Mpira umeisha kwa Amani wanaodai Haki haikutendeka wanataka kuvuruga michuano ya AFCON.

Mpira umeisha kwa Amani wanaodai Haki haikutendeka wanataka kuvuruga michuano ya AFCON.

Ndugu mtanzania kutuma picha au video zozote zinazohusu mechi ya Morocco na Tanzania hasa pale kwenye kudai penalty ni uvunjaji wa taratibu za kisheria. Ni kosa kubwa mno kutishia amani
1767551112794.jpg
 
Watanzania hatujui kipaumbele chetu ni nini, Amani kwanza au Haki kwanza.

Baada ya mechi kwisha na Tanzania kutolewa kwa (0-1) na Morocco, wachezaji na benchi lote la ufundi walisimama wakimlalamikia refa kuwa hakutenda Haki, vile vile kuna Watanzania wanasema refa hakutenda haki kawanyima Stars penalty ya wazi.

Mimi nasema tumshukuru Mungu mpira umeisha kwa Amani kabisa, turudi nyumbani tujipange upya, wanaodai Haki wanataka kuvuruga Amani ya michezo ya AFCON.

Tunamuomba kiongozi wa msafara Paul Makonda awafikishie viongozi wenzake jinsi inavyouma pindi unaponyimwa haki yako.
Kama hao unaowatumia ujumbe wana werevu wa kuelewa somo!
 
Boniface Mwabukusi.

TWISEHENI YA HAKI NA AMANI.

Hapa Mungu ametupitisha sote katika kujifunza Umuhimu wa Haki katika jamii.Taifa stars wamenyimwa Haki ili kulinda Amani na Utulivu wa Wamoroco.

Nimefurahi somo hili gumu lakini limekuja kwa wakati sahihi . Nimeona hata wale wanao himiza Amani katika hili wanadai refa alitakiwa kwenda kwenye VAR ili haki ionekane imetendeka.

HAKI ndiyo Msingi wa Amani.
 
Back
Top Bottom