Mpenzi wangu kanisingizia nimemuibia

Mpenzi wangu kanisingizia nimemuibia

Ulimpatia kwa wale wadada Wa sinza nini.hawa wanawake Wa mjini ukiwachekea kidogo utarudi kijijini kwenu unalia
 
Ungeanza kuandika hivi,
Aliyekua mpezi wangu .......
maana huyo hafai tena kuwa mpenzi
au umeiba kweli jamaa
 
ha haha wewe kwa nini ukamdai ? ha ha ha amefanya janja yake kapata hela .. sasa muache tu
 
Jana mpenzi wangu aliniita kuchukua hela nliyomkopesha. Ilikuwa tsh 100,000. Nlikaa kidogo, baada ya kunipa hio hela nikaondoka. Baadae jioni, masaa ma4 hiv akanipikia kuwa ameibiwa hela na anahisi ni mimi. Bahati nzuri ile hela alonipa bado nlikua nayo. Nikaenda nikamkuta na rafiki zake. Waliponiona wakatoka nje kidogo wakaongea af yeye akarudi ndani kwake, marafiki zake wakaingia vyumbani kwao. Nikamuuliza nn kinaendelea,. Akanambia ameibiwa tsh 80,000. Na anahisi ni mimi. Nikwamwambia sijachukua hela ake, na sijawahi kuiba hela wala kitu cha mtu. Akasisitiza mm ndo nimeichukua. Nikaona isiwe shida nikachukua tsh 80,000 nikampa. akafanya kukataa. Nikamwekea mezani nkaondoka. Nikabakiwa na tsh 20,000.

Leo asubuhi nimemjulia hali kwa sms hajajibu.

Kama ni ww ungefanyeje.

Hahaha umeshaibiwa wewe
Una huakika huyo ni mpenzi wako
 
Huyo ni mwizi! Hata akijirudisharudisha baada ya roho kumsuta muweke kama spea tu ya kumalizia ukame ila si wa kutegemea
 
Alikuwa anakutafutia visa... ulipompa hiyo pesa kakosa sababu. Roho inamsuta jaribio lake limeshindwa..
 
yaan kuna watu wakisema ni wanaume unaanza kuutafuta uko wapi huo uanaume.
kwanza anakupigia simu umeniiibia na ww hujaiba unaenda unamlipa?
mie angejifunza kusoma nakuambia
na angejua nane ni sifuri zilizoungana ama ni tatu zilizogeukiana
Unadhani kati ya huyu jamaa na huyo dada nani mjinga? I'd have done the same, 80K kitu gani bwana. Hakuna kitu kibaya kama mtu mnayeaminiana kukuzushia uongo.

Tena ingekuwa mimi namwachia hiyo 100K kabisa, ataitumia miaka mingapi? Then that'd be it...
 
Mtoa mada you're right IMO, tena umemuaibisha huyo mpuuzi. Watu wajinga na waroho wa pesa hiyo ndio dawa yao, you won't lose sh!t

Ila muache, achana nae hakufai huyo.
 
Kila siku tunashauri dada zetu wawe wajasiriamali...she is just trying to be one!
 
Mimi nisingempa,kabisa maana najua kabisa sijaiba na ulivo mtumia sms hajakujibu huensa roho inamsuta kwa alicho kifanya
 
Umefanya kosa kubwa kumpa hiyo 80,000. Pole kwa kutapeliwa. Baadhi ya wanaume tabia zao zinasikitisha sana.

Jana mpenzi wangu aliniita kuchukua hela niliyomkopesha. Ilikuwa tsh 100,000. Nilikaa kidogo, baada ya kunipa hio hela nikaondoka. Baadae jioni, masaa ma4 hivi akanipikia kuwa ameibiwa hela na anahisi ni mimi. Bahati nzuri ile hela alonipa bado nilikuwa nayo. Nikaenda nikamkuta na rafiki zake.

Waliponiona wakatoka nje kidogo wakaongea alafu yeye akarudi ndani kwake, marafiki zake wakaingia vyumbani kwao. Nikamuuliza nini kinaendelea. Akanambia ameibiwa tsh 80,000. Na anahisi ni mimi. Nikwamwambia sijachukua hela yake, na sijawahi kuiba hela wala kitu cha mtu. Akasisitiza mimi ndo nimeichukua. Nikaona isiwe shida nikachukua tsh 80,000 nikampa akafanya kukataa.

Nikamwekea mezani nikaondoka. Nikabakiwa na tsh 20,000.

Leo asubuhi nimemjulia hali kwa SMS hajajibu.

Kama ni wewe ungefanyeje?
 
Back
Top Bottom