye mitandao wakivipigania vyuo vyao walivyosoma kwamba ni bora kuliko vyuo vingine,almaarufu vyuo vya "kata".

Ili la kushindanisha vyuo lina faida mno na litasaidia/linasaidia kukuza elimu yetu.

Walimu pia wasiongezewe mishahara na ikiwezekana ipunguzwe,wakigoma tutawaleta walimu kutoka marekani waje watufundishe.
Ni hayo.
Mkuu hydroxo,
Hapa tatizo si ufaulu, tatizo linaloonekana ni vyuo vyetu havifanyi tafiti za kutosha au kama vinafanya basi impact ya tafiti yake ni ndogo katika mazingira yetu au hazina impact kabisa.
Tatizo lingine ni mafunzo

Lakini pia mtazamo wa chuo kimataifa mf idadi ya wanafunzi wa wafanyakazi kutoka nje wanaosoma na kuhudumu katika vyuo.
 
digrii za chupi, undugunization na pesa ndo zimetufikisha hapa..elimu ya tz inapumulia mashine..niombeeni sina mil 7.
 
Elimu ya Tanzania inahitaji mtazamo mpana kuikoa na si huko kuhangaika na madaraja na viwango vya udahili. Kitakachoendelea kuimaliza kabisa hii elimu yetu ni haya maamuzi ya mtu mmoja kadri anavyoona yeye inafaa. Haiwezekani mtu uamini 100% akili yako kuwa unachofikiri wewe ni sahihi 100% kwa sababu wewe ni PhD holder au Professor.
 
Tupandishe alama za ufaulu katika masomo yetu.

A ya advanced level subjects ianzie 80 badala ya 75.

Tena ikiwezekana A ianzie 90 kabisa.

Tupandishe viwango vya kwenda chuo kikuu,kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita kutoka E mbili mpaka D mbili,D inayodondokea kati ya 50-59!.

Kwa wale wa diploma to degree tupandishe GPA kutoka 2.7 mpaka 3.5 au ikiwezekana 4.0 kabisa.

Ila tukiona GPA hiyo ni kubwa sana na kiwango cha elimu yetu kimepanda kuliko nchi yoyote duniani isipokuwa wanafunzi wanaofika huko vyuo vikuu ni wachache basi tutaishusha mpaka 3.0 au kadri ya tunavyotaka.

Bila kusahau wahitimu kwa wanafunzi wa hivyo vyuo vikuu wanatakiwa watiwe moyo kushinda kwenye mitandao wakivipigania vyuo vyao walivyosoma kwamba ni bora kuliko vyuo vingine,almaarufu vyuo vya "kata".

Ili la kushindanisha vyuo lina faida mno na litasaidia/linasaidia kukuza elimu yetu.

Walimu pia wasiongezewe mishahara na ikiwezekana ipunguzwe,wakigoma tutawaleta walimu kutoka marekani waje watufundishe.
Ni hayo.
Haaa kwan xaiz A ya advance inaanzia ngapi na viwango vya kuingia chuo ni ngapi kama sio D mbili? Nahic kama ujafanya uchunguzi vile au sijakuelewa



NB:ni mtazamo tuu
 
Tupandishe alama za ufaulu katika masomo yetu.

A ya advanced level subjects ianzie 80 badala ya 75.

Tena ikiwezekana A ianzie 90 kabisa.

Tupandishe viwango vya kwenda chuo kikuu,kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita kutoka E mbili mpaka D mbili,D inayodondokea kati ya 50-59!.

Kwa wale wa diploma to degree tupandishe GPA kutoka 2.7 mpaka 3.5 au ikiwezekana 4.0 kabisa.

Ila tukiona GPA hiyo ni kubwa sana na kiwango cha elimu yetu kimepanda kuliko nchi yoyote duniani isipokuwa wanafunzi wanaofika huko vyuo vikuu ni wachache basi tutaishusha mpaka 3.0 au kadri ya tunavyotaka.

Bila kusahau wahitimu kwa wanafunzi wa hivyo vyuo vikuu wanatakiwa watiwe moyo kushinda kwenye mitandao wakivipigania vyuo vyao walivyosoma kwamba ni bora kuliko vyuo vingine,almaarufu vyuo vya "kata".

Ili la kushindanisha vyuo lina faida mno na litasaidia/linasaidia kukuza elimu yetu.

