Mpenzi wangu wa zamani anaomba nimchangie kwenye harusi yake

Status
Not open for further replies.
mpendwa, sijui kama wewe ni muumini wa dhehebu gani, lakini mie nina ushauri hapa......................

1.
yeye kaomba umchangie-kama una uwezo wa kuchanga, mchangie kwa msingi wa ombi lake na kulingana na uwezo wako, usije ukalaza watu wa nyumbani mwako na njaa kwa sababu ya kuchangia harusi hii, kumbuka kila aombaye hupokea, je tukiwasaidia wale tu walio wapenzi wetu, tutapata ama kustahili thawabu gani ya ziada? mafarisayo na wenye dhambi na watu wa mataifa nao hawafanyi hivyohivyo? hakika haki yetu lazima ipite haki ya mafarisayo, watoza ushuru na wenye dhambi, vinginevyo hatuwezi kuurithi ufalme wa Mungu.

2.
ushinde ubaya kwa wema-kwa kuwa unakiri kuwa hukumkosea, lakini bado Mungu anampa fursa na ujasiri wa kukutafuta na kuomba umuunge mkono au umsaidie, kumbuka unapaswa kuushinda ubaya kwa wema. kwa wema wako atatambua kosa lake la kumkataa mke mwema na pamoja na kuwa huna tena nafasi kwake, lakini atayasimulia matendo yako makuu siku zote za maisha yake na kufanyika baraka mlangoni mwako maisha yake yote na hivyo Mungu kutukuzwa kupitia maisha yako.

3.
kushiriki ama kutoshiriki harusi nashauri usikilize dhamiri yako inataka nini. mimi ningeshauri ushiriki kama na nafasi na usiwe kwazo katika shughuli yao ile kwa namna yoyote bali ufanyike baraka. si mbele yake bali mbele za Baba yetu aliye mbinguni. atakapoziona baraka kupitia kwako, atamshukuru Mungu na kumuinua siku zote za maisha yake na ataamini kuwa kweli wewe ni mtoto wa Mungu kwani unakata mashauri kwa jinsi ya Mungu na si kwa jinsi za wanadamu. kumbuka tena mpendwa kuwa haki yako mbele za Mungu lazima ipite haki ya afarisayo na wenye dhambi ili kustahili thawabu

thamani ya ushauri huu itategemea imani yako na kiwango cha uchaji wa Mungu ulichonacho.............ni hayo tu mpendwa........................... unarikiwe na Bwana
Namshukuru Mungu aliyekufunulia kunena haya! Ubarikkiwe sana!!
 
Nawashukuru wote mliochangia mawazo yenu.kwa kweli bado niko njia panda,natafakari lipi nifanye,nichange ama la na je nikichanga niende kwenye harusi au nisiende.Nikaamua rasmi lipi lakufanya nitawajulisheni.Asanteni once again.
 
Mpendwa usiwe hivyo mchangie tena ukipewa kadi nenda kwenye harusi yake onyesha uungwana vinginevyo inatia wasiwasi huenda bado una wivu naye? Mchangie na toa ushirikiano wote anaotaka ndiyo uungwana kwani huwezi jua haya maisha huenda ukafika siku nwe au mwanao akahitaji msaada kwake pengine ukaenda ofisi ukamkuta ndiyo mtu muhimu wa kutatua tatizo lako utajisikia faraja sana hata naye atafarijika sana kukusaidia,ndiyo maana siku zote sipendi wanaoachana kwa zogo na ugomvi hawtumii busara kabisa kuna leo na kesho wakumbuke
 
Thread yako ya kwanza niliisoma. Mi naamini huyu mtu unamchukuia kuliko maelezo ingawa bado unampenda kuliko inavyoweza kutamkwa, sijui ndiye aliyekuingiza ktk dunia hii ya ufisadi (mapenzi). Na kwasababu hiyo nakushauri kata shauri sasa kama mmeachana basi mfute kabisa ktk mutwe wako kabisa.
 
kwa sababu uliwahi kumpenda na ameamua kuachana na wewehata kama hukuwa tayari hujui ni mangapi ambayo amekuepusha nayo. Kuna mahali fulani panasema "mshukuruni bwana kwa kila jambo na furaha yenu ijulikane kwa watu wote". Sasa, uushine uchungu kwa msamaha.

Msamahe na usimshike mateka ndani ya moyo wako. Na uamue kumuacha moyoni mwako ili aende huko alikokwenda. Si wako tena na haisaidii kuendelea kumshikilia kwenye gereza lako.

So.. kwa furaha.. get kama laki moja hivi.. mchangie.. na wakikupa mwaliko wa kwenda nenda na mwenzi wako mpya and get over her! kwa sababu.. sasa hivi yawezekana umekuwa ukiombea kuwa one "day she will come back to you". She won't.
 
Lakini kwa nini mtu utake kwenda kwenye harusi ya ex wako? Mimi kama naoa sitafurahia hata kidogo kuwaona ma ex wa mke wangu mtarajiwa. Mambo gani haya...yaani unaiona njemba iliyokuwa inamega mke wako mtarajiwa? Mambo mengine ni hapana kabisa aisee. Kama mtu mmeshaachana basi ni bora kuendelea na maisha yenu kivyenu vyenu. Mambo ya kuendeleza ties na ma ex ni chanzo cha mizozo ktk ndoa au uhusiano wenu. Hayafai.
 
ndio maana nimesema aende na mwenzi wake.. hakuna ulazima wa kwenda pale na kutoa machozi ya "I wish".. on the other hand, in times of needs you never know.. wanaweza kuanzisha uhusiano wenye mafao..
 
ndio maana nimesema aende na mwenzi wake.. hakuna ulazima wa kwenda pale na kutoa machozi ya "I wish".. on the other hand, in times of needs you never know.. wanaweza kuanzisha uhusiano wenye mafao..

Mmmh..okay...I guess I have learned a lot from experience and experience has taught me that it wise to cut all ties with your ex partners (in the event there are no kids involved) because otherwise it will come back and bite you in your new relationship. But at the end of the day to each his/her own...

Ila hii maana yake ndio nini "in times of needs you never know.. wanaweza kuanzisha uhusiano wenye mafao".....
 
Wewe funga macho, tia mkono mfukoni toa mchango.....You never know, pengine unainvesti samsing hapo...ohooo wee shauri yako tu... :D
 
Mchangie tu na nakushauri kuwa rafiki does not cost you a shilling. Unless sababu zake ziwe ni zile zile za kutokubaliana na uamuzi wake wa kuoa mtu mwingine. Maana mambo ya maisha bwana, hujafa hujaumbika. Huwezi jua nini kiko mbele yake na yako! Kuwa na marafiki wengi ni muhimu sana.
 
Usilipe BAYA kwa BAYA maana MABAYA hayataisha nyumbani kwako.... Mimi nakusihi MCHANGIE utakuwa umempalia makaa ya moto kichwani pake.. Kama alikuwa anakujaribu, shauri yake.
 
Si uchange tuu na ili ikuweke kwenye mood nzuri fikiria the good times you had and not the ones.
 
Wewe changia tu bana...huwezi jua....anaweza akakupa tena ummege siku akiboreka na huyo mumewe mpya

sijawahi kuona double standard ya maneno kama hii, we Ngabu umelogwa, kuchanga au kutochanga ni hiari na wala sio lazima eti mtu ulikuwa na uhusiano nae, mimi naona kama jamaa hatachanga ataonyesha inferiority complex kwa huyo mwanamke, na wala moyo wake ucwe na hata chembe ya hisia kuwa what happen in the past then itumike kama excuse, hell no, man we changa tu, huo ndo utakuwa wamuuzi wa busara, never on the earth ukalipaiza baya kwa baya, you never know huyo huyo ataweza kukuokoa na maswahiba mengine mbele ya maisha yako, usiwe mtu wa visasi kamanda.
 
Kumbuka kuwa mkivuliana nguo, hata siku moja hamuhachani kamwe, hivyo mchangie na wewe utakuwa nyumba ndogo yake, na kuna wengine wanafikia kuwa matroni au best man siku ya harusi sembuse kuchangia harusi tu.
 
kwa sababu uliwahi kumpenda na ameamua kuachana na wewehata kama hukuwa tayari hujui ni mangapi ambayo amekuepusha nayo. Kuna mahali fulani panasema "mshukuruni bwana kwa kila jambo na furaha yenu ijulikane kwa watu wote". Sasa, uushine uchungu kwa msamaha.

Msamahe na usimshike mateka ndani ya moyo wako. Na uamue kumuacha moyoni mwako ili aende huko alikokwenda. Si wako tena na haisaidii kuendelea kumshikilia kwenye gereza lako.

So.. kwa furaha.. get kama laki moja hivi.. mchangie.. na wakikupa mwaliko wa kwenda nenda na mwenzi wako mpya and get over her! kwa sababu.. sasa hivi yawezekana umekuwa ukiombea kuwa one "day she will come back to you". She won't.

Ndio kweusi sawa, lakini kwenye red, no, no, no, kabisa!
 
Kumbuka kuwa mkivuliana nguo, hata siku moja hamuhachani kamwe, hivyo mchangie na wewe utakuwa nyumba ndogo yake, na kuna wengine wanafikia kuwa matroni au best man siku ya harusi sembuse kuchangia harusi tu.

Kaitaba,hapa hapana.Unasema mivuliana nguo hamuachani kamwe?hee.how this wil be possible?to me ni big no!
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom