Mponda agoma kujiuzulu

Mponda agoma kujiuzulu

Ajiuzuru waziri wa tanzania kwa hiari, thubutu! Aliweza Mwalimu tu. Hawa wengine NO. Wote hadi walazimishwe, angalia Seifu Sharif, Mwinyi, E. Lowasa, Mbilinyi, Mpologonyi, About Jumbe, aah wengine siwakumbuki bana.
 
Kukimbilia kujiuzulu siyo suluhu sana ya tatizo. Kwasababu kama ni hivyo, watu wanaweza kuharibu mambo kwa maksudi wakitegemea watajiuzulu na kukaa pembeni."

Alieleza kwamba hadi jana jioni, hakuwa na uamuzi wowote kuhusu hilo na alikuwa akiendelea na majukumu yake kama kawaida huku akisisitiza;

"Unajua mtu anaweza kufikiria zaidi kujiuzulu kama atakuwa amefanya au amesababisha kitu na yeye mwenyewe nafsi yake ikathibitisha hilo. "

Alisema binafsi, ameguswa na mgomo huo wa madaktari ambao umeathiri huduma za afya nchini, huku baadhi ya watu wakipata madhara zaidi ya maradhi.

Lakini, alipoulizwa kwamba kutokana na hali hiyo, haoni kwamba alipaswa kuwajibika kwa kujiuzulu kama sehemu ya kuumizwa na madhara yaliyowapata Watanzania kutokana na Wizara yake alijibu; "Naomba ni reserve(nihifadhi) kauli yangu katika hilo. Lakini, nani wanataka nijiuzulu, ni wewe (mwandishi) au nani? Maana sijasikia hilo unalosema. Nikisikia nitaamua."

Alifafanua kwamba kuwajibika wakati mwingine baadhi ya watu wamekuwa wakitafsiri dhana hiyo tofauti .

"Kwa mfano, mimi nimeguswa sana na mgomo wa madaktari, nawapenda sana Watanzania, sasa hapo kuna tofauti kidogo."

Dk Mponda alisema ndiyo maana alikuwa akifanya jitihada zote kuhakikisha anakutana na madaktari hao kuhakikisha mgomo huo unamalizika, lakini bahati mbaya juhudi hizo hazikufanikiwa haraka.

"Kwakweli nimeguswa sana na mgomo huo wa madaktari, ndiyo maana nimekuwa nikifanya kila jitihada kuhakikisha unamalizika, lakini bahati mbaya hilo halikutokea. Kwa hiyo, nimeumia sana," alisisitiza Dk Mponda, baada ya kuulizwa tena kwamba kama ameguswa ni kwanini asiwabijike kwa kujiuzulu hata kama hakutenda kosa.

Alisema anatambua umuhimu na dhana ya uwajibikaji, lakini akasisitiza kuwa "Siwezi kusema zaidi kwa sasa. Wakati ukifika nitaweza kuzungumza."

MUNGU akusamee maana hujui utendalo
 
The number ure calling is not reachable pse try again later
 
Waziri hajaguswa na lolote. Huo mgomo unaonesha kuwa wizara haiwezi. Aache ili afanye shughuli zingine zilizo ndani ya uwezo wake.

Quality
 
Madaktari wameeleza waziwazi hawana imani naye huyu Waziri. Sasa atafanyaje kazi na watu ambao hamkubali na wala hawana imani naye?
 
uwapendi watanzania acha unafiki wako, unajipenda wewe na posho unazopokea ungekuwa unawapenda watanzania ungekuwa umeshajiuzuru kuokoa maisha ya watanzania badala ya kuendelea kungangania madaraka.
 
Sisi wajuvi tunajua kuwa hatuna Waziri wa Afya.......there is only an impostor put in by an impostor of a president

wedau 2015 mnaitajika kumpatia rais ajae washauri wazuri na wenye misimamo, akinamponda na wengine wanatoka katika jamii yetu na tumewachagua sisi, je hatukujua kuwa si watu wasio jua wajibu wao na wakishindwa wanastili kuwajibika!!!!! tunapasika tuanze kujilaumu sisi then tuweze kuwawajibisha wanaodhani wanatutawala badala ya kutuongoza. Katiba inakuja mtaani tutumie fursa hii kuweka vitu vya msingi, ikiwa ni pamoja na si lazima mbunge akae miaka mitano kama hana kitu kipya cha kuiletea taifa hili maisha bora kama "slogan" ya watala isiyotekelezeka.

MPONDA HAONI SABABU KWANI HUSEEN MWINYI HAKUONA SABABU IWEJE YEYE AWE MBUZI WA KAFARA........., NI NGUMU KWA KIPINDI HIKI KWANI WATAWALA WETU WANAONA BILA WAO NCHI HII HAIWEZI KWENDA.

TUCHUKUE HATUA KUBADILI MFUMO NA TUSIPIGANE NA MTU MMOJA MMOJA, NI MFUMO MZIMA UMEHARIBIKA.
 
Back
Top Bottom