ytara jr.
Member
- Feb 6, 2014
- 61
- 22
Jana mpenzi wangu aliniita kuchukua hela niliyomkopesha. Ilikuwa tsh 100,000. Nilikaa kidogo, baada ya kunipa hio hela nikaondoka. Baadae jioni, masaa ma4 hivi akanipikia kuwa ameibiwa hela na anahisi ni mimi. Bahati nzuri ile hela alonipa bado nilikuwa nayo. Nikaenda nikamkuta na rafiki zake.
Waliponiona wakatoka nje kidogo wakaongea alafu yeye akarudi ndani kwake, marafiki zake wakaingia vyumbani kwao. Nikamuuliza nini kinaendelea. Akanambia ameibiwa tsh 80,000. Na anahisi ni mimi. Nikwamwambia sijachukua hela yake, na sijawahi kuiba hela wala kitu cha mtu. Akasisitiza mimi ndo nimeichukua. Nikaona isiwe shida nikachukua tsh 80,000 nikampa akafanya kukataa.
Nikamwekea mezani nikaondoka. Nikabakiwa na tsh 20,000.
Leo asubuhi nimemjulia hali kwa SMS hajajibu.
Kama ni wewe ungefanyeje?