Mpenzi wangu wa zamani anaomba nimchangie kwenye harusi yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpenzi wangu wa zamani anaomba nimchangie kwenye harusi yake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Regia Mtema, Mar 9, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu.
  Niliwahi kutoa sredi hapa kwamba nilikuwa na mpenzi wangu ambaye alikuwa wa kwanza nilikutana naye nikiwa chuo tukaachana siku ya wapendanao..Jamaa yangu huyu anatarajia kufunga pingu za maisha mwezi wa tano mwaka huu.Siku chache zilizopita alinipigia simu na kuniambia kwamba anatarajia kufunga pingu za maisha na kuniomba nimchangie ili kufanikisha harusi yake.ikumbukwe kwamba hatkumalizana vizuri na huyu jamaa ingawa amekuwa akilazmisha mara nyingi kwamba tuwe best friends,hili alilisema hata wakati tunaachana lakini kwangu mimi niliona ni upuuzi,sikujisikia kuwa karibu naye hasa kirafiki ingawa tumekuwa tukiwasiliana kwa njia ya simu mara moja moja kila mtu akimkukmbuka mwenzake.Nilimueleza bila kuficha kwamba sitamchangia hata senti moja kwani sijisikii kufanya hivyo.Ikumbukwe kuwa tuliachana tukiwa hatujagombana hata kidogo wala kuwa na makosa ya kupelekea kuachana.
  Naombeni ushauri nafanya vibaya kutomchangia?
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red maelezo yako yanajichanganya! Kwa Kinyamwezi tunaita ''double standards''!
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hkuna tatizo hapa bana,we changia tu
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kama hujisikii kwenda usichange. as simple as that.
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Pia anaweza kumchangia na aisende tu,sidhani hata kama kuna haja ya kuomba ushauri katika hili.......Hasa ukizingatia waliachana kwa amani
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mie staki kuwa mnafiki kw akweli, hata sikumoja sitajilazimisha kuchangia harusi ya mtu kama nina kikwazo cha aina yoyote ile
  so if you feel like doing that, do vinginevyo usifanye
  ya nini kumchangia mtu huku unaumia moyoni......
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Mar 9, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Wewe changia tu bana...huwezi jua....anaweza akakupa tena ummege siku akiboreka na huyo mumewe mpya
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  eeeh kumbe wanyamwezi wanongea kiivo??
   
 9. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Yeah! Muulize Sikonge atakwambia!
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Navyo elewa mahawara wengi huwa hawaachani wewe mchangie tu bana unaweza fikiriwa dili la kuzibua masikio mtoto.
   
 11. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,442
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Usiharibu mazingira bali jenga mazingira,unaweza kupata hitaji la kupunga upepo siku moja hapo bustanini,who knowz. Fanya fair play kwa kuchangia kisha kuhudhuria harusini ni uamuzi wako kwenda au upotezee.
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Ni situation ngumu kidogo
  Ushauri wangu fanya kile moyo wako unavyokutuma

  ila nina swali
  Umesema hamkumalizana vizuri na huyo jamaa yako wa zamani, swali linakuja ulitaka mmalizanaje vizuri? Please tuweke wazi kumalizana vizuri kivipi?
   
 13. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  what wrong with kuchangia/ no big deal au bado una feelings?
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nadhani hapa hujanielewa.Ni hivi tuliachana nikiwa bado na namhitaji na hatukugombana popote ila yeye akadai anataka tusiendelee kuwa wapenzi lakini tuwe marafiki wa karibu.Personally sikulikubal hili kwani nilikuwa bado namhitaji na hatukugombana popote..Hivyo kwangu mimi hatukumalizana vizuri kwani sikukubali proposals zake zote mbili za kuachana na za kuwa bset friends.
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Kwanza kamalizaneni, then mchangie kwa roho nyeupe!
  hapo kwenye red panahusika sana.
  you are in conflict with your feeling....wanaitaga denial sijui?
   
 16. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mpendwa, sijui kama wewe ni muumini wa dhehebu gani, lakini mie nina ushauri hapa......................

  1.
  yeye kaomba umchangie-kama una uwezo wa kuchanga, mchangie kwa msingi wa ombi lake na kulingana na uwezo wako, usije ukalaza watu wa nyumbani mwako na njaa kwa sababu ya kuchangia harusi hii, kumbuka kila aombaye hupokea, je tukiwasaidia wale tu walio wapenzi wetu, tutapata ama kustahili thawabu gani ya ziada? mafarisayo na wenye dhambi na watu wa mataifa nao hawafanyi hivyohivyo? hakika haki yetu lazima ipite haki ya mafarisayo, watoza ushuru na wenye dhambi, vinginevyo hatuwezi kuurithi ufalme wa Mungu.

  2.
  ushinde ubaya kwa wema-kwa kuwa unakiri kuwa hukumkosea, lakini bado Mungu anampa fursa na ujasiri wa kukutafuta na kuomba umuunge mkono au umsaidie, kumbuka unapaswa kuushinda ubaya kwa wema. kwa wema wako atatambua kosa lake la kumkataa mke mwema na pamoja na kuwa huna tena nafasi kwake, lakini atayasimulia matendo yako makuu siku zote za maisha yake na kufanyika baraka mlangoni mwako maisha yake yote na hivyo Mungu kutukuzwa kupitia maisha yako.

  3.
  kushiriki ama kutoshiriki harusi nashauri usikilize dhamiri yako inataka nini. mimi ningeshauri ushiriki kama na nafasi na usiwe kwazo katika shughuli yao ile kwa namna yoyote bali ufanyike baraka. si mbele yake bali mbele za Baba yetu aliye mbinguni. atakapoziona baraka kupitia kwako, atamshukuru Mungu na kumuinua siku zote za maisha yake na ataamini kuwa kweli wewe ni mtoto wa Mungu kwani unakata mashauri kwa jinsi ya Mungu na si kwa jinsi za wanadamu. kumbuka tena mpendwa kuwa haki yako mbele za Mungu lazima ipite haki ya afarisayo na wenye dhambi ili kustahili thawabu

  thamani ya ushauri huu itategemea imani yako na kiwango cha uchaji wa Mungu ulichonacho.............ni hayo tu mpendwa........................... unarikiwe na Bwana
   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hapo mkuu una mfumo dume. Kama ye ndo wa kumegwa itakuwaje?
   
 18. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mi nionavyo huna haja ya kumchangia, hiyo harusi itafanyika tu, kwani ana maana gani kukuomba mchango? si mliachana? achukue time.
   
 19. F

  FM JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani ameombwa mchango wa kufanikisha harusi, siyo achangie ili aende!
   
 20. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mkuu nimekukubali! hiyo namba mbili mwakemwake.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...