Walimu pia wasiongezewe mishahara na ikiwezekana ipunguzwe,wakigoma tutawaleta walimu kutoka marekani waje watufundishe.
Ni hayo.
Nani kakudanganya kwamba chuo kufanya vzur kwenye rank za dunia wanaangalia grade za mitihani ya form6 au 4.
Unachekesha sana kijana.
Uoni hubert kairuki kinachukua watu wenye division 3 wengii lakini mwsho w siku kairuki ni the best kuliko vyuo vngne vya private ukiachia Muhas.
Pale mdogo wangu nakukumbusha awaangalii grade.
HUANGALIWA VIFUATAVYO.

1.Wanafunzi wenu wanakidhi ubora katika sekta usika ndani na nje ya Nchi. (Competent Doctors and Engineers)

2.Research mnazo fanyaa je wanafunzi wenu waliopo chuoni au waliohitimu wamefanya nini kipya.
Mfano SUA waligundua panya wakutegulia mabomu.

3.Ubora wa ma Drs na Maprofesars katika chuo husika.
NB chuo kufanya vzur aidepends na
Kuwa na wanafunzi wenye ufaulu mkubwa.
 
Hatutafika mbali na hizi approaches zetu za elimu ya kujua kuandika na kusoma tu. Elimu ni zaidi ya hapo.....moja wapo ni kitu kinaitwa employability nayo ni determinant wa ubora wa elimu ya mtu au taasisi.
 
Waende zao kwani sisi tumefanya utafiti nchini kwao kujua ukweli?
Kwa upande mwingine Watz tuweke mkakati wa kuendeleza vipaji vya wabunifu, COSTEC mpo?
wewe jamaaa nimekukubali mbona si mbona hatuendi kufanya utafit kwao... kwa vigezo vyao ni sawa ila kumbuka kila kitu chamsing watanzania tuliokua wengi hatujui kujihoji kabla ya kupokea takwimu tulizopewa... kwanini imekua hvyo? kwann ubora we elimu umeporomoka? je elimu inayotolewa katika ngazi tofaut tofaut inakidhi maitaji ya wanafunz katika kipindi husika? elimu itolewayo ina changamoto gani ili kufikia malengo tuliyo jiwekea? so ukinaliza yote haya utakua na wigo mpana wa kuweza kutafsiri takwimu zote zitolewazo na taasisi mbalimbali [emoji6] [emoji6] [emoji6]
 
Nani kakudanganya kwamba chuo kufanya vzur kwenye rank za dunia wanaangalia grade za mitihani ya form6 au 4.
Unachekesha sana kijana.
Uoni hubert kairuki kinachukua watu wenye division 3 wengii lakini mwsho w siku kairuki ni the best kuliko vyuo vngne vya private ukiachia Muhas.
Pale mdogo wangu nakukumbusha awaangalii grade.
HUANGALIWA VIFUATAVYO.

1.Wanafunzi wenu wanakidhi ubora katika sekta usika ndani na nje ya Nchi. (Competent Doctors and Engineers)

2.Research mnazo fanyaa je wanafunzi wenu waliopo chuoni au waliohitimu wamefanya nini kipya.
Mfano SUA waligundua panya wakutegulia mabomu.

3.Ubora wa ma Drs na Maprofesars katika chuo husika.
NB chuo kufanya vzur aidepends na
Kuwa na wanafunzi wenye ufaulu mkubwa.
Rudia kusoma tena nilichokiandika.

Usisome vitu nusunusu.
 
Nafikiri tuna tatizo kubwa sana hasa katika kutofautisha siasa na taaluma. Taaluma yetu imeingiziwa siasa. Wanafunzi wanapambana vyuoni lakini hawapati msaada wa nyenzo za kisasa tunabaki kusema hawana akili.

Tafiti nyingine za kisiasa zinaingizwa kwenye taaluma. Mfano ile tafiti iliyoletwa na kusema 65% ya wahitimu vyuo vikuu Tanzania ni vilazer italigharimu taifa miongo na miongo.

Kuhusu alama za ufaulu ili kujiunga vyuo vikuu vyetu sio kweli kwamba ziko chini. Alama hizo hizo huenda nazo baadhi ya watu nchi za nje na wa kurudi wako competent kuliko wale waliopata alama za juu na kusoma hapa Tanzania.

Ushauri
Serikali iboreshe mazingira ya wanachuo ya kusoma ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu bora na ya kisasa pia kuhakikisha wahadhiri wanaofundisha wamefikia viwango.
Mwisho siasa isiingizwe kwenye taaluma, tafiti za elimu zifanyiwe kazi sio kuwekwa mabango.
 
Iseee ina maana kile chuo kongwe hapa nchini a.k.a chuo cha vipanga hakipo kwenye list ya vyuo 30 bora africa??? duuuuuh shida nini tena????????????????
 
Back
Top Bottom