Mpenzi wangu mpya anauza majeneza

Mpenzi wangu mpya anauza majeneza

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,533
Reaction score
3,837
Wakuu,

Nimekuwa na huyu kwenye mahusiano kwa muda wa miezi sita sasa. Ana duka la vifaa vya simu maeneo ya Kariakoo na ndio hapo tulipofahamiana

Nilikuwa sifahamu mpaka leo nilipomuuliza upo wapi? Akasema nipo kuchukua mzigo umefika tokea wiki iliyopita, nikasema nakuja (nafahamu kampuni ambayo huwa inamletea mizigo yake). Akawa anakataa, nikasema poa. Nikahisi atakuwa na mwanaume, ikabidi niende kimya kimya.

Kufika nakuta kuna canter inapakia majeneza, nikamuuliza mzigo wako upo wapi? Akasema ndio huo hapo, nikawa mdogo kama piritoni.

Kumbe ana frem pale Muhimbili, huwa anaagiza majeneza China na Thailand. Nilitaka kula mzigo leo, sina hata hamu dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1st

Sasa wewe hapo tatizo lako nini?

Hiyo ni biashara tu

Hebu nipe namb yake anipe kazi ya kuwa namsogezea hiyo mizigo ikifika.
 

Ukaona atakuuzia na wewe? Hiyo si ni biashara tu kama biashara zingine jamani!!!
 
Mkuu ulitaka auze rozari..

However you may not start conversation with the following recipient;Tairus
 
Back
Top Bottom