Mpina: Mawaziri wapatikane kwa njia ya Ushindani siyo Uteuzi ili tupate Mawaziri Bora badala ya Bora Mawaziri!

Yaani waziri akaombe kazi kwa afisa utumishi au?, Sasa uwaziri si utakua wa kununua sasa?, Na hao mawaziri watawajibika kwa nani?
 
Mawaziri waendelee kuteuliwa na Rais, wathibitishwe na Bunge
Yale yale tu, usipomuamini Rais aliechaguliwa kwa kura, hakuna mtu mwingine utaamini,, wabunge wanaounda serikali hawawezi kukataa kupitisha teuzi za Rais,, hata wakikataa, Rais atateua mwingine wampitishe,,
Tukisema watume maombi na iundwe timu ya kuwachagua, sana sana wajumbe wa timu watatajirika sana,, 😂.
Na mawaziri hawatawajibika kwa rais, maana yake hata wakiharibu, Rais hatakua na lawama, na kiufupi urais hautakua urais ,, hata tukisema maombi ya uwaziri yatumwe UN, na umoja wamataifa ndo uteue,, swali liko palepale,, mawaziri watakua answerable kwa nani? 😁🤷🏼‍♂️
 
Back
Top Bottom