Wala hauko Njia panda mkuu, mbona upo njia kuu tena high way!! We umeoa sasa X wa nini? Kama ni safari mwambie akutumie nauli za watu wawili wewe na mkeo uende nae! Geuza hayo mawazo yako na situation yako kwa mkeo,
kuwa ana X wake yupo nje na bado anampenda na anahitaji kumtumia ticket aende akamuone! How would you feel and react??? Usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwenzio! Mkeo ana thamani kuliko hata hizo zawadi unazotumiwa na huko nje aliko huyo X wako.
Nakushauri usiwe na urafiki na ma X! Hakunaga urafiki kwa waliowahi kupendana wakaachana, utavunja ndoa yako ama kuleteana magonjwa maana hata mkeo anao ma X wake!