Mpinzani wa Mbowe ajitoa

Mpinzani wa Mbowe ajitoa

IKWETE

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
4,057
Reaction score
696





Hamkani hali si shwari ndani ya Chadema! Kansa Mohamed Mbaruku, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Tabora, amejitoa kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa, hivyo kumfanya kwa mara nyingine Freeman Mbowe kuwa katika mashindano ya 'farasi' mmoja.


Kwa mujibu wa 'Mwananchi Breaking News', Mbaruku ameamua kujitoa kwa madai kwamba katiba ya chama hicho imekiukwa na akasema atakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uchaguzi huo na kuomba ufafanuzi wa kikomo cha uongozi.


Mbaruku amejitoa siku moja tu kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake, ambao umepangwa kufanyika kesho Jumapili Septemba 14.


Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba kujitoa kwa mgombea huyo kunaweza kusababisha mpasuko ndani ya Chadema kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya uongozi kwamba unaendesha chama kama 'taasisi

binafsi'.


Awali Mbaruku aliwasilisha pingamizi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, ambapo pamoja na mambo mengine, alidai kwamba Mbowe hana sifa kikatiba ya kugombea tena nafasi hiyo.


Pia duru za siasa ndani ya chama hicho zilieleza kwamba, majina mawili yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda katika chama hicho, Benson Kigaila, kwamba nao walijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti, Daniel Ruvanga na Garambenela Frank, yalikuwa majina hewa yaliyolenga kumsafishia njia Mbowe ya kubakia kuwa mgombea pekee baada ya kuenguliwa kwa Mbarouk.


Inaelezwa kwamba, Katiba ya Chadema hairuhusu kiongozi wa nafasi hiyo kugombea vipindi zaidi ya viwili vya miaka mitano.
 
Hivi kweli mtuw kama huyu alizaliwa na wazazi binadamu kama wengine au mwenzetu alizaliwa na bata?? Mbona hana mshipa wa haya huyu...Hivi kweli anamke,mtoto,ndugu au majirani wa kawaida huyu? Sidhani kama ni binadamu wa kawaida sidhani....anatakiwa kupimwa si bule huenda zimeruka/hazijatimia.....

BACK TANGANYIKA
 
Huyu kansa hata mbunge mmoja hana tabora,halafu ndio awe mwenyekiti taifa ni kituko
 
Amejua tu kuwa ataambulia 0 kwa kuzingatia kuwa yeye si mjumbe angekosa hata kura moja. Hiyo no geresha ya kutafuta ujiko kabla ya kuhamia ACT kwa gia ya aliekuwa mgombea wa CHADEMA Taifa.
 
Amekimbia aibu ya kushindwa hana lolote

Mwanaume mzima anakubali kushindwa kirahisi namna hii!! Kama kweli yeye kidume angesubiri hadi sekunde ya mwisho si kukimbia. Si alishapeleka pingamizi sasa kisa cha kujitoa ni nini? Shame
 
Taarifa za kiintelligencia zinasema Zitto yuko nyuma ya huyu mhuni....
 
Last edited by a moderator:







Hamkani hali si shwari ndani ya Chadema! Kansa Mohamed Mbaruku, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Tabora, amejitoa

kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa, hivyo kumfanya kwa mara nyingine Freeman Mbowe kuwa katika mashindano ya

'farasi' mmoja.


Kwa mujibu wa 'Mwananchi Breaking News', Mbaruku ameamua kujitoa kwa madai kwamba katiba ya chama hicho imekiukwa na

akasema atakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uchaguzi huo na kuomba ufafanuzi wa kikomo cha uongozi.


Mbaruku amejitoa siku moja tu baada kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake, ambao umepangwa kufanyika kesho Jumapili

Septemba 14.


Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba kujitoa kwa mgombea huyo kunaweza kusababisha mpasuko ndani ya

Chadema kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya uongozi kwamba unaendesha chama kama 'taasisi

binafsi'.


Awali Mbaruku aliwasilisha pingamizi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, ambapo pamoja na mambo mengine, alidai

kwamba Mbowe hana sifa kikatiba ya kugombea tena nafasi hiyo.


Pia duru za siasa ndani ya chama hicho zilieleza kwamba, majina mawili yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na

Usimamizi wa Kanda katika chama hicho, Benson Kigaila, kwamba nao walijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti, Daniel Ruvanga na

Garambenela Frank, yalikuwa majina hewa yaliyolenga kumsafishia njia Mbowe ya kubakia kuwa mgombea pekee baada ya kuenguliwa

kwa Mbarouk.


Inaelezwa kwamba, Katiba ya Chadema hairuhusu kiongozi wa nafasi hiyo kugombea vipindi zaidi ya viwili vya miaka mitano.

Taarifa hii ilikuwa nzuri kama taarifa,umeharibu ulipoonesha ushabiki uliposema"duru za kisiasa zinasema kujitoa kwa mbaruku kutaleta mpasuko ndani ya chadema"hapa umeweka chumvi zako labda kwakuumia kuona kapteni Mbowe anapita bila kupingwa kwakuwa anakubalika na kila mtanzania na kuwa uwezekano wa kuiua chadema ndiyo unazikwa rasmi.Unajua kabisa hakuna mpasuko wowote kwani huyo kansa hana influence yoyote katika chama na katika jamii,anachofanya ni kuigiza ili waliomtuma waone kuwa hela zao walizompa zinafanya kazi.
Nakushauri uwe unaongea ukweli acha uongo.
Chadema oyeeeeeeeeeee!!!!!!
 
Aache wendawazimu , yeye amekuwa mwenyekiti wa mkoa wa tabora kwa vipindi vitatu mfululizo kwa kutumia katiba hiyohiyo halafu leo anataka itumike kwa mbowe, what a shame.

Hajitambui huyo bora amejiengua kwani kesho ilikua tumwazibu kwa kura vyakutosha.
 
Halafu atajitangaza kujiunga na nyumba ndogo wa CCM
 
mwendawazimu mkubwa huyu

Tungehakikisha anapata kura 0
 
Taarifa hii ilikuwa nzuri kama taarifa,umeharibu ulipoonesha ushabiki uliposema"duru za kisiasa zinasema kujitoa kwa mbaruku kutaleta mpasuko ndani ya chadema"hapa umeweka chumvi zako labda kwakuumia kuona kapteni Mbowe anapita bila kupingwa kwakuwa anakubalika na kila mtanzania na kuwa uwezekano wa kuiua chadema ndiyo unazikwa rasmi.Unajua kabisa hakuna mpasuko wowote kwani huyo kansa hana influence yoyote katika chama na katika jamii,anachofanya ni kuigiza ili waliomtuma waone kuwa hela zao walizompa zinafanya kazi.
Nakushauri uwe unaongea ukweli acha uongo.
Chadema oyeeeeeeeeeee!!!!!!

Mkuu nimekopi na kupesti tu
 
Huyo ndie Kansa, bingwa wa propaganda zilizoshindwa. Kagombee act ndio kunafanana na watu wa aina yako. Naona hata magamba awawezi kupokea watu wa aina yako. Pole kwa kununuliwa kwa bei ya mandazi mh. Kansa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom