Mpenzi wangu kanisingizia nimemuibia

Mpenzi wangu kanisingizia nimemuibia

Alitaka tu arudishe pesa aliyokurudishia... Usimtafute wala nini! Muache roho imsute
 
Kwan mnamazoea yakukopeshana pesa mara kwa mara?? Maana kuna wapenzi wengine mnakopeshana vizur lakin siku yakulipa anakulipa kwakinyongo yaan anahisi kama vile ukupaswa kumkopa bali ulipaswa umpe bila bure sasa yawezekana alipokwambia uende pesa yako alikuwa anajua utamjibu kuwa abaki nayo tu au ungechukua nusu naingine ungemwachia
 
Kwan mnamazoea yakukopeshana pesa mara kwa mara?? Maana kuna wapenzi wengine mnakopeshana vizur lakin siku yakulipa anakulipa kwakinyongo yaan anahisi kama vile ukupaswa kumkopa bali ulipaswa umpe bila bure sasa yawezekana alipokwambia uende pesa yako alikuwa anajua utamjibu kuwa abaki nayo tu au ungechukua nusu naingine ungemwachia

Hiyo tabia wanayo madem wengi, yan swala la kuwapa wapenz wao hela halipo kwenye kamusi yao flulanga
 
Jana mpenzi wangu aliniita kuchukua hela niliyomkopesha. Ilikuwa tsh 100,000. Nilikaa kidogo, baada ya kunipa hio hela nikaondoka. Baadae jioni, masaa ma4 hivi akanipikia kuwa ameibiwa hela na anahisi ni mimi. Bahati nzuri ile hela alonipa bado nilikuwa nayo. Nikaenda nikamkuta na rafiki zake.

Waliponiona wakatoka nje kidogo wakaongea alafu yeye akarudi ndani kwake, marafiki zake wakaingia vyumbani kwao. Nikamuuliza nini kinaendelea. Akanambia ameibiwa tsh 80,000. Na anahisi ni mimi. Nikwamwambia sijachukua hela yake, na sijawahi kuiba hela wala kitu cha mtu. Akasisitiza mimi ndo nimeichukua. Nikaona isiwe shida nikachukua tsh 80,000 nikampa akafanya kukataa.

Nikamwekea mezani nikaondoka. Nikabakiwa na tsh 20,000.

Leo asubuhi nimemjulia hali kwa SMS hajajibu.

Kama ni wewe ungefanyeje?
Hata Mimi nina wasiwasi kuwa ni wewe kwanini umerudisha?
 
Mtoa mada unabusara sana...umefanya vyema kumludishia...
 
Naumefanya la maana sana kumjulia hali asubhi uo ndo upendo wenyew..
 
Hata kumjulia hali ulkua unatafuta kiki.. Uez mcngzia mpnz wako amekuibia sababu unamuamni kwann ackuibie nanliu uibe hela labda anakujua wew mdokoz! Ila ningekua mm hapo ndo ingekua see you on the other side of the road
 
Jinga wewe yaani unampa 80 loooh ningekua Mimi ningesema asante na kwaheri ya kuonana.

Usirudie tena hafai kuwa mke huyo anatamaa ya pesa sana
 
Yaani huyo kakuchoka sema tu alikua anatafuta njia ya kukupiga chini,,,,, ndio zao hao wavulana wakishakinai
 
Mmesnzi lini kukopeshana na mpenzi wako? Kama kwenye tatizo hamsaidiani mnakopeshana basi tatizo lilianzia hapo, sasa sijui ukishamaliza kupiga game ndio unakumbushia deni lako..
 
Huyo hakuwa na nia ya kukulipa hiyo hela. Achana naye fanya mambo mengine.
 
80000/=unazitoa bila wasiwasi wowote, Duuuh, Mimi ningeanguka na kuzimia hapohapo.
 
Kwaiyo umeenda kudai laki kwa mpenzi wako.ni jinsia gani kwanza?
 
umefanyanya makosa makubwa sana ulivyompa 80 ulitakiwa ukate mawasiliano kabsa.....
 
wema ukitenda wema nenda zako weeeema wema ____________________.
 
Sasa umempa ya nini wakati hukuchukua hiyo hela nimekuonea huruma sana Mkuu.

Kupenda usipopendwa ni kazi kweli
 
Back
Top Bottom