Mpenzi wangu mpya anauza majeneza

Mpenzi wangu mpya anauza majeneza

Wakuu,

Nimekuwa na huyu kwenye mahusiano kwa muda wa miezi sita sasa. Ana duka la vifaa vya simu maeneo ya Kariakoo na ndio hapo tulipofahamiana

Nilikuwa sifahamu mpaka leo nilipomuuliza upo wapi? Akasema nipo kuchukua mzigo umefika tokea wiki iliyopita, nikasema nakuja (nafahamu kampuni ambayo huwa inamletea mizigo yake). Akawa anakataa, nikasema poa. Nikahisi atakuwa na mwanaume, ikabidi niende kimya kimya.

Kufika nakuta kuna canter inapakia majeneza, nikamuuliza mzigo wako upo wapi? Akasema ndio huo hapo, nikawa mdogo kama piritoni.

Kumbe ana frem pale Muhimbili, huwa anaagiza majeneza China na Thailand. Nilitaka kula mzigo leo, sina hata hamu dah

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila kukosea wewe ni mwajiriwa wa sekta duni kabisa hapa nchini, au huenda hata kazi huna. Kiufupi huyo "dem" siyo size yako, huyo ni mchakarikaji mwenye kipato chake. Endelea kuyaogopa majeneza, siku ukifiwa utayatafuta mwenyewe.
 
Badala ya kuogopa zinaa uliyotaka kufanya unaogopa jeneza ambalo taka usitake siku moja utaingia. Anza kulizoea brother!
 
Wakuu,

Nimekuwa na huyu kwenye mahusiano kwa muda wa miezi sita sasa. Ana duka la vifaa vya simu maeneo ya Kariakoo na ndio hapo tulipofahamiana

Nilikuwa sifahamu mpaka leo nilipomuuliza upo wapi? Akasema nipo kuchukua mzigo umefika tokea wiki iliyopita, nikasema nakuja (nafahamu kampuni ambayo huwa inamletea mizigo yake). Akawa anakataa, nikasema poa. Nikahisi atakuwa na mwanaume, ikabidi niende kimya kimya.

Kufika nakuta kuna canter inapakia majeneza, nikamuuliza mzigo wako upo wapi? Akasema ndio huo hapo, nikawa mdogo kama piritoni.

Kumbe ana frem pale Muhimbili, huwa anaagiza majeneza China na Thailand. Nilitaka kula mzigo leo, sina hata hamu dah

Sent using Jamii Forums mobile app
HAHAHAHAHAHAHAH
AKYANANI
UUUWI
WE KULA TU BABA SI UMEMPENDA!
UKIPENDA BOGA PENDA NA MAJENEZA YAKE
CC: 50thebe
 
Write your reply... firimasoni huyo bro, mda wote anaomba wagonjwa wafe ili apge pesa
 
kuna dada mmoja anauza majeneza pale muhimbili(kwa heshima sitaji jina la duka lake) ..aisee ni mzuri ile mbaya,ni watu wa fani ya mapambo muda mrefuu hapa dar,nadhani ni kampuni iliasisiwa na baba yake ambaye alifariki miaka sio mingi..ila yule nadhani kaolewa
 
Back
Top Bottom