Mpinzani Mpya wa Mwigulu apatikana

Status
Not open for further replies.
Kwa mazingira ya Iramba haiwezekani kwa mtu hadi kufikia kiwango hicho cha elimu asijulikane mtaani hata wilayani.
 
Ni Mwanasheria machachari George Kidindima ametangaza nia ya kugombea Ubunge ktk Jimbo la iramba magharibi 2015 kupitia CHADEMA
-Kidindima amepata kuwa Mhadhiri msaidizi ktk Chuo ya uhasibu Singida campus pia ni mwandishi wa vitabu kadhaa vya business law,

Source;Mwigulu nchemba vs Kitila mkumbo(fb group)

Binti Kishoa vp tena? Mtabadilisha sana, kweli Mwigulu noma.
 
Hiki chama sasa kimekuwa kama jamvi la wageni. Mtu anajiunga leo kesho anatangaza kugombea ubunge. Afande sele, pro jay huyu naye. Huko iramba kaz ngum, Kitila, Kishoa, Huyu naye huyoooo
 
Kila mtu anayeamua kufanya jambo anajiamini kuwa anao uwezo kwani huyo mbunge wa sasa anauwezo gani kama sio chama kilimbeba na sent zileee! Za kapu la bibi? Acheni ushabiki wa kinaa huyo jamaa aende akishindwa anajipanga awamu nyingine atapita tu he is stil young man.
 
kila mtu anayeamua kufanya jambo anajiamini kuwa anao uwezo kwani huyo mbunge wa sasa anauwezo gani kama sio chama kilimbeba na sent zileee! Za kapu la bibi? Acheni ushabiki wa kinaa huyo jamaa aende akishindwa anajipanga awamu nyingine atapita tu he is stil young man.
songela ....lengo ni kumtoa nyang'au mwigulu
 
Ndugu zangu, mapema leo asubuhi mmeona post ya BAVICHA-IRAMBA ikisema kuwa nimetangaza rasmi kugombea UBUNGE katika jimbo la Iramba-Magharibi. Hilo haliwezi kuwa tangazo langu rasmi kwa sababu zifuatazo:-
1. Mgombea wa nafasi kubwa na nyeti kama hiyo hawezi kusemewa na yeyote ila yeye binafsi. Hivyo basi kama nia hiyo ninayo nitatangaza rasmi mimi mwenyewe muda wakufanya hivyo ukimea (ukiwadia).
2. Jumuiya ya chama (kama ilivyo Bavicha) sio haki kumuunga mkono mwanachama yeyote ambaye hata hajaidhinishwa na chama kugombea nafasi husika. Hii inaleta picha mbaya kwa yeyote mwingine mwenye nia yakugombea nafasi husika.
3. Muda wakutangaza kugombea haujafika hivyo kufanya hayo ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama pamoja na kanuni zake. Napenda ieleweke kuwa mimi kama Mwanasheria na mdau wa siasa kwa muda mrefu naielewa Sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini, na katiba ya CHADEMA naielewa KINDAKINDAKI (“in and out”), hivyo siwezi kuikiuka kwa namna iwayo yote.
Aidha nimesikitishwa sana na Baraza hilo la vijana la CHADEMA kwakunilisha maneno na kusema uongo kuwa nilitoa matamshi hayo pale Katala Beach Hotel, jambo hili sio la kweli. Kwa ufafanuzi tu kuhusu hili ni kwamba miezi takribani miwili kasoro iliyopita nilialikwa hotelini hapo kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya “SIO KOSA LANGU” iliyoigizwa na wanafunzi wa chuo cha uhasibu (T.I.A-Singida Campus). Pale sikuongelea suala lolote la kisiasa kama nilivyoripotiwa na BAVICHA-IRAMBA zaidi yakutoa mchango wangu na kushiriki mnada wa DVD hizo.
Nawaombeni radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, hasa wale wenzangu wenye nia ya kugombea nafasi hiyo adhimu, nawaambia msizimie moyo mapambano yangali bado. Aidha nawashukuru nyote mliofurahishwa na tangazo hilo na kunitia moyo kuwa naweza, napenda muelewe kuwa hili ni suala la muda tu, ukifika na nia ikingali basi nitawaombeni ushirikiano. Asanteni sana.
George Kidindima,
04/02/2014.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom