"Wakati Serikali ikijitetea kuifanya TPDC kuwa muagizaji pekee wa mafuta kwa kigezo cha kwamba itapunguza bei ya mafuta nchini, viwango vya faida (premium) vilivyowekwa na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa miezi ya Mei na Juni baada ya mfumo wa ushindani kufutwa, viko juu zaidi.
Kwa dizeli, tozo iliyotangazwa (premium) ilipanda kutoka
Dola 98.5 kwa mita za ujazo (takriban
TZS 251 kwa lita) hadi
Dola 267 kwa mita za ujazo (takriban
TZS 681 kwa lita), ikiwa ni ongezeko la
81.5%.
Kwa petroli, tozo ilipanda kutoka
Dola 157 kwa mita za ujazo (takriban
TZS 400 kwa lita) hadi
Dola 285 kwa mita za ujazo (takriban
TZS 727 kwa lita), ikiwa ni ongezeko la
81.5%."
"Inasikitisha sana kuona kuwa kampuni ya Vitol inauza mafuta kwenye masoko ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupitia Bandari ya Beira kwa bei ya chini zaidi ikilinganishwa na inavyouza hapa Tanzania. Katika baadhi ya shehena, tofauti ya bei imezidi
Dola 300 kwa mita za ujazo (sawa na zaidi ya
TZS 765 kwa lita) ukilinganisha na bei ya mafuta yaliyoingizwa Tanzania."
"Ukweli kwamba Vitol imepewa kiwango cha juu sana cha
premium kuliko kinachotozwa katika nchi jirani—na juu zaidi ya kile walichokuwa wakitoza awali—inamaanisha kuwa kampuni hii imeipora umma na taifa letu zaidi ya
TZS bilioni 501.67."
"Hivyo basi, kwa kipindi cha miezi mitatu ya Aprili, Mei, na Juni 2026, inakadiriwa kuwa taifa letu limepata hasara inayofikia jumla ya
TZS trilioni 2.16, ikijumuisha:
- TZS trilioni 1.5 kutokana na upandishaji holela wa bei za mafuta.
- TZS bilioni 501.67 ya malipo ya ziada kwa kampuni ya Vitol.
- TZS bilioni 161.98 za tuhuma za malipo ya kifisadi ya ruzuku katika sakata hili la uagizaji mafuta.
Kiasi hiki ni kikubwa sana ukilinganisha na TZS bilioni 700 tulizokuwa tumekadiria hapo awali."
— Luhaga MpinaNaibu Waziri Mkuu Kivuli, ACT Wazalendo