Mpesa ya vodacom kuna nini?

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,976
2,755
Nilienda mjini tarehe 27/02/2012 kuweka pesa yangu kwa wakala wa MPESA mjini. Wakala akapokea pesa na kuiweka akaniambia nisubiri msg ya kuwekea pesa toka MPESA kama kawaida. nilisubiri weee bila kupata ujumbe pamoja na juhudi nyingi kufanywa na wakala. mwisho niliamua kuondoka nikiacha id zangu na contact. Hadi leo sijapata huo ujumbe. nilirudi kwa wakala jana akanieleza nisubiri na hawezi kunirudishia pesa yangu kwa sababu tayari walishatuma MPESA. Wanasema eti MPESA kuna tatizo la network. Nimewapigia MPESA HQS simu yao ni unreachable. Je kuna mtu amepata Uzoefu huu wanajamii?
 
hio huwa inatokea. Unachotakiwa kufanya ni kuwapigia Vodacom customer care uwaambie issue yako. Watakuuliza uliponunulia hivyo uwe na namba ya huyo agent na namba yako halafu watapush hio message tena.
 
asante Tofty nitafanya hivyo because nilishachanganyikiwa. nikaona mhh hii kali.
 
Hata hao mawakala huwa nowadays wamekuwa vigeugeu wanakupiga changa la macho hivihivii
 
Hii ilitokana na faiba kule mombasa kukatwa na meli iliyokuwa inatia nanga,lakini mpaka jana saa tisa M PESA ilkuwa ipo poa unachotakiwa kufanya ni kufika kwa wakala au kupiga voda 15366 kila kitu utapata

You will never loss your cash
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom