Namshukuru Mungu aliyekufunulia kunena haya! Ubarikkiwe sana!!mpendwa, sijui kama wewe ni muumini wa dhehebu gani, lakini mie nina ushauri hapa......................
1.
yeye kaomba umchangie-kama una uwezo wa kuchanga, mchangie kwa msingi wa ombi lake na kulingana na uwezo wako, usije ukalaza watu wa nyumbani mwako na njaa kwa sababu ya kuchangia harusi hii, kumbuka kila aombaye hupokea, je tukiwasaidia wale tu walio wapenzi wetu, tutapata ama kustahili thawabu gani ya ziada? mafarisayo na wenye dhambi na watu wa mataifa nao hawafanyi hivyohivyo? hakika haki yetu lazima ipite haki ya mafarisayo, watoza ushuru na wenye dhambi, vinginevyo hatuwezi kuurithi ufalme wa Mungu.
2.
ushinde ubaya kwa wema-kwa kuwa unakiri kuwa hukumkosea, lakini bado Mungu anampa fursa na ujasiri wa kukutafuta na kuomba umuunge mkono au umsaidie, kumbuka unapaswa kuushinda ubaya kwa wema. kwa wema wako atatambua kosa lake la kumkataa mke mwema na pamoja na kuwa huna tena nafasi kwake, lakini atayasimulia matendo yako makuu siku zote za maisha yake na kufanyika baraka mlangoni mwako maisha yake yote na hivyo Mungu kutukuzwa kupitia maisha yako.
3.
kushiriki ama kutoshiriki harusi nashauri usikilize dhamiri yako inataka nini. mimi ningeshauri ushiriki kama na nafasi na usiwe kwazo katika shughuli yao ile kwa namna yoyote bali ufanyike baraka. si mbele yake bali mbele za Baba yetu aliye mbinguni. atakapoziona baraka kupitia kwako, atamshukuru Mungu na kumuinua siku zote za maisha yake na ataamini kuwa kweli wewe ni mtoto wa Mungu kwani unakata mashauri kwa jinsi ya Mungu na si kwa jinsi za wanadamu. kumbuka tena mpendwa kuwa haki yako mbele za Mungu lazima ipite haki ya afarisayo na wenye dhambi ili kustahili thawabu
thamani ya ushauri huu itategemea imani yako na kiwango cha uchaji wa Mungu ulichonacho.............ni hayo tu mpendwa........................... unarikiwe na Bwana
Lakini kwa nini mtu utake kwenda kwenye harusi ya ex wako? Mimi kama naoa sitafurahia hata kidogo kuwaona ma ex wa mke wangu mtarajiwa. Mambo gani haya...yaani unaiona njemba iliyokuwa inamega mke wako mtarajiwa? Mambo mengine ni hapana kabisa aisee. Kama mtu mmeshaachana basi ni bora kuendelea na maisha yenu kivyenu vyenu. Mambo ya kuendeleza ties na ma ex ni chanzo cha mizozo ktk ndoa au uhusiano wenu. Hayafai.
ndio maana nimesema aende na mwenzi wake.. hakuna ulazima wa kwenda pale na kutoa machozi ya "I wish".. on the other hand, in times of needs you never know.. wanaweza kuanzisha uhusiano wenye mafao..
Ila hii maana yake ndio nini "in times of needs you never know.. wanaweza kuanzisha uhusiano wenye mafao".....
MM, onyesha busara...unajua hata sisi tunataka kujifunza from here!???maana ni kwamba wakati wa mahitaji they could have a relationship with benefits of sorts.
MM, onyesha busara...unajua hata sisi tunataka kujifunza from here!???
Wewe changia tu bana...huwezi jua....anaweza akakupa tena ummege siku akiboreka na huyo mumewe mpya
kwa sababu uliwahi kumpenda na ameamua kuachana na wewehata kama hukuwa tayari hujui ni mangapi ambayo amekuepusha nayo. Kuna mahali fulani panasema "mshukuruni bwana kwa kila jambo na furaha yenu ijulikane kwa watu wote". Sasa, uushine uchungu kwa msamaha.
Msamahe na usimshike mateka ndani ya moyo wako. Na uamue kumuacha moyoni mwako ili aende huko alikokwenda. Si wako tena na haisaidii kuendelea kumshikilia kwenye gereza lako.
So.. kwa furaha.. get kama laki moja hivi.. mchangie.. na wakikupa mwaliko wa kwenda nenda na mwenzi wako mpya and get over her! kwa sababu.. sasa hivi yawezekana umekuwa ukiombea kuwa one "day she will come back to you". She won't.
Kumbuka kuwa mkivuliana nguo, hata siku moja hamuhachani kamwe, hivyo mchangie na wewe utakuwa nyumba ndogo yake, na kuna wengine wanafikia kuwa matroni au best man siku ya harusi sembuse kuchangia harusi tu.