Mtanzanyika
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 368
- 425
Habari za jioni wana MMU,
Mimi ni mfanyakazi katika benki moja maarufu nchini, nafanya kazi katika moja ya matawi yake mkoani Mwanza. Nimeoa na nimebahatika kupata watoto wawili. Mke wangu ni mtumishi wa umma yeye ni mwalimu wa moja ya shule za Sekondari hapa mkoani Mwanza.
Sasa kuna msichana mmoja niliwahi ku-date naye kipindi hiko nipo Chuo kikuu cha Mzumbe, miaka 7 iliyopita. Yeye alikuwa anasoma LLB kwa bahati mbaya aka-disco first year, kwa kuwa wazazi walikuwa vizuri kifedha akaenda kusoma chuo Marekani. Sasa alivyoenda kule tukawa bado tunawasiliana, yeye alisoma Bachelor na kuunganisha na Masters moja kwa moja.
Tuliendelea kuwa na mawasiliano kwa takribani miaka 2 then baadaye mawasiliano yakapungua taratibu na baadaye kukatika kabisa.
Sasa siku ya Ijumaa kuu nikiwa kanisani kwenye ibada wakati wa kuabudu msalaba nikamuona huyo msichana, nilistuka sana kwa kweli maana sikutegemea kuonana naye.
Nikamfuatilia kwa macho mpaka nikafanikiwa kumuona mahali alipoketi, baada ya ibada kuisha nikajisogeza eneo alipo na kuonana naye, kwa kweli tulishangaana sana na kutoamini macho yetu kama tumeonana tena.
Tuliongea mambo mengi sana na kuahidiana kuonana Jumatatu ya Pasaka ili kuongea kwa kirefu. Tukaachana pale kanisani kwa kila mtu kuingia kwenye usafiri wake na kuondoka.
Sasa Jumamosi mke wangu akaniambia kuna rafiki yake anataka kuja Pasaka nyumbani maana ni miaka mingi hawajaonana na yupo Mwanza. Nikamuambia it's ok mkaribishe sana.
Basi J2 ya Pasaka nikiwa nimetulia nyumbani mke wangu akifanya maandalizi ya chakula huyo rafiki yake akaja, yaani wana MMU sikuamini macho yangu maana alikuwa ni yule yule ex - girlfriend wangu wa Mzumbe tuliyekutana kanisani, kila mmoja kati yetu alistuka sana na kupigwa na butwaa la ajabu, mpaka mke wangu akashtuka sana na kutuuliza kama tunafahamiana.
Ikabidi tumwambie ukweli kwamba tunafahamiana tulisomaga wote chuo Mzumbe, basi tukapiga story pale na kushinda naye kutwa nzima mpaka mida ya jioni alipotuaga na kurudi kwake.
Basi kesho yake Jumatatu ya pasaka tukaonana kama kawaida, tuliongea mambo mengi sana na akanipa hongera kwa kuwa na familia na akamsifu mke wangu kuwa ni mwanamke mwenye tabia njema sana.
Ila sasa nikashangaa sana aliponiambia kwamba bado ananipenda sana na anahitaji tuendelee kuwa wote japo mimi nina mke na watoto wawili. Mimi nikamuambia ni jambo ambalo haliwezekani coz tayari nina familia na ninampenda sana mke wangu na kumheshimu. Akaniambia nikafikirie vizuri then nimjibu baada ya kutafakari, tukaagana na kuachana pale kila mtu akarudi kwake.
Sasa nikafika nyumbani nikaweka simu yangu chumbani na mimi nikawa nipo sebuleni naangalia TV na wanangu. Mara simu yangu ikawa inaita mke wangu aliyekuwa chumbani anapanga nguo akaichukua akawa ananiletea sebuleni, jina limeandika la yule rafiki yake. Nikapokea na kuongea naye akawa ananiuliza kama nimefika salama nikamwambia ndiyo.
Nilivyomaliza kuongea naye mke wangu akaniomba simu yangu nikampa, kumbe akaichukua kuprove ile namba kama kweli ni ya rafiki yake, kwa bahati mbaya kulikuwa na sms mbili kumbe zimetumwa akafungua akazisoma moja ilisema "Nimefurahi sana kuonana tena na wewe leo nimekumbuka mbali enzi za Mzumbe tukiwa kwenye penzi moto moto, nilikumiss sana mpenzi, japo umeshaoa nazidi kukuomba usinisahau".
Ndugu wana MMU hivi ninavyoandika thread hii, tangu juzi mke wangu amenuna na hataki kabisa kuniongelesha wala kunisemesha. Nimejitetea vya kutosha mke wangu hataki kunielewa, nmemwambia hadi huyo ex - girlfriend wangu ampigie mke wangu na amuombe radhi lakini mke wangu bado hataki kunielewa kabisa. Anahisi bado natoka na huyo msichana na anahisi hiyo juzi tulienda kufanya mapenzi.
Naombeni ushauri wana MMU, nampenda sana mke wangu na sikuwahi kumvunjia heshima hata siku moja. Ebu nishaurini nifanye nini ndugu yenu, kazi haziendi ofisini, nipo na mawazo sana